04/12/2025
Njia hizi zitakusaidia kupata Usingizi mzuri;
1.Punguza Matumizi ya mwanga wa Blue au vitu venywe mwanga mkali wakati wa siku,k**a vile kwenye Taa au simu,Computer,TV n.k.. Tafiti zinaonyesha kwamba mwanga wa Blue hupunguza uzalishaji wa Homoni au kichocheo aina Ya Melatonin ambacho ndyo huhusika na kuleta Usingizi.
2.Kaa kwenye Mwanga wa Kutosha wakati wa Mchana, Hii husaidia mwili wako kuweza kutofautisha wakati wa usiku ni upi na wakati wa Mchana ni upi,hivo kukusaidia wewe kupata usingizi mzuri wakati wa usku.
3.Matumizi ya Vinywaji vyenye Caffeine hasa wakati wa Usiku huuchangamsha mwili wako na kukusababishia kukosa Usingizi kabsa wakati wa Usku. Hivo epuka matumizi haya ya Vinywaji vyenye Caffeine wakati wa Usku.
4.Punguza tabia ya kulala wakati wa mchana,hii itakusaidia wewe kulala vizuri wakati wa Usku.
5.Inashauriwa kwa asilimia kubwa muda wa kulala na kumka kila siku uzingatiwe sana,hali hii huuzoesha mwili kwamba sasa ni wakati wa usku na ni wakati wangu wa kulala.
6.Epuka matumizi ya pombe au kilevi chochote,kwani hivi huathiri uzalishaji wa kichocheo au homoni hii ya Melatonin ambayo inahusika na Usingizi moja kwa moja.
7.Boresha Mazingira yako ya kulala,Tafiti zinaonyesha watu wengi wanaosumbuliwa na matatizo ya kukosa Usingizi, hulala kwenye vyumba ambao si rafiki mfano,Chumba ambacho kina mwanga sana,chumba chenye Joto sana,Chumba chenye baridi sana,Chumba ambacho kina makelele ya aina yoyote,mfano Redio au watu.
8.Epuka matumizi au ulaji mwingi wa chakula wakati wa usiku,pia Epuka kula vyakula vizito sana wakati wa Usku.
9.Pumzisha akili yako na iburudishe na vitu k**a Mziki laini n.k kabla Ya kulala na epuka kutazama vitu k**a Movies ndefu za kutisha wakati wa usku
10.Hakikisha umeoga kabla ya kwenda kulala Au kuupumzisha mwili wako kitandani.
11.Fanya mazoezi kila siku wakati wa mchana kabla siku yako haijaisha au kabla hujaenda kulala kitandani
12.Epuka kunywa kwa wingi vimiminika,kwani vitakufanya uanze kuamka amka mara kwa mara wakati wa usku,hivo kupelekea kukosa usingizi mzuri.