15/08/2025
WAZAZI WETU WALIKUWA WAKWELI β Tuwashukuru na Tuwaheshimu
ββββββββββββββββββββββββββββ
Kuna wakati katika maisha yetu, hasa tulipokuwa watoto au vijana, tulidhani kwamba wazazi wetu walikuwa wakitoa visingizio. Tulipowasikia wakisema:
βMwanangu, sina pesaβ¦ bado sijapata mshahara wa mwezi huu.β
π€¦πΎββοΈ Tuliishia kwa huzuni, au pengine tukajihisi kutelekezwa kabisa. Lakini leo, tukiwa tumeingia kwenye majukumu ya maisha, tunaelewa vizuri kwamba walikuwa wakituambia ukweli wa moyo wao.
Msanii maarufu duniani, Idris Elba, aliwahi kusema:
βWe all owe our parents an apology for not believing them when they said they donβt have money even on payday.β
Akimaanisha kwamba: ‡οΈ
βSote tunapaswa kuwaomba radhi wazazi wetu kwa kutowaamini walipotuambia hawana pesa, hata siku ya mshahara.β
ππΎ Kauli hii si maneno matupu β ni sauti ya ukweli inayotufikia moja kwa moja kwenye dhamiri. Wazazi wetu walikuwa askari wa mstari wa mbele katika mapambano ya maisha, wakipigana ili waweze kutupatia makazi, chakula, elimu, na hata furaha ndogo tulizoona k**a za kawaida sana.
π¨πΏβπΌ Walikuwa wanajinyima ili sisi tupate. Walikuwa wanavumilia njaa ili Sisi tule. Walikuwa wanavaa nguo zilizochakaa ili sisi tuvae vizuri shuleni. Lakini sisi tulichokiona ni kauli ya kuepuka majukumu tu.
π Leo hii, baada ya kupitia gharama za maisha, bili zisizopungua, na majukumu yasiyoisha, tunagundua kwamba hakuna mzazi aliyekuwa akidanganya. Bali wazazi walikuwa wanasema ukweli, ukweli ambao wakati ule sisi tuliuona k**a uongo.
π Hii leo, tuchukue muda kuwatambua k**a mashujaa wetu wa kweli. Tuwaombe radhi, tuwashukuru, na zaidi ya yote, tuwape heshima wanayostahili.
πΉ Kwa sababu nyuma ya kila βsina pesaβ kulikuwa na moyo uliojaa mapenzi, kujitolea, na kujitoa sadaka kwa ajili yetu.
π¬ Kumbuka: Shukrani isiyosemwa ni deni lisilolipwa.
π€²πΎππ» Usisahau kusambaza ujumbe huu Kwa marafiki zako ili na wao waweze kukumbuka Swala hili na waweze kuwashukuru wazazi wao.
Follow Baaqir Media na ‡οΈ
https://whatsapp.com/channel/0029Vb8HuEw9mrGcbCt1ts27