Hopefully.life

Hopefully.life Welcome to our mental health consultation centre to help you achieve your best self.

USIRUHUSU WATU KUTUMIA HISTORIA YAKO KUKUNYANYASA!Kuna mambo mengi ambayo uliyafanya kipindi cha nyuma, kuna hatua nying...
10/02/2024

USIRUHUSU WATU KUTUMIA HISTORIA YAKO KUKUNYANYASA!

Kuna mambo mengi ambayo uliyafanya kipindi cha nyuma, kuna hatua nyingi ulipitia, zipo nzuri zipo mbaya, kuna mambo mengi ambayo unatamani kuyasahau katika maisha yako lakini huwezi, kuna mambo mengi unatamani kuyabadilisha katika maisha yako lakini huwezi. Yameshatokea na ni sehemu ya maisha yako, haya tunayaita historia, si sehemu tena ya maisha yako, wewe ni mtu mpya, huwezi kubadilisha historia lakini usijihukumu au kuruhusu watu kukuhukumu kutokana na historia yako.

Ulikua Malaya kweli, ulikua mwizi kweli, umetoka katika familia ya kimasikini, ulikua mshamba, ulikua unadanga, ulikua marioo na chochote kile ambacho ulikua, k**a umeshapita katika hali yoyote mbaya na sasa hauko huko cha kufanya ni kuangalia historia na kumshukuru Mungu hauko kule tena. Acha kujihukumu, acha kujisikia vibaya na kubwa kabisa usiruhusu watu kukufanya ujisikie vibaya.

Anaweza kuwa mume au mke, wanaweza kuwa majirani au ndugu, watataka kukudharau kwakua ulikua flani, watataka kukudhalilisha kwakua unatokea katika hali flani, watataka kukukatisha tamaa kwakua huna elimu flani. Huna haja ya kuwasikiliza, huna sababu ya kuwapa akili yako, wala huna sababu ya kujielezea kwako. Wewe ni mtu mpya hivyo acha kulia, acha kuhuzunika, acha kujiona mbaya, acha kujiona umepungukiwa kwakua tu historia yako si tamu.

Share na Mungu akubariki!!

16/05/2023

..... HUZUNI KATIKA MAHUSIANO....

Huzuni Katika maisha ya mahusiano ni hali ya afya ya akili ambayo huathiri maisha ya mahusiano kwa kiasi kikubwa...

Mtu aliye na huzuni katika maisha ya mahusiano yake anaweza kupata dalili kadhaa za kiakili na za kimwili....

Miongoni mwa dalili hizo zinaweza kuwa....

Kujisikia kutokuwa na thamani,hasira kupita kiasi, kutokujijali, kupoteza hamu ya tendo la ngono, Kushindwa kudumisha uume wakati wa tendo la ngono, kupunga kwa ufanisi kazini, kupoteza hamu ya kula, Kula kupita kiasi, kukoswa usingizi, Kujitenga, mawazo ya kujiua, Nakadhalika...

Dalili hizi zinaweza kuonekana kawaida lakini kadri siku zinavyoenda dalili hizi hodhoofisha afya ya akili na mwili pia kwa mhusika, ikiwa hazitashughulikiwa...

Baadhi ya mambo yanayoweza kuchangia huzuni katika maisha ya mahusiano Ni:-

Mawasiliano mabaya, Kukosekana kwa uaminifu, kusalitiwa, kunyanyaswa, Kutelekezwa, mahusiano ya umbali mrefu, kupuuzwa, Kutengwa au kubaguliwa, Kumbukumbu za matukio mabaya ya nyuma yaliyotokea. Nakadhalika..

Unapopitia huzuni katika maisha yako ya mahusiano, unaweza kuhisi mahusiano yako ni mzigo mzito unaokuelemea.

Wakati mwingine Kukosekana kwa msaada wa huzuni unayoipitia.Kunaweza kuwa na matokeo K**a vile, mawazo ya kujiua, kujiona hufai, kujihisi huna thamani hustahili kupendwa au kupenda. Nakadhalika...
......Habari njema ni kuwa....

Sio kila mtu anaweza kuelewa huzuni unayopitia katika mahusiano yako, usiteseke kimya kimya na huzuni yako. Kuna watu wanasikiliza, wanajali na wanasaidia katika kila hatua ya kupona maumivu yako, watu Hawa ni Wanasaikolojia na washauri nasihi. ..

.....Tafuta msaada Kisaikolojia ( Tiba ya Mazungumzo) kutoka kwa wataalamu wa afya ya akili kwa tatizo lako unalolipitia ..

TUZIDI KUJIFUNZA, TUSICHOKE KUJIFUNZA ✍️

Kwa Huduma ya msaada wa Kisaikolojia ( Tiba ya Mazungumzo)..

Wasiliana nami kupitia namba 0620375138

Psychologist & Counselor

01/04/2023
29/03/2023

Muendelezo.....
ya kuacha kunywa pombe katika mwili wako ni mdogo sana. Pia, hatua hii hupunguza hatari kwako ya kupata ugonjwa wa moyo na mishipa ya damu. Hii ni kwa sababu, pombe katika mwili wako huongeza shinikizo la damu na kufanya moyo wako kufanya kazi kwa bidii tofauti na inavyotakiwa.

4️⃣... Baada ya Mwezi Mmoja:

〰️ Mwezi mmoja bila kunywa pombe ni mafanikio makubwa sana. Ukifikia hatua hii utaanza kujihisi vizuri zaidi na kujiona tayari umeacha kunywa pombe.

Lakini, usiposimamia sababu za maamuzi yako ya kuacha pombe unaweza ukawa katika hatari ya kuirudia hali yako kutokana na mazingira unayoishi au aina ya marafiki ulionao.

5️⃣... Baada ya Miezi Sita:

〰️ Unapofikisha miezi 6 bila kunywa pombe, utaanza kupata manufaa. Hatari yako ya kupata saratani itapungua, na utendakazi wa ini katika mwili wako utakuwa umeuboresha sana kwa sababu utakuwa umepunguza kiwango kikubwa cha sumu katika mwili wako. Pia, ngozi yako itaanza kuonekana yenye afya zaidi.

6️⃣ ... Baada ya Mwaka Mmoja:

〰️. Unapofanikiwa kufikisha mwaka mmoja bila kunywa pombe mwili wako unakupa Hongera kwa kutimiza miezi 12 bila kunywa pombe.

Katika hatua hii, hatari ya kupata aina zote za ugonjwa itapunguzwa na msongamano wa mifupa yako utaanza kuongezeka kwa uimara zaidi...

✍️... HITIMISHO

🩺... Kumbuka kuwa Tunatofautiana, yawezekana kwa mwingine akapitia hatua 1 tuu kufanya maamuzi na akaacha kunywa pombe, kwako ikawa hatua kwa hatua mpaka kufikia kuacha.Kuna mwingine anaweza kufikia mpaka hatua ya miezi sita lakini akateleza kwa kutokuzingatia malengo ya maamuzi yake akajikuta ameirudia Hali yake ya utegemezi wa pombe au kunywa pombe kupita kiasi....

Wakati wa kuacha pombe inaweza kuwa changamoto Sana kwako, Lakini ni muhimu kukumbuka kwamba kuna faida muhimu sana utakazozipata baada ya kuacha kunywa pombe.

TUZIDI KUJIFUNZA NA TUSICHOKE KUJIFUNZA ✍️

Huduma ya msaada wa Kisaikolojia ( Tiba ya Mazungumzo inapatikana)

Wasiliana nami kupitia namba:-
0620375138( Piga simu)

P

29/03/2023

Nini Hutokea Unapofanya maamuzi ya kuacha Pombe?

🩺... Ikiwa umekuwa tegemezi katika unywaji wa pombe kupita kiasi.Umekuwa ukipambana na matumizi mabaya ya unywaji wa pombe kupita kiasi.

Hujachelewa bado, unaweza kufanya maamuzi ya kuacha kunywa pombe na maamuzi hayo yakaleta mafanikio ya afya ya mwili wako, akili yako na Mafanikio yako kwa ujumla..

Nini Kinatokea unapofanya maamuzi ya kuacha kunywa pombe?

Ikiwa maisha yako yamekuwa tegemezi kwa matumizi ya pombe, unakunywa pombe kila siku, unakunywa pombe kupita kiasi kila unapopatwa nafasi ya kufanyaa hivyo..

Ratiba hii inaweza kuwa na msaada mkubwa kwako ikiwa utafanya maamuzi ya kuacha kunywa pombe kwa kujizuia kutokunywa au kusogelea mazingira yanayokushawishi kunywa pombe..

1️⃣ ... Jizuie Siku ya kwanza;

〰️ Unapoamua kufanya maamuzi ya kuacha kunywa pombe siku ya kwanza huwa ngumu zaidi, maamuzi ya hatua hii ni muhimu sana ikiwa utayavumilia mwili wako utaanza kutoa sumu za kujiondoa katika tatizo lako.

Kwa watu walio na utegemezi mkubwa wa pombe, dalili za kujiondoa kwa haraka katika utegemezi wa pombe zinaweza kuwa mbaya zaidi hivyo zinahitaji mwongozo wa matibabu ya msaada wa Kisaikolojia au matibabu ya dawa kutoka kwa Mtaalamu wa Magonjwa ya akili kitengo cha dawa ( Psychatrist)

2️⃣... Baada ya Siku Tatu:

〰️ Baada ya siku tatu, kuna uwezekano mkubwa wa kujihisi mwenyewe vizuri. Hata hivyo, watu ambao wamekuwa wakinywa pombe kupindukia kwa muda mrefu katika hatua hii wanaweza kupata dalili za ugumu wa kujiondoa katika unywaji wa pombe kupindukia, dalili hizi zinaweza kuwa ni ishara ya kutisha katika mabadiliko ya afya ya mwili Pamoja na mabadiliko ya kimaisha kwa ujumla.

Ikiwa katika hatua hii utakuwa na wasiwasi kuhusu dalili zako, ni muhimu kutafuta Msaada wa matibabu katika kituo Cha afya kwa kuonana Mtaalamu wa Magonjwa ya akili kitengo cha dawa ( Psychatrist)

3️⃣...Baada ya wiki Moja:

〰️ Baada ya wiki moja kupita bila kunywa pombe, uwezekano wa kukumbwa na mabadiliko ya maamuzi yako

28/03/2023

Acha uzembe, watu hawajaisha, kule mliko kutania bado wapo, tena wengi tu wenye upendo wa kweli, wanaojua thamani, bado wapo, akiondoka aende atakuja mwingine,
Tena huyo ndiye anazuia baraka zako.

3. Fear of perjury pain of love.
Wengi wanaogopa sana kuachika Kwaiyo wanalazimisha kuendelea kukaa na hao wakorofi kwasababu ya kuogopa aibu, wala sio kwamba anapenda.

Ukimuuliza atakwambia kachoka lakini anaogopa, sasa kubali aibu kwa usalama wa maisha yako, move on..

Nina wasalimu

© 2023 TANZANIA

28/03/2023

MLIPO KUTANIA NA HUYO HAWAJAISHA, UTAWAPENDA WENGI, HUYO MWACHE AENDE.

MOVE ON…….

Yes, move on.., ukiendelea kukomaa hapo utakuja kujifia bure.

Kuna wakati Mungu anaruhusu maumivu yakupate iwe k**a darasa kwako, pengine alisema nawe awali ukagoma, sasa ameruhusu ujifunze, umesha maliza darasa just move on...

“Bali wewe, uwe na kiasi katika mambo yote, ……..” 2 Timotheo 4:5

Una nyanyasika bado unavumilia, amefika hatua, anakutukana tena matusi ya nguoni, bado, tu amefika hatua anakupiga bado unavumilia afu cha kushangaza ni mchumba tu akiwa mume utaozea ndani…

Unaona kabisa anatafuta sababu ya wewe muachane, anakuonyesha dharau waziwazi, una uthibitisho kuwa anatoka na mtu mwingine, bado una sumbuka kutafuta ushauli tu?

Tafiti zina onyesha wadada wengi huwa wanakuwa wagumu kuchukua hatua ya kuondokana na penzi ambalo ni mwiba, kwasababu mbalimbali moja ya sababu ni hizi

1.blind of love
Huu ni upofu wa mapenzi, ambao unatengenezwa na matendo kabla ya mpasuko

Akikumbuka jinsi alivyo thaminiwa mwanzo, moyo unajipa tumaini kuwa haja achwa kumbe kaachika muda sana, akikumbuka zawadi alizopewa ndio kabisa, anakosa nguvu ya kutoka,

Matendo aliyo kufanyia mwanzo sio kigezo cha kubaki na kuhatarisha afya yako, usalama wa maisha yako ni muhimu, wala usilazimishe kutumia upendo wa zamani kuziba ukweli mbaya wa sasa ambao ni hatari sana

Wengi tuna kuwa na huu upofu, hatutaki kuamini kingine kuhusu huyo mtu kwasababu tulisha aminishwa kwa zawadi za mwanzo

Ukweli ni kwamba, box la zawadi huwa halina thamani, zawadi inapo pokelewa na kuondolewa ndani yake

Namaanisha hivi, k**a hana upendo tena nawe, hata hizo zawadi, out alizo kutoa, ahadi na mambo aliyokufanyia mazuri mwanzo, hayana thamani, ishi kwa upendo wa sasa acha kuwa kipofu binadamu wanabadilika wewe.

2.life after separation
Wengi huwa wanashindwa ku move on sababu ya kujiuliza itakuwaje baada ya kuachana naye, na wanajisemea kuwa kumpata mwingine ni ngumu,

Inaendelea

thougnts are controller of your action, mind itAfdek-centreAfdek-centreAfdek-centre
24/03/2023

thougnts are controller of your action, mind it
Afdek-centreAfdek-centreAfdek-centre

23/03/2023

Ukweli ni Kwamba HAKUPENDI, Ila Ukimuuliza "Unanipenda?" Hakujibu Ndio au Hapana Ila anakujibu Hivi👇

"Kwanini Unauliza Hivyo"

Huyo anajua anachokifanya, anajua fika kuwa matwndo yakw kwako unayaona na yanakugusa, anakuuliza hivyo. Ili apate uhakika kuwa ujumbe wake umeupata kupitia matendo yake au vp.
AAfdek-centreAfdek-centreAfdek-centre

🦅Kisaikolojia hamna mtu anaye kufa kiume.Yaani ukitunza jambo ukafa nalo kwenye saikolojia hatusemi umekufa kiume.Bali t...
22/03/2023

🦅Kisaikolojia hamna mtu anaye kufa kiume.

Yaani ukitunza jambo ukafa nalo kwenye saikolojia hatusemi umekufa kiume.

Bali tunasema matatizo yako uliyotunza ndio yamekuzidia na kukuua.

Hayo ndio yanaaminika yamekufanya ufe sababu yalizidi katika moyo yakakupelekea ukawa na mawazo mengi na kwakuwa ulikosa sehemu ya kutua mzigo huo yakakuwaisha ahera.

Na wengine huchukua maamuzi ya moja kwa moja kujinyonga, na wengine hufa taratibu kutokana na stress ya changamoto yake aliyonayo.

Asilimia kubwa ni bora mtu mzungumzaji anatoa na kupunguza mzigo katika moyo wake na kushirikisha wenzio, na wengine wakawa sehemu ya tatizo lake na akajiona tuko wengi, huyu amani inapatikana na anaona maisha yanaendelea.

Hakikisha unapata sehemu ya kushirikisha changamoto yako, usikubali changamoto ikukatishe tamaa ya kuishi
#+255620375138

Address

Dodoma

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 17:00

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Hopefully.life posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to Hopefully.life:

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram