04/09/2025
*Iba Siri Hii | Jinsi PID Inavyo mumunya Ndoto za Uzazi wako....*
Kuna ugonjwa mmoja ambao unatembea kimya kimya...
Unakula ndoto za ndoa, Unavunja tumaini la uzazi, na kugeuza furaha kuwa machozi...
*Umesikia nini kuhusu PID..!? (Pelvic Inflammatory Disease)* 🤔
Naam..! PID, Ni adui wa uzazi wa wanawake, Lakini cha kushangaza zaidi, Wanaume ndio chanzo kikuu bila hata kujua...☠️
*Ipo hivi.....*
PID (Pelvic Inflammatory Disease) Ni ugonjwa unaomchoma mwanamke —Si mwanaume.📌
Kwa sababu PID ni maambukizi yanayopanda juu kupitia njia ya uzazi ya mwanamke na kuathiri kizazi, mirija ya fallopian, na ovari...
*Hapa ndipo siri ilipo…* 👇
Mwanaume hauguwi PID, ila anaweza kuwa mhifadhi na msambazaji wa vimelea (bacteria k**a Chlamydia trachomatis na Neisseria gonorrhoeae)...
Bila dalili, bila maumivu, unajiona mzima lakini unabeba kifurushi kisichoonekana ambacho kwa kila tendo la ndoa, kinasafiri hadi kwa mke wako..🤒
*Na matokeo yake..?*
↳ Mirija inaziba kabisa, Yai haliwezi tena kusafiri...
↳ Hormone imbalance, Mfumo mzima wa mwili wa mwanamke unavurugika...
↳ Maisha Bila mtoto, Familia inageuka uwanja wa lawama, na maumivu ya kimya...
*Sasa, jiulize swali hili....*
Kwa nini wanawake wengi wakitibu PID hawaponi kabisa..?☠️
*Jibu ni gumu, lakini ukweli ni huu…* 👇
Sio PID pekee inayokuumiza, Ni usugu wa vimelea unaosababishwa na matumizi mabaya ya dawa..
↳ Dawa za kuweka ukeni bila ushauri..
↳ Sindano za mara kwa mara, Wengine wamechomwa hadi 7 days bila mafanikio...
↳ Kutumia dawa bila kufuata mpango kamili wa tiba sahihi...
*Matokeo yake?*
Vimelea vinakuwa sugu, vinakataa dawa, na ugonjwa unarudi mara kwa mara huku ndoto za uzazi zikizidi kufifia...☠️
*Siri ya ukombozi ipo hapa...* 👇
↳ Kupima kwa usahihi, Bila vipimo sahihi, tiba itakuwa ni kubahatisha.
↳ Kufuata ushauri wa daktari, Sio kujitibu ovyo ovyo kwa kununua dawa maduka ya dawa au mitandaoni...
↳ Wanaume kushiriki matibabu, Kwa sababu chanzo mara nyingi kiko upande wao..
*NB:* K**a wanaume tunalo jukumu la kulinda wake zetu.
K**a familia tunalo jukumu la kulinda vizazi vyetu.
Na k**a jamii, tunalo jukumu la kuvunja ukimya, ili PID isiendelee kuua ndoto za uzazi....
Hii sio tu elimu, ni wito wa mapinduzi ya afya ya uzazi, Tuchukue hatua, Leo...🫡 K**a upo na mimi nipe Reaction 👍 Kisha ni follow Seen Afya Kwanza kujifunza zaidi