10/10/2020
SIMULIZI FUPI: NITARUDI
MTUNZI: JACOB NZOWA
MWANDISHI: JMB 23
MWAKA: 2020
MAWASILIANO: 0716579834
******* KWENYE MAISHA JITAHIDI SANA KUWA NA MSIMAMO KATIKA MAMBO YAKO, SIYO YOTE YANAYOSEMWA AU KUFANYIWA NA FULANI NAWE UYAFANYE AU UYAFATISHE.... KWA MAANA HATA WASWAHILI WALISEMA “ MIRUZI MINGI HUMPOTEZA MBWA”**
Mbele ya nyumba moja ya kifahari alionekana bwana mmoja mbele ya nyuma akiwa amezunguukwa na watu k**a wanne wakiwa na vifaa maalumu vya kuandikia wakiwemo na polisi wakiwa na pingu, huku kwengine walijazana majilani kushuhudia lile tukio.
Yule bwana alitambulika kwa jina la SUDI alionekana kuomba wampe hata wiki mbili aweze kuwalipa wale mabwana maana biashara yake haikuenda vizuri kwaiyo izo week mbili anaweza akapata hela yake na kuwalipa, lakini kwa upande wa pili anao waomba msamaha hawakuwa na mda nae, wakampa amri moja tu.
~ unaondoka au huondoki~
~ naondoka~ alijibu bwana sudi huku mkewe akiwa anaangalia tu hakuwa na lakufanya wala kuongea.
~ tunakupa dakika 10 uwe ushatoa mabegi yako ya nguo na usichukue kingine chochote~
sudi hakuamini aliachoambiwa lakini ndio hivyo haikuwa ndoto akaenda ndani na mkewe wakachukua nguo zao, kwa bahati nzuri sadi alikua na vijisenti vyake akavihifadhi na kutoka zao nje na mkewe, wale mabwana wakafanya mnada ile nyuma, lilikua jumba kubwa la kifahari.
Sudi na mkewe wakaondoka huku wakiangalia ile nyumba kwa mara ya mwisho mwisho, majilani waliwafariji lakini haikuleta faida yoyote wakaamua kujiondokea zao wakiwa njiani mkewe akambadilikia kibao mumewe, na kumwambia awezi kwenda kuishi maisha magumu kijiji kwaiyo amuache aende kijijini peke ake siku akipata hela atamfata.
Sudi alishangazwa na kauli ya mkewe akataka kumfokea nae mkewe akapandisha kibesi akaona isiwe tabu sudi akakubaliana na matokeo maana mdau huo alikua kashachanganyikiwa, akapanda kibajaji hadi stendi na kupanda gari la kijijini kwao.
Kwa upande wa mkewe nae akachukua simu yake na kumpigia hawala wake baada ya dakika kadhaa alifika na gari wakaondoka zao.
Sudi baada ya masaa kadha mida ya usiku alikua kijijini kwao, wazazi wake walimpokea kwa upendo wote na kumuasa kuwa aachane na mwanamke maana anaweza kumsababishia matatizo makubwa zaidi ya yale, bwana sadi aliweza kusikiliza ushauri wa wazazi wake lakini kwenye fikra zake alizidi kumkumbuka Yule mwanamke wake aliyebarikiwa sura nzuri na shepu namba nane,
lakini muda mwingine roho ilimuuma maana yeye ndiye chanzo cha yote kufilisika kwake hadi nyumba yake kupigwa mnada, akabaki kumshukuru Mungu.
Miaka ikaanza kwenda, mwaka wa kwanza , wa pili , watatu sudi akasahau kabisa kuhusu mkewe , akapata kibarua cha kuendesha tax ya mtu,biashara ile ya tax ilimkubali sana na alifahamika sana kwa jina la SUDI BISHOO maana alikua smart sana akinukia manukato mazuri mda wote.
Siku moja mida ya saa tatu alipata abilia wak**e akiwa amepaka MARASHI yenye harufu kali sana, hadi kichwa cha Sudi kilimuuma lakini akavumilia maana hawezi kumshusha mteja wake akakosa pesa kisa marashi.
Baada ya dakika chache yule mteja wake akaweza kufika mahali anapotaka, akashuka na kumkabidhi pesa elfu hamsini tathilimu .
“ dada mbona pesa kubwa sana hii , kutoka kule hadi hapa ni elfu kumi tu dada yangu” sudi aliikataa ile hela na kutaka kurudisha elfu arobaini.
“ hapana kaka angu chukua tu, ni haki yako iyo” yule mdada alijibu huku akiachia tabasamu mwanana akiwa na macho mregezo na sura mviringo ukimuangalia kwa haraka unaweza sema umekutana na malaika.
“daaah! Sawa dada angu kwakua umeridhia mwenyewe kunipa nashukuru sana”
“ usijali , ila samahani naweza kupata mawasiliano yako, ili atasiku nyingine nikitaka kuenda safari zangu nikuchue”.
“ ok usijali dada yangu, chukua kikadi changU cha namba hiki hapa” sudi alikijtoa na kumpa yule mdada, akakipokea yule mdada na kusoma jina la sudi.
“ unajina zuri, mimi naitwa Yusra “
“Ooh! Hata wewe unajina zuri mwanadada”
“ ahsante, ngoja nikuache basi , nitakutafuta sawa kaka”
‘ “sawa dada angu”
Sudi baada ya kuagana na yule mdada akageuza gari yake na kurudi kijiweni kwao huku akiwa na furaha tele akijiona amepata bahati ya mtendeni siku hiyo kwa maana biashara ilikua imemuendea vizuri, kwa maana alipata elfu arobaini bila kuitolea jasho.
K**a unavyojua vijana tunavyopenda majigambo, sudi alifika kwa wenzie na kuadisia wenzie jinsi alivyopewa pesa pamoja na kuombwa namba, wengine walimbeza wengine walimuonea donge, wengine walimsupport kwenye maongezi yake.
Wiki pili zilipita sudi hakutafutwa na yule mdada, lakini sudi nae hakuwa na kumbu kumbu k**a aliombwa namba na yule mdada ndipo siku moja akiwa anarudi zake usiku kwa ajili ya kuenda kupumzika ndipo akapigiwa na Yusra amfate mahali, hakuwa na wasi wasi aliweza kumfata ndipo akamkuta ametulia kwenye sehemu tulivu akijipatia maji na matunda tunda.
Sudi alipofika akakaribishwa na yule mdada hakuweza kukataa kwa kuwa kaombwa waliweza kula yale matunda huku wakipiga story muda ulipofika wa kuondoka wakaenda kwente tax na kuondoka zao, k**a kawaida ya yule mdada yusra aliposhuka akatoa kiasi cha juu,
Sudi nae alishazoea akashukuru na kuondoka zake, ila yule mwanadada alionekana anaduku duku moyoni mwake, lakini alikua anashindwa kulitoa akawa anatembea nalo kila siku.
Ndipo siku moja sudi alipoitwa na yule mwanadada Yusra akiwa pale pale mahali anapokulaga matunda, siku hiyo yusra akaamua kutoa duku duku lake alilokua anatembea nalo kila siku.
“ nakupenda sudi’
“ mmmmh!” sudi aliguna na kushindwa kusema lolote
“ mbona umeguna” yusra aliuliza huku akimuangalia kwa macho aibu sudi
“umenistua ulivyonambia ivo’”
“ kwani vibaya jamani kukupenda sudi’
“ hapana ! sijamaanisha ivo nimestuka kutoa hisia zako alafu mtoto wa k**e maana sisi wakiume ndiyo tumezoea kutongoza wanawake”
“ basi leo imekuwa tofauti’
“ sawa mimi sina neno kwakuwa umenitamkia mwenyewe haina shida ila daaah! Watoto wak**e nyie changamoto sana!”
“ kivipi sudi” yusra aliongea huku akimshika mkono wake sudi na kumfanya sudi asisimke kutokana na mikono laini ya Yusra.
“ nilishawai kuoa kabisa ila mke wangu alikua na hawala wake , hawala wake akamshawishi anifilisi ili wakaishi wote ndio mwisho wa siku ,
nikaja kufirisika na kurudi kijijini kwetu na kuanza maisha upya nikiwa sina mbele wala nyuma” sudi alisimulia kwa hisia kiasi cha kumfanya yusra aingiwe na huzuni.
“ pole sana sudi, nakuahidi sitokufanyia uliyofanyiwa na hautamkumbuka sawa”
“ sawa nimekuelewa”
“ok tuondoke” yursa akaomba waondoke, sudi hakuwa na shida wakatoka na kuingia katika Tax na kuondoka zao hadi mahali kwenye kiwanja cha mpira Yusra akaomba ashushwe pale kwa maana kwao siyo mbali na pale aliposhushwa.
“ jamani, si nikupeleke tu home kabisa”
“hapana mpenzi, nafika mwenyewe usijali, hadi hapa bei gani” yusra akauliza huku akitoa pochi yake ili atoe hela
“ hela ya nini mama, nimekuleta bure kabisa usijali hela nilizopata leo zinatosha” sudi akajitetea na kukataa hela za yusra.
“Hapana chukua tu hii elfu 30 kwa ajili ya mafuta” YUSRA alimsisitiza sudi Kuchukua ile hela ndipo sudi akakubali. Yule mwanadada akashuka zake na kutokomea gizani,
hata dakika moja haijapita sudi akajaribu kuwasha taa ili amuone yusra anapoenda cha ajabu yusra hakuonekana, alipatwa na mshangao kwa maana ni mda ule ule tu akajaribu kuenda mbele kuangalia labda yupo kwa mbele lakini hakumuona, wasi wasi ukamjaa na kuanza kupatwa na uoga akageuza gari lake na kuondoka zake.
Kile kitendo cha kupotea kwa Yusra kwenye macho yake hakuweza kunyamaza akaenda kuwasimulia wenzie, k**a unavyojua watu wa kijiweni kila mtu Ataongea Lake.
“Aaaah! Demu huli peke ako kaka wahuni wameenda kumla huyo hahahahaha!”
“ mmmh! Asiwe dem ni jini mshikaji tukaja kukukosa shauriako” hayo yote yalikua maoni mbali mbali ya washiaji zake hakuweza kuamini lipi ni sawa akaamua kuachana nayo yote.
Siku zikaanza kwenda, mahusiano ya sudi na yusra yalizidi kunoga lakini cha kushangaza sudi kila akiomba akutane na yusra kimwili hakuweza kukubaliwa kwa kigezo hadi wafunge ndoa,
sudi hakutaka kuteseka kisa utamu wa yusra, akajichanga changa na kufanikiwa kuoa mwanadada Yusra,, kwa upande wa Yursa waliweza kuja ndugu zake wawili tu kwenye harusi waliovalia nguo ndefu sana kuanzia chini hadi juu huku wakiwa na pete zinazong’aa sana halikua ni jambo la kushangaza kwa siku hiyo ya sherehe kwa maana kila mtu anajipamba anayotaka.
Maisha ya ndoa yakaanza kwa sudi na Yusra furaha na upendo ulitawala ndani yao, gafla maisha yalivyozidi kwenda sudi alizidi kunawili na kupata wateja wengi na kuanza kufanya biashara kubwa kubwa na kufikia kujenga jumba kubwa huku akiwa na biashara sehemu mbali mbali akiwa ameachana na kazi yake ya TAX DRIVER.
Maisha yalikua mazuri sana kwa sudi na mkewe hadi rafiki zake wakamuonea wivu kutokana na mizunguuko mingi ya biashara, ndipo sudi akamshauri Yusra waamie jijini dare s salaam itakuwa rahisi kwake kuendesha biashara zake,
jambo la kuamia dar es salaam halikua na shida shida ilikua ni kukutana kimwili kati ya Yusra na Sudi , Yusra hakuweza kumruhusu sudi kukutana nae kimwili, kile kitendo kilimkera sana sudi ndipo siku akamkalipia na kumtukana mkewe matusi makubwa makubwa.
Yusra alilia sana na kumwambia ukweli ya kuwa yeye sio mwanadamu basi ni mtoto wa malikia katika falme za majini na sharti lao kubwa ni kumsaidia mwanadamu na siyo kufanya nae mapenzi, sudi alitamani azimie baada ya kusikia anachoambiwa na Yusra ,
Kwa maana siku zote alikua anaishi na jinni bila ya yeye kujua, ila alichosisitizwa na Yusra asiweze kumwambia mtu yeyote iwe siri yake ataendelea kuwa na maisha mazuri.
Sudi mwanzoni haikuwa rahisi kuuukubali ukweli lakini siku zilivyozidi kwenda akaizoea ile hali huku moyoni akiwa na duku duku,
wazazi wake waliweza kumuuliza kuhusu watoto hakuweza kuwajibu jibu sahihi.
Miaka ikazidi kwenda ndipo akaanza kuchoka hali ile ya kutoa kuwa na mtoto ingali umri unaenda, siku moja akiwa zake katika mizunguuko ya biashara aliweza kustuliwa na mdada, alipomuuliza shida yake nini, ndipo yule msichana alipojitambulisha kuwa ni mkewa aliyeachana nae.
Sudi alimshangaa sana kutokana na hali dhohofu aliyokuwa nayo, alipomuuliza ndipo alipomwambia baada ya kuachana alienda kwa yule hawala wake, yule hawala wake alikua ni mtu wa kuruka viwanja hakuweza kutulia na mwanamke mmoja, alimtapeli mali zote na kutokomea pasipo julikana.
Kutokana na huruma aliyo nayo sudi aliweza kumsaidia kiasi cha pesa na kumuachia namba ya simu, akiwa na shida aweze kumsaidia k**a binadamu mwenzie.
Sudi aliweza kumsaidia mke wake wa zamani ila siku zilivyozidi kwenda wakaanza kujenga ukaribu sana, ndipo Yusra akiwa na mumewe akamuasa kuwa kuna hatari inamkaribia karibu yake , kwaiyo akae nayo mbali.
Hakuweza kumuelewa sudi na wala hakuyajali yale maneno , siku zilivyozidi kwenda ndipo sudi akazama kimapenzi upya na yule mke wake wa zamani na kumwambia siri zake zote kuhusu mkewa na sharti alilopewa, sudi alifanya yote bila yeye kujijua k**a alifanyiwa dawa na yule mke wake wa zamani.
Ndipo sudi kaanza kubadirika na kuanza kurudi usiku sana, na kumjibu mkewe, siku moja mkewe wa zamani akamshauri waende kwa mganga ili waweze kumuuwa yule mkewe jini ili wakifanikiwa waendelee kuishi pamoja na wazae watoto ili wazazi wake wawe na furaha.
Kutokana na akili za kushikiwa sudi akakubali na kupanga safari ya kwenda kwa mganga, siku iliyofuata sudi akaongozana na yule mke wa zamani na kwenda kwa mganga, walipofika kwa mganga wakasikilizwa na kupewa masharti ya kufanya ukiwepo kumtilia sumu yule mkewe , lile sharti halikuwa gumu kwa sudi kutokana na madawa aliyofanyiwa na yule mke shetani wa zamani.
Siku ya ijumaa, mida ya jioni sudi aliandaa mwenyewe chakula na kutegesha ile sumu , mkewe akiwa hajui hili wala lile, mda wa kula sudi akazuga anaenda kununua vinywaji mkewe aanzekula,ndipo akatoka zake na kufunga mlango kwa nje na kuondoka akaenda kulala kwa yule hawala wake.
Asubuhi na mapema aliweza kurudi zake na kukuta nyumba yake imetulia akafika kwenye mlango wa nyumba yake na kufungua mlango haku mtu akaingia ndani na kuangalia kila chumba hakumuona mtu yeyote, akaamua kurudi zake sitting room ndipo akasikia kicheko kikali kikiambatana na upepo mkali, sudi alichanganyikiwa akataka kutoka nje milango ikajifunga kisha kicheko kikakata.
Akaangalia huku na huku ndipo akaiona barua iko juu ya meza ya kioo akaenda kuichukua huku akiwa anatetemeka kwa hofu akaifungua na kukuta maandishi yaliyoandikwa kwa damu.
“ NILIKUPENDA SANA SUDI, NA KUJITOLEA KUKUSAIDIA NA KUKUAMBIA UKWELI WANGU,LAKINI HUKUTAKA KUNISIKILIZA UKAAMUA KUNIUA, ILA NITARUDI KWA AJILI YAKO NA SITA KUWA K**A MWANZO NILIVYOKUWA” ile barua ilisomeka vile sudi aliachnganyikiwa na kupiga makelele kwa uoga lakini hakupata msaada wowote.
Gafla akaanza kucheka cheka ovyo na kuongea peke ake akanyanyuka na kwenda mlangoni mlango ukafunguka na kutoka zake nje huku akianza kuvua nguo zake na kubakia na boxer.
Majirani zake walimshangaa sana na kuhisi labda kapatwa na uchizi, wakaamua kumk**ata na kumfunga kamba na kumuwahisha hospital, zile habari za kutembea bila nguo yule mke wake wa zamani alizisikia akaamua kwenda hospital na kumkuta mtu wake anacheka peke yake na kucheka cheka bila sababu.
Yule mdada alipoona vile akatoa taarifa kwa ndugu wa mwanaume kuhusu yaliyomkuta, alipohakikisha ametoa taarifa akatoka zake nje ili aende kuchukua pesa za kulipia gharama za kumlaza mgonjwa wao, akiwa njia anatembea gafla kilisikika kishindo kizito , watu walijazana kuangalia nini kimetokea ndipo wakamkuta yule mdada amegongwa na gari huku ile gari ikipotelea pasipojulikana.
Yule mdada akawaishwa haraka hospital lakini hakuweza kuvuta tena pumzi ya dunia alifariki akiwa njiani anawaishwa hospital,ndugu wa sudi waliweza kufika hospital na kukuta ndugu yao akiwahajielewi wakaamua kumchua na kuondoka nae kijijini kwa ajili ya matibabu.
Baaa ya siku mbili tatu, alipelekwa kwa mganga ndipo mganga akawaelezea kuwa sudi alikua anaishi na jini kutokana na kukiuka masharti ya yule jini na kumuekea sumu kwenye chakula ili afe ndiyo yamemkuta k**a wanavyomuona na kuhusu swala la tiba halitowezekana kwa maana yule jini anauwezo mkubwa sana, ndugu wa sudi hawakukubali kushindwa walizurula kwa waganga wengi sana lakini paligonga mwamba.
Mwisho wa siku ndugu wakachoka na kuamua kumueka sudi nyumbani, siku zilivyozidi kwenda sudi alizidi kubadilika na kudhofika kiafya Siku ya ijumaa mida ya usiku Sudi aliaga dunia akiwa anatoka damu puani na mdomoni.kule mjini mali za sudi zilipotea potea kwa mazingira ya kutatanisha hata ile nyumba haikuweza kuonekana pale mahali lipokuwa, siku zikaenda na kuhusu story ya sudi ikasahaulika kwenye vichwa vya watu.
********** MWISHO***********