AFYA YAKO kwanza.

AFYA YAKO kwanza. Health education

07/08/2021

FAHAMU UGONJWA WA P.I.D

(PELVIC INFLAMMATORY DIDEASE)

Huu ni ugonjwa unaoshambulia sana njia ya uzazi, mlango wa mfuko wa uzazi(cervicitis), mfuko wa uzazi(endometritis), mirija za uzazi(salpingitis), mahali mayai yanako zalishwa(oophoritis).
Maambukizi haya hasa husababishwa na Bacteria (Gonorrheal and clamydial organism), na wakati mwingine huweza kusababishwa na fangasi, virusi na wadudu wengine.

Ugonjwa huu unapokua umefika mbali zaidi husababisha matatizo ya uzazi k**a vile kutokupata ujauzito, vidonda katika mirija ya uzazi, maumivu makali kiunoni yenye kujirudia, mimba kutunga nje ya kizazi. Pia k**a umefika mbali zaidi husababishwa mtu kuondolewa sehemu ya njia ya uzazi au kizazi chote (Hesterectomy)

DALILI ZAKE.
Uonapo dalili yoyote au zote kati ya hizi usipuuzie.
1)Maumivu maeneo ya kiunoni
2)Maumivu wakati wa tendo la ndoa
3)Kutokwa na uchafu/majimaji sehemu za siri ambayo huwa mweupe k**a maziwa mgando(usio na harufu) au wanjano,kijani au rangi ya brown wenye harufu.
4)Homa
5)Kukosa hamu ya kula
6)Kichefuchefu au kutapika.
7)wakati mwingine mimba kuharibika
8)Muwasho sehem za siri
9)Wakati mwingine maumivu wakati wa haja ndogo.

MATIBABU
Kwa maelezo zaidi na matibabu usisite kunitafuta piga/sms/whatsapp kwa namba...
0742251673

Weka appointment na daktari kwa sh elf kumi tu (10000). Piga kwa namba iliotajwa kupata utaratibu wa malipo kabla ya huduma.

LIKE kisha SHARE na rafiki zako wapate elimu hii

Sasa ni rahisi kwa tatizo lolote unaweza wasiliana na Daktari wako muda wowote kupitia namba 0742251673, sms au WhatsApp
09/04/2021

Sasa ni rahisi kwa tatizo lolote unaweza wasiliana na Daktari wako muda wowote kupitia namba 0742251673, sms au WhatsApp

KWA GHARAMA NAFUU PATA TUBA SAHIHI
30/03/2021

KWA GHARAMA NAFUU PATA TUBA SAHIHI

FIBROIDS (UVIMBE KATIKA KIZA)Huu ni uvimbe ambao mara kwa mara huonekana katika mfumo wa uzazi wa mwanamke. Uvimbe huu k...
28/05/2020

FIBROIDS (UVIMBE KATIKA KIZA)

Huu ni uvimbe ambao mara kwa mara huonekana katika mfumo wa uzazi wa mwanamke. Uvimbe huu kitaalamu unaweza kuwa Uterine myomas, leomyomas, au fibromas. Asilimia 20 hadi 50 ya wanawake walio katika umri wanoweza kubeba mimba hupata uvimbe huu katika mfumo wa uzazi hivyo kupelekea matatizo katika mfumo wao wa uzazi.

SABABU YA KUTOKEA KWA UVIMBE KATIKA MFUMO WA UZAZI.

Hakuna sababu maalum inayoelezwa katika kutokea kwa uvimbe huu isipokua uvimbe huu huchipua na kukua kwa haraka kutoka kwenye misuli laini ya mfumo wa uzazi. Ukuaji wake wa haraka ni kwasababu ya uwepo wa homoni ya estrogen kwa wingi katika mfumo wa uzazi wa mwanamke.

DALILI ZA UVIMBE KWENYE MFUMO WA UZAZI. (FIBROIDS)

Uonapo dalili moja wapo kati ya hizi usipuuzie

1. Kutokwa na damu nyingi wakati wa siku zako.
2. Kuwa katika siku zako kwa muda mrefu isiyo kawaida (zikizidi siku 3-5, wengine hadi 7 )
3. Kutokwa kwa damu isiyo ya kawaida katika mizunguko yako ya hedhi.
4.Maumivu ya nyonga(kiuno)
5. Kupata haja ndogo mara kwa mara
6. Maumivu chini ya mgongo
7. Maumivu wakati wa tendo la ndoa
8. Kuwepo kwa uvimbe unaoonekana au unaoweza kuupapasa chini ya kitovu.

MATIBABU

Madhara yake ni makubwa sana katika mfumo wa uzazi ambayo huweza kusababisha kutokua na uwezo wa kubeba mimba na wakati mwingine kutolewa kizazi k**a mtu hatopata matibabu ya mapema.

Malipo ni sh. Elf kumi (10000) tu kumuona daktari, piga namba hio chini kujua utaratibu wa malipo kabla ya huduma.
Usisite kunipigia/sms/whatsapp kwa namba 0742251673. NITAKUSIKILIZA NA KUKUSAIDIA.

LIKE, SHARE pia na wenzako wapate faida hii.

12/05/2020

It's world nurse day

FAHAMU KUHUSU UVIMBE KATIKA OVARI (OVARIAN CYST).O***y ni sehemu katika mfumo wa uzazi wa mwanamke kwaajili ya utengenez...
12/05/2020

FAHAMU KUHUSU UVIMBE KATIKA OVARI (OVARIAN CYST).

O***y ni sehemu katika mfumo wa uzazi wa mwanamke kwaajili ya utengenezwaji wa mayai ya uzazi kila mwezi. Ovarian cysts hutokea pale vifuko vinavyobeba mayai (follicles) kujaa maji kabla au baada ya kutoa yai kwenda kwenye mirija ya uzazi (falopian tubes)

AINA ZA UVIMBE KATIKA SEHEMU YA UTENGENEZWAJI WA MAYAI.
(TYPES OF OVARIAN CYST)
>Kuna aina sita za ovarian cyst ambazo ni Dermond cysts, Endometrioma cyst, Cystadenomas, Follicle cyts, corpus luteum cysts, Polycystic Ovarian Syndrome (PCOS)
Katika aina hizi mara nyingi mtu huweza kuwa nayo moja kati ya hizi na asipate dalili. Dalili huanza kuonekana Cyst hizi zikianza kukua.

DALILI ZA OVARIAN CYSTS

1). Mabadiliko ya mzunguko wa hedhi kila mwezi
2).Maumivu chini ya kitovu pembeni kwenye nyonga na chini ya mgongo
3). Maumivu wakati wa tendo la ndoa
4). Maumivu kwenye matiti
5). Maumivu ya kiuno kabla au wakati wa hedhi

DALILI ZINAZO HITAJI MATIBABU YA HARAKA ZAIDI

Kwa dalili hizi huwenda uvimbe umepasuka na kuvuja. Mtu huweza kupoteza mpaka maisha au kusababisha madhara makubwa zaidi k**a atachelewa matibabu aonapo dalili hizi:

1). Maumivu makali sana ya nyonga au kiuno.
2). Kujiskia kizunguzungu au kupoteza fahamu
3). Homa
4). Kupumua haraka haraka
5). Kupungua uzito kwa haraka bila sababu
6). Uvimbe chini ya kitovu.

MADHARA YA OVARIAN CYSTS.

Cysts hizi huja na kuondoka zenyewe bila kuonesha dalili, zikianza kukua huonesha dalili zilizotajwa hapo juu.
Madhara ni k**a yafuatayo k**a mtu hatopata matibabu ya mapema

1). Kupoteza uwezo wa kuzalisha mayai ya uzazi(hatoweza kubeba mimba).
2). Kansa ya mfumo wa uzazi
3). Kupoteza maisha kabisa.

MATIBABU

Asilimia kubwa ya wanawake hupata ugonjwa huu bila kujua. Cysts huweza kutokea kila mwezi na kuondoka zenyewe bila kuonesha dalili zozote. Zinaposhindwa kuisha zenyewe hukua na kuleta madhara makubwa na dalili k**a ilivyoelezwa hapo juu

Ovari zote zinapokua zimeharibika sana hulazimika mtu kufanyiwa operation na kutolewa kizazi

Kumuona daktari malipo ni sh. Elf kumi tu (10000). Piga namba chini hapo kupata utaratibu wa malipo kabla ya huduma.

Matibabu ya mapema yapo. Wasiliana nami muda wowote nikusikilize kwa namba
0742251673.
issues_afya

MENSTRUAL CRAMP(MAUMIVU YA TUMBO WAKATI WA HEDHI) MAUMIVU YA TUMBO huwapata wanawake wengi sana kila wanapokaribia hedhi...
10/05/2020

MENSTRUAL CRAMP
(MAUMIVU YA TUMBO WAKATI WA HEDHI)

MAUMIVU YA TUMBO huwapata wanawake wengi sana kila wanapokaribia hedhi au wakiwa ndani ya hedhi. Maumivu haya ya tumbo wakati wa hedhi kitaalam tunaita Dysmenorrhea ambayo huanza taratibu na baadae kuwa makali zaidi ambayo huisha ndani ya siku 2 hadi 4.

MAUMIVU haya wanawake wengi huchukulia ni kawaida na wakati kitaalamu si kawaida.

AINA ZA MAUMIVU WAKATI WA HEDHI

1) Primary menstrual cramp.
Aina hii ya maumivu husababishwa na homoni ''prostaglandins" ambayo husababisha kujikunja kwa mfuko wa uzazi hivyo kupelekea damu kutofika kwa wakati katika kuta za mfuko wa uzazi. Aina hii pia huweza kusababishwa na kuwepo kwa wingi wa homoni " leukotrines" .

2)Secondary menstrual cramp
Aina hii ya maumivu husababishwa na magonjwa mbalili mbali katika mfumo wa uzazi ambayo huweza kuwa Uvimbe katika mfumo wa uzazi (Endometriosis, Uterine fibroids) au mashambulizi ya bakteria au fangasi katika mfumo wa uzazi(pelvic inflammatory disease(PID))

●Tabia zinazoweka kupelekea pia maumivu haya ni pamoja na Mtu kukaa muda mrefu bila kulala, mawazo na lishe pia.

DALILI.

Dalili hutofautiana na mtu anaweza pata zote au baadhi:

1. Maumivu makali chini ya kitovu na kiuno
2. kichefuchefu na nakutapika
3. kutokwa jasho
4. kuharisha au kutopata choo kabisa
5. kichwa kuuma
6. Kujihisi kizunguzungu na wengine hupoteza fahamu.

MATIBABU

Wanawake wengi huchukulia ni kawaida kwako kuteseka na hali hii kila mwezi. Maumivu haya si kawaida na huenda yakaashiria madhara makubwa katika mfumo wa uzazi mfano Uvimbe katika kizazi au maambukizi au homoni kuzalishwa kwa wingi ambayo si kawaida.

Kumuona daktari malipo ni sh. Elfu kumi tu (10000), piga namba hio chini kujua utaratibu wa malipo kabla ya huduma.

Usichukulie poa. Kwa yeyote mwenye dalili hizi matibabu yapo.
Nipigie/meseji/whatsapp kwa namba: 0742251673
nikusikilize upate ufumbuzi pia wa tatizo hili.

WAKATI WOWOTE KARIBUNI

Fahamu afya yako ya uzazi. Muda wote mtaalamu wako yuko nawe.
10/05/2020

Fahamu afya yako ya uzazi. Muda wote mtaalamu wako yuko nawe.

TB inatibika bila kujali wewe ni mgonjwa mpya au ulishawahi kutibiwa ikarudi tena. Kwa sasa serikali kwa kushirikiana na...
06/03/2020

TB inatibika bila kujali wewe ni mgonjwa mpya au ulishawahi kutibiwa ikarudi tena. Kwa sasa serikali kwa kushirikiana na wadau na mashirika mbalimbali wameboresha matibabu..uonapo dalili nilizozitaja katika somo lililopita tafadhali fika kituo cha afya chochote kilichopo karibu yako kwaajili ya kupima na kuanza matibabu

NJIA ZA KUEPUKA UGONJWA WA KIFUA KIKUU(TB)1. Epuka kukaa karibu na MTU anayeumwa au kudhaniwa kuumwa kwa kuelekeana USO ...
04/03/2020

NJIA ZA KUEPUKA UGONJWA WA KIFUA KIKUU(TB)

1. Epuka kukaa karibu na MTU anayeumwa au kudhaniwa kuumwa kwa kuelekeana USO kwa USO na kwa ukaribu.

2. Epuka sehemu za misongamano k**a sokoni, kwenye dalala n.k

3. Unapokohoa au kupiga chafya. Ziba mdomo kwa kitambaa kuepuka kusambaza wadudu wa kifua Kikuu.

5. K**a ni muathirika wa UKIMWI hakika unatumia dawa za kuzuia kifua kikuu( ISONIAZID) K**a ulivyoelekezwa kwa kipindi chote cha miezi sita.
6. Epuka matumizi ya dawa za kupunguza kinga ya mwili kwa muda mrefu. Mfano dawa aina ya Steroids k**a vile prednisolone

7. Hakikisha nyumba unayoishi ina mzunguko wa hewa wa kutosha.

8. Epuka tabia hatarishi k**a unywaji wa pombe na uvutaji wa sigara au madawa ya kulevya.

Moja ya malengo ya maendeleo endelevu ni kutokomeza janga la ugonjwa wa kifua kikuu au TB ifikapo mwaka 2030. Mkakati wa...
02/03/2020

Moja ya malengo ya maendeleo endelevu ni kutokomeza janga la ugonjwa wa kifua kikuu au TB ifikapo mwaka 2030. Mkakati wa shirika la afya ulimwenguni, WHO wa kutokomeza TB unataka kupunguzwa kwa vifo vitokanayvo na ugonjwa huo kwa asilimia 90 na kupunguza visa vyake kwa asilimia 80. Malengo haya yatafikiwa iwapo tiba sahihi itapatikana kwa wakati sahihi kwa wagonjwa, pia mikakati ya kuzuia kueneza ugonjwa. Je nchini Tanzania upatikanaji wa huduma ya TB ukoje? Basi ungana nasi kujifunza zaidi kuhusu kujikinga, tiba, ushauri na namna ya kuutokomeza ugonjwa huu katika jamii yetu

Address

Dodoma Regional Referral Hospital
Dodoma

Telephone

+255742251673

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when AFYA YAKO kwanza. posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to AFYA YAKO kwanza.:

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram