Taasisi ya Tiba ya Mifupa - MOI

Taasisi ya Tiba ya Mifupa - MOI Tunatoa matibabu ya Kibingwa na bobezi ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo,Mgongo, Mishipa ya fahamu, huduma za dharura na ajali

The Muhimbili Orthopaedic Institute (MOI) is an autonomous Institution established through an Act of Parliament No 7 of 1996 with the main objective of providing primary,secondary and Tertiary care for preventive and curative health services in the field of Orthopaedic,Traumatology and neurosurgery
The management of the Institute is based on Public/Private Mix concept geared towards performance improvement and and self sustainability.

Je unafahamuHakuna sababu ya kuwahi asubuhi mapema kwa ajili ya kupata namba ya kumuona daktari bingwa na mbobezi MOISca...
09/12/2025

Je unafahamu

Hakuna sababu ya kuwahi asubuhi mapema kwa ajili ya kupata namba ya kumuona daktari bingwa na mbobezi MOI

Scan QR Code au bonyeza link https://onlineappointment.moi.ac.tz/appointment/ kuweka Miadi

Ukipata changamoto wasiliana nasi +255 718 582 000

ya kidigitali

09/12/2025
SPIKA ZUNGU  AFURAHISHWA NA KAMBI MAALUM YA UGAWAJI WA MIGUU BANDIA BURENa Amani Nsello- SWAMISpika wa Bunge la Jamhuri ...
08/12/2025

SPIKA ZUNGU AFURAHISHWA NA KAMBI MAALUM YA UGAWAJI WA MIGUU BANDIA BURE

Na Amani Nsello- SWAMI

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. M***a Azzan Zungu ametembelea kambi ya utoaji viungo bandia na kufurahishwa na hatua hiyo ambayo ni miongoni mwa njia bora za kugusa maisha ya Watanzania wanaoishi na ulemavu wa viungo.

Akizungumza leo Jumatatu Disemba 08, 2025 eneo la Swami Vivekanand Cultural Centre (SVCC), Masaki Jijini Dar es Salaam wakati alipotembelea kambi hiyo, Mhe. Zungu amesema hatua ya wataalamu wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) kujengewa uwezo wa kutengeneza miguu bandia ni muhimu kwa ustawi wa huduma jumuishi nchini Tanzania.

“Tunataka zoezi hili liwe endelevu, pindi wataalamu wetu wa ndani watakapokuwa wamejengewa uwezo kamili, miguu bandia iwe inapatikana kwa bei nafuu... Chini ya laki tano, badala ya zaidi ya milioni mbili na nusu k**a ilivyo sasa” amesema Mhe. Zungu

Wakati huo huo, Mhe. Zungu ameushukuru pia Ubalozi wa India nchini Tanzania kwa kuchangia uanzishwaji na utekelezaji wa kambi hiyo, akisisitiza kuwa ushirikiano huo umeleta faraja kwa Watanzania wengi.

Kwa upande wake, Lakshay Anandi, Afisa Mawasiliano na Siasa wa Ubalozi wa India nchini Tanzania, amesema serikali ya India itaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kuboresha sekta ya afya na kubadilishana utaalamu.

Naye, Mtaalamu wa Vifaa Tiba na Viungo Saidizi (Bandia) kutoka MOI, Bw. Charles Mahua, amesema mpaka sasa jumla ya wahitaji 178 tayari wameshapatiwa viungo bandia kupitia kambi hiyo huku waliosajiliwa ni zaidi ya 1000.

WATU WENYE UHITAJI 140 WAPATIWA VIUNGO BANDIA BURE KATIKA KAMBI MAALUM Na Abdallah Nassoro- MOITaasisi ya tiba ya mifupa...
05/12/2025

WATU WENYE UHITAJI 140 WAPATIWA VIUNGO BANDIA BURE KATIKA KAMBI MAALUM

Na Abdallah Nassoro- MOI

Taasisi ya tiba ya mifupa kwa kushirikiana na Ubalozi wa India pamoja na Taasisi ya BMVSS imerejesha tabasamu kwa wahitaji 140 waliopoteza miguu na mikono kwa kuwapatia viungo bandia bure katika kambi maalum inayoendelea jijini Dar es Salaam.

Mratibu wa kambi hiyo kutoka MOI ,Bi. Mary Chandeu ameyasema hayo leo Ijumaa, Desemba 5, 2025 kuwa idadi hiyo ya wahitaji waliofaidika na msaada huo ni kati ya 255 waliofanyiwa uchunguzi wa awali na kubainika kukidhi vigezo vya kitatibu vya kuweza kutumia viungo hivyo bandia.

“Kambi yetu ilianza Novemba 26, 2025 na hadi Jana Desemba, 04 tumesajili wahitaji 872, zoezi la usajili linaendelea… Kati ya hao, 255 wameshafanyiwa uchunguzi wa awali ili kubaini iwapo wanasifa ya kutumia kiuongo bandia au laa, na 140 wamekabidhiwa viungo hivyo, wengine wanaendelea kusubiri” amesema Bi, Chandeu na kuongeza kuwa

“Lengo la kambi hii ni kutoa viungo bandia kwa watu wenye uhitaji 600 bure, hivyo wenye uhitaji wasisite kujitokeza ili waweze kutumia fursa hii adhimu kwao… Wale ambao watakosa kwa sababu mbalimbali zikiwemo za kitabibu au kutimia kwa idadi ya walengwa, tutatengeneza mkakati mwingine wa kuhakikisha wote wenye uhitaji wanafikiwa”

Amefafanua kuwa wahitaji wanne tu ndiyo waliobainika kukosa sifa za kupata msaada huo kwa sasa kukutokana na majeraha kutopona vizuri na mazingira yasiyo rafiki kwa matumizi ya vifaa hivyo yaliyosababishwa na mfumo wa matibabu waliyopata wakati wa kupoteza kiungo husika.

“Hawa wanne wapo waliobainika kuwa wanahitaji kusubiri wapone na wengine wanatakiwa kuendelea na matibabu ya kutengeneza umbo la kiungo katika mfumo utakaoweza kuruhusu matumizi ya kiungo bandia"

05/12/2025
WAUGUZI MOI WAHIMIZWA KUTOA HUDUMA BORA KWA WATEJANa Amani Nsello- MOITaasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI...
04/12/2025

WAUGUZI MOI WAHIMIZWA KUTOA HUDUMA BORA KWA WATEJA

Na Amani Nsello- MOI

Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) imeendelea kuwekeza katika kuboresha huduma zake kwa kutoa mafunzo mahsusi kwa wauguzi wake yakilenga kuboresha namna wanavyowahudumia wagonjwa na wateja kwa ujumla.

Katika mafunzo hayo wauguzi hao wamefundishwa umuhimu wa kutoa huduma kwa ukarimu, kuwapokea wagonjwa kwa huruma na 'kuvaa viatu vya mteja' ili kuelewa hisia, mahitaji na changamoto wanazopitia wagonjwa.

Akizungumza leo Alhamis Desemba 04, 2025 Bw. Jumaa Almasi Meneja Ustawi wa Jamii na Tiba Lishe wa MOI amesisitiza umuhimu wa kubadili fikra na mtazamo wa utoaji wa huduma.

"Ni muhimu kila mgonjwa anayekuja hapa (MOI) ahisi kuthaminiwa, hivyo mafunzo haya yanatupa nafasi ya kujipanga upya, kuboresha mawasiliano yetu na wagonjwa na kuhakikisha tunatoa huduma zenye utu na zinazozingatia viwango bora vya kitaaluma" amesema Bw. Almasi

Pia, Bw. Almasi amewaambia wauguzi hao kuzingatia mila na desturi za kila mgonjwa anayefika katika taasisi hiyo na kuzielewa hisia za wateja.

Kwa upande wake, Meneja Wagonjwa wa Ndani wa MOI Bi. Magreth Kumpuni, amewaasa wauguzi hao kuzingatia mafunzo waliyopatiwa na kuyatafsiri moja kwa moja katika utendaji kazi wa kila siku.

Mafunzo hayo yanatarajiwa kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma, kuhakikisha kila mgonjwa anapata huduma yenye ustaarabu na kuifanya MOI kuendelea kuwa taasisi inayoaminiwa na wananchi kwa kutoa huduma bora.

Siku ya UKIMWI Duniani
01/12/2025

Siku ya UKIMWI Duniani

MOI yaendeleza ubabe SHIMMUTA, Morogoro
28/11/2025

MOI yaendeleza ubabe SHIMMUTA, Morogoro

BODI YA WADHAMINI MOI YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADINa Abdallah Nassoro- MOIBodi ya Wadhamini wa Taasisi ya Tiba y...
27/11/2025

BODI YA WADHAMINI MOI YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI

Na Abdallah Nassoro- MOI

Bodi ya Wadhamini wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) imeeleza kuridhishwa na hali ya utekelezaji wa miradi ya taasisi hiyo inayolenga kupanua maeneo ya utoaji huduma na kupunguza msongamano wa wagonjwa wa nje (OPD), katika eneo la sasa la kutolea huduma.

Makamu Mwenyekiti wa bodi hiyo CPA Augustino Mbogela amebainisha hayo leo Novemba 27, 2025 baada ya kufanya ziara ya ukaguzi wa mradi wa jengo lililokuwa hospitali ya Tumaini (X-Tumaini) na ujenzi wa kituo cha utengamao kilichopo Bweni jijini Dar es Salaam.

“Miradi hii licha ya kuwa itasogeza huduma karibu na jamii lakini pia itapunguza msongamano wa wagonjwa wa nje katika eneo la sasa la kutolea huduma…niseme tumeridhishwa na kasi ya ujenzi na nitoe rai kwa wakandarasi kuzingatia muda ili wagonjwa waweze kufaidika na huduma hizi” amesema Mbogela na kuongeza kuwa

“Unapopanua huduma unaruhusu kuwafikia watu wengi zaidi, lakini hii inakwenda sambamba na uboreshaji wa huduma hizo, naipongeza Menejimenti kwa utekelezaji wa miradi hii, ni imani yangu kuwa mara itakapoanza kufanya kazi basi kila mmoja wetu atashuhudia matunda ya uwekezaji huu”

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Mhe. Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya amesema mradi wa ukarabati wa X-Tumaini utekelezaji wake umefikia asilimia 96 na kwamba mwanzoni wa Januari 2025 utoaji wa huduma unatarajia kuanza.

“Hapa tutatoa huduma za wagonjwa maalum na wakimataifa, kwa sasa huduma hizi zinatolewa katika eneo dogo pale MOI na kusababisha msongamano wa wagonjwa, lakini kukamilika kwa jengo hili kunafungua njia ya huduma za wagonjwa maalum na za kimataifa kufurahia huduma katika jengo hili” amesema Dkt. Mpoki

Ameongeza kuwa “Hapa zitaendeshwa kliniki na pale mgonjwa atakapolazimika kulazwa basi atapelekwa kwenye wodi zetu…pia mradi wa kituo cha utengamao Bweni k**a ulivyo huu, ni mradi wa kimkakati wa kujaribu kusogeza huduma karibu na watu wa eneo hilo ambapo huduma za kibingwa na bobezi zitatolewa pamoja na huduma za utengamao”.

MOI YAIGALAGAZA TPDC MPIRA WA MIGUU SHIMMUTANa Mwandishi wetu - MOROGOROTimu ya mpira wa miguu ya Taasisi ya Tiba ya Mif...
27/11/2025

MOI YAIGALAGAZA TPDC MPIRA WA MIGUU SHIMMUTA

Na Mwandishi wetu - MOROGORO

Timu ya mpira wa miguu ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) imefanikiwa kuibuka na ushindi wa 2 - 0 dhidi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) katika mashindano ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma, Taasisi na Makampuni Binafsi Tanzania (SHIMMUTA) yanayoendelea kurindima mkoani Morogoro.

Mchezo huo umechezwa leo Novemba 27, 2025 katika uwanja wa Jordan, Nahodha wa timu ya MOI Amiri Ramadhani amesema ushindi huo umepelekea kuongoza katika kundi D kwenye mashindano hayo.

“Tumeibuka na ushindi katika mchezo wa leo kwa kupata alama tatu muhimu, niwapongeze wachezaji wenzangu kwa kuwa na nidhamu na kufuata vizuri maelekezo ya kocha wetu Max” amesema Ramadhani

Ameongeza kwa kusema kuwa katika mchezo huo goli la kwanza limefungwa na yeye mwenyewe na la pili limefungwa na Binuru.

Mashindano hayo yalianza Novemba 25, 2025 na yatafikia tamati Desemba 6, 2025.

MOI YAPATA USHINDI MNONO MPIRA WA PETE, YAICHAKAZA NIT Na Mwandishi wetu - MOITimu ya mpira wa pete ya Taasisi ya Tiba y...
27/11/2025

MOI YAPATA USHINDI MNONO MPIRA WA PETE, YAICHAKAZA NIT

Na Mwandishi wetu - MOI

Timu ya mpira wa pete ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) imepata ushindi mnono wa 39 - 14 dhidi ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) katika Mashindano ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma, Taasisi na Makampuni Binafsi Tanzania (SHIMMUTA) yanayoendelea kurindima mkoani Morogoro.

Akizungumza baada ya mchezo huo uliochezwa leo Novemba 27, 2025 katika uwanja wa Magadu, Kocha wa timu hiyo Paulo Mathias amewapongeza wachezaji wake kwa ushindi mnono na kuwataka waongeze morali zaidi kwenye michezo inayofuata.

“Niwapongeze kwa ushindi wa leo kwa kuwafunga NIT na tumefanikiwa kupata alama tatu, niwaombe muongeze ari na kujituma zaidi kwenye michezo mingine ili tufikie malengo yetu” amesema Mathias

Kwa upande wake Mchezaji wa timu hiyo Farida Mlema amesema wataongeza juhudi, ubunifu na morali katika michezo mingine inayofuata ili kuhakikisha wanapata matokeo mazuri.

Mashindano hayo yalianza Novemba 25, 2025 na yatafikia tamati Desemba 6, 2025.

WAZIRI WA AFYA ATOA WITO KWA WALIOPOTEZA MIGUU, MIKONO KUCHANGAMKIA FURSA YA VIUNGO BANDIA 600 VINAVYOTOLEWA BURE   N Ab...
26/11/2025

WAZIRI WA AFYA ATOA WITO KWA WALIOPOTEZA MIGUU, MIKONO KUCHANGAMKIA FURSA YA VIUNGO BANDIA 600 VINAVYOTOLEWA BURE

N Abdallah Nassoro-MOI

Waziri wa Afya Mhe: Mohamed Mchenjelwa ametoa wito kwa wananchi waliopoteza miguu na mikono kujitokeza kwa wingi kupata viungo bandia vinavyotolewa bure na kampuni ya Emcure Pharmaceuticals ya nchini India ikishirikiana na Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) kwa uratibu wa Ubalozi wa India nchini.

Wito huo ameutoa leo Novemba 26, 2025 katika hotuba yake iliyosomwa na Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Mhe: Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya wakati wa uzinduzi wa kambi maalum ya utengenezaji na ugawaji wa miguu na mikono bandia kwa wahitaji 600.

Amesema upatikanaji wa miguu hiyo bila malipo kunatoa fursa kwa wahitaji wenye kipato cha chini kufurahia maisha yako kwa kuweza kufanya kazi k**a ilivyokuwa awali kabla ya upoteza kiungo husika.

“Tuhakikishe viungo vyote 600 vinapata wahitaji, wengi wamekuwa wakimudu kununua kiti mwendo kwa ajili ya kurahisisha kutembea kutokana na miguu bandia kuwa na bei kubwa ambayo hawawezi kuimudu, lakini leo hii huduma hiyo inatolewa bure hapa, kwanini basi mtu akose huduma hii” amesema Mhe: Mchenjelwa na kuongeza kuwa

“Sisi Wizara ya Afya tunaushukuru ubalozi wa India nchini kwa kuratibu jambo hili, lakini pia tunaishukuru kampuni ya Emcure Pharmaceuticals iliyotoa msaada huu, nimeambiwa viungo hivi vinatumia teknolojia ya kisasa na imara ya Jaipur, pia taasisi yetu ya MOI itumie fursa hii kujifunza teknolojia mpya ili msaada unapoisha tuweze kuendelea kuwasaidia watu wetu”

Kwa upande wake Balozi wa India Nchini Mhe: Biswadip Dey amesema msaada huo ni muendelezo wa ushirikiano mzuri ulipo baina ya Tanzania na India, ikiwa ni kambi ya pili kufanyika kwa lengo la kurejesha utu, furaha na upendo kwa waliopoteza viungo.

“Mwaka 2019 tulifanya kambi ya kwanza na mwaka huu tumerudi tena ikiwa ni sehemu ya kuimarisha uhusiano wetu, bila kujali gharama za vifaa hivyo sisi tunavitoa bure kwa wahitaji, naishukuru sana serikali ya Tanzania na Taasisi ya MOI kwa kuwezesha jambo hili, kwetu ni faraja kuwa sehemu ya kurejesha furaha kwa wengine” amsema Mhe: Dey

Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa MOI

Address

P. O. BOX 65474
Dar Es Salam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Taasisi ya Tiba ya Mifupa - MOI posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to Taasisi ya Tiba ya Mifupa - MOI:

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram

Category

Our Story

The Muhimbili Orthopaedic Institute (MOI) is an autonomous Institution established through an Act of Parliament No 7 of 1996 with the main objective of providing primary,secondary and Tertiary care for preventive and curative health services in the field of Orthopaedic,Traumatology and neurosurgery The management of the Institute is based on Public/Private Mix concept geared towards performance improvement and and self sustainability.