Hillary health care,Afya kwanza.

Hillary health care,Afya kwanza. karibu katika page yetu ujifunze juu ya magonjwa ya kitabia na jinsi ya kutibu kupitia mimea na matunda

Mimea na matunda ndio tiba pekee isiyo na madhara kiafya, kwa kulitambua hilo Hillary health care imejizatiti katika kutoa elimu juu ya magonjwa ya kitabia (lifestyle diseses), k**a kisukari, upungufu wa nguvu za kiume, matatizo ya hedhi, vidonda vya tumbo, matatizo ya viungo na mifupa, shinikizo la damu, na namna ya kuyatibu kupitia mimea na matunda.

11/10/2021

HABARI WADAU WA AFYA KWANZA ,HABARI NJEMA NI KUWA SASA DAWA HALISI YA BAWASILI TUMEIPATA NI YA UHAKIKA NA INATATUA TATIZO HILO LINALO SUMBUA WATU WEMGI MPAKA KUFIKIWA KUFANYIWA UPASUAJI, SISI TUNAKUPATIA DAWA NZURI NA UZIMBE HUO UNAPOTEA KABISA ,
KARIBU TUKUSAIDIE
WASILIANA NAMI
0767282485

19/06/2019

ili uweze kupunguza uzito mkubwa unahitaji, miongozo ya lishe sahihi, elimu ya kutosha juu ya lishe na mwili wako pamoja na hamasa (motivation).

Hamasa humfanya mtu azidi kutekeleza kwa juhudi kile alichojifunza bila kuchoka.

Sasa tumekuletea WEIGHT LOSS CONTEST, hii itakusaidia sana wewe ambae uko katika safari ndefu ya kushusha zaidi ya 20kg.

Shindano hili litakua linafanyika kila baada ya miezi miwili mshindi anaibuka na zawadi nono ya zaidi ya 200,000, pia kila wiki kutakua na zawadi ndogo ndogo za kumuhamasisha mwanafunzi wetu.

Lengo ni kukuhamasisha wewe uweze kujitahidi angalau uibuke katika 10 bora na matoeko yake unajikuta umeimarika kiafya na muonekano unaotaka.

Sisi tutakupatia mongozo kila baada ya siku 21 na kila mongozo tunategemea upungue 4kg-7kg.

Ni lishe tu, hatuna dawa, wala mazoezi, tunaimani miongozo yetu ya lishe wala hauhitaji kujinyima kula.

Huna haja ya kushinda njaa.

Jiunge katika shindano hili kwa 10,000 tu ndani ya miezi miwili.

Tuma neno UZITO kwenda whatsapp namba 0767282485

10/04/2019

WENYE UHITAJI WA KUJIFUNZA MLO MZURI UNAO SAIDIA KUTATUA TATIZO LA KUVIMBA KINYAMA SEHEMU ZA HAJA KUBWA SASA UFUMBUZI UMEPATIKANA TUWASILIANE 0767282485 AU 0715913492

10/04/2019

HELLO MARAFIKI

30/09/2018

Habari wadau wangu... K**a unasumbuliwa na bawasili ., yaan kuvimba kinyama sehemu ya haja kubwa,, usiteseke tena karibu nitakusaidia na utapona kabisa....
Unapata choo kigumu.. Yote hayo yataisha..
Dawa zetu ni bora kabisa hazina kemikali ni asili kabisa zimetengenezwa kwa ubora wa hali ya juu.
Like na comment page yangu..
Mawasiliano
0715913492

14/09/2018

FAHAM CHANZO NA TIBA YA TATIZO LA MWANAMME KUKOSA HAMU YA KUFANYA TENDO LA NDOA

Asalaam alaykum warhmatullah wabarakatul mpendwa msomaji wetu ni matumaini yangu kwamba wewe na familia yako mnaendelea vizuri kiafya leo napenda tulijadili tatizo la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa, kwa maneno lugha ya mitaani linaitwa tatizo la kukosa nyege. Tutajadili sababu zinasababisha mwanamme kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa, madhara yanayotokana na hali hiyo na kisha kuona ni nini cha kufanya ili kuongeza hamu ya kufanya tendo la ndoa au kuongeza nyege. Bahati nzuri ni kwamba kuna mambo unayoweza kuyafanya kupunguza ukubwa wa tatizo hili au kuliondoa kabisa. Watu wengine wanamini kuwa hamu ya kufanya tendo la ndoa inapungua kadri umri wa mwanamme unavyoongezeka. Wakati ni kweli kwamba hilo huwatokea wengi,ila sio lazima kwamba hamu ya kufanya mapenzi ipungue umri unapoongezeka. Kuna idadi kubwa tu ya wanaume ambao hamu yao ya kufanya tendo la ndoa imebaki vilevile hata umri wao ulipokuwa mkubwa kabisa. Kwanza tuanze kwa kutazama ukubwa wa tatizo hili.

UKUBWA WA TATIZO LA KUKOSA HAMU YA KUFANYA TENDO LA NDOA

Wanaume wengi hawapenzi kulizungumzia tatizo hili waziwazi na hata wanawake pia. Pamoja na kwamba tatizo hili halijitokezi sana kwa wanaume ukilinganisha na wanawake, inakadiriwa kuwa asilimia 15 hadi 16 ya wanaume wana tatizo hili, kwa lugha nyepesi kuna mwanamme mmoja mwenye tatizo hili baina ya kila wanaume sita au saba. Idadi ya wanawake wenye tatizo hili ni mara mbili ya wanaume. Tatizo hili huwakera zaidi wanaume kuliko wanawake kwa sababu wanaume huchukulia urijali k**a sehemu ya ukamilifu wa mwanamme na hunyongea wanapoona wana mapungufu kuhusu mambo ya mapenzi, tofauti kabisa na wanawake.Idadi ya wanaume wanaoridhika kuishi na tatizo hili ni ndogo sana ukilinganisha na ile ya wanawake. Hata hivyo tatizo la mwanmme kukosa hamu ya kufanya mapenzi limebainika kuwa ndilo linaloongoza katika kuleta migogoro ya unyumba kuliko matatizo mengine yote.

NAMNA UNAVYOWEZA KUGUNDUA K**A UNA TATIZO LA KUKOSA HAMU YA KUFANYA TENDO LA NDOA
Tatizo hili halitokei ghafla k**a vile umelala halafu ghafla asubuhi unaamka una mafua, la hasha. Ni kitu kinachotekea pole pole na pengine mwenyewe usijigundue. Sanasana pima mwenendo wako wa masuala ya mapenzi kwa mwaka uliopita au miezi kadhaa iliyopita. Vile vile kutofanya tendo la ndoa kwa kipindi fulani haimaanishi kutokuwa na hamu ya kufanya mapenzi, pengine una hamu thabiti lakini mazingira hayakukuruhusu. Lakini iwapo hakuna kikwazo cho chote na upo na mwenzi wako halafu inapita wiki bila kufanya tendo la ndoa au unalifanya tendo hilo mara moja au mbili tu kwa mwezi, inabidi uanze kujiuliza maswali. Lakini ieleweke pia kuwa kuhesabu umefanya tendo la ndoa mara ngapi katika kipindi fulani si kipimo pekee cha tatizo hili. Mawazo yako kwa ujumla kuhusu tendo hili ni muhimu pia – jinsi unavyolichukulia na kuliwazia tendo hili kabla, wakati wa tendo na baada ya kumaliza tendo ni muhimu katika kujipima.
Viashiria vingine vyaweza kuwa: kumtomasa mkeo mkiwa ndani tu – chumbani na si penginepo. Iwapo tendo hili unalifanya pale tu mwezi wako anapokuanza na huwa unalifanya k**a mazoea bila kuwa na mawazo ya kushiriki kikamilifu. K**a humwazii mpenzi wako anapokuwa hayupo kwamba angekuwapo ungeweza kufanya naye tendo la ndoa. Vitu hivi k**a vinakutokea basi kuna dalili za kuwa unakosa hamu ya kufanya tendo la ndoa na kwamba inabidi utafute suluhisho.

VISABABISHI VYA TATIZO LA KUKOSA HAMU YA KUFANYA TENDO LA NDOA KWA WANAUME

Tatizo la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa kwa mwanamme linaweza kusababishwa na vitu vingi sana. Sababu hizo zinaweza kuwa za kimaumbile au kisaikolojia au za mchanganyiko wa vitu hivyo viwili. Hebu tuone baadhi ya vyanzo vya tatizo hili.

Mahusiano Baina Ya Mwanamme Na Mwanamke
Matatizo ya mahusiano kati ya mwanamme na mwanamke yana mchango mkubwa sana katika kusababisha tatizo la kukosa hamu ya mapenzi. Jee, unapata raha na una amani katika mahusiano yako na mpenzi wako? Huna wasiwasiwo wote na mahusiano yenu? Haya ni maswali ya msingi ya kujiuliza.
K**a mahusiano yako na mpenzi wako yamekuwa ya miaka mingi sana, unaweza kuwa umemzoea mno mkeo kiasi kwamba ukaanza kukosa hamu ya kufanya naye tendo la ndoa. Hili nalo hutokea mara nyingi.
K**a kuna mambo yanasababisha tendo la ndoa lisifanyike kwa urahisi, ufanisi na kufurahia, hamu ya kufanya tendo hilo inaweza kupungua. Kwa mfano, k**a mwanamme anawahi kufika kileleni au k**a ana matatizo ya kushindwa kusimamisha uume tendo zima la ndoa halitakuwa la kukufurahisha sana hivyo unaweza kupoteza hamu ya kulifanya. Hebu fikiria tunda linalokufurahisha sana ukilila, ukilikosa kwa siku kadhaa, utalikumbuka na kulitafuta lakini ambalo halikufurahishi sana ukilila hutalikumbuka na kulitafuta.

Mawazo Mengi Na Uchovu
Matatizo ya kikazi na hadhi yako kazini vyaweza kuchangia. K**a unabezwa sana kazini na kujiona hutimizi kazi yako ipasavyo au k**a unachoka sana kazini unaweza pia kukosa hamu ya kufanya mapenzi urudipo nyumbani. Kukosa mpango mzuri wa shughuli zako za kila siku na kujaribu kulazimisha kufanya mapenzi katikati ya ratiba yako iliyojaa. Mahusiano ya kimapenzi yanataka yatengewe muda wake na unaotosha.

Msongo Wa Mawazo
Msongo wa mawazo (depression) unatofautiana na kukosa raha au kujisikia si mtu wa thamani kwa kipindi kifupi. Msongo wa mawazo ni ugonjwa wa hali ya kuwa na mawazo makali ya muda mrefu ya kukukosesha raha kutokana na kujisikia si mtu wa thamani au kukosa starehe katika vitu ulivyozoea kuvifanya na kukufurahisha hapo zamani. Mawazo ya namna hii huathiri mwenendo wako wa maisha yako pamoja na matamanio yako ya kimapenzi.

Matumizi Ya Madawa Na Pombe
Matumizi ya baadhi ya madawa na unywaji wa pombe wa kupindukia huweza kuleta tatizo hili la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa. Madawa yanayochangia tatizo hili ni pamoja na:
– madawa ya high blood pressure
– madawa ya kuondoa msongo wa mawazo
– madawa yote yanayozuia ufanyaji kazi au uzalishaji wa testosterone, kwa mfano, cimetidine, finasteride na cyproterone
– na mengineyo

Umri Kuwa Mkubwa
Homoni ya msingi sana kuhusiana na masuala ya mapenzi huitwa testosterone. Kwa mwanammme homoni hii hutolewa kwa kiwango kikubwa na korodani na kwa mwanamke hutolewa na ovari. Homoni ikipungua katika mwili wa binadamu, humfanya apoteze hamu ya kufanya tendo la ndoa. Kiwango cha testosterone katika mwili wa mwanamme hupungua kwa asilimia 1-2 kila mwaka kadri mwanamme anvyozidi kuwa na umri mkubwa. Kiwango cha testosterone kikishuka sana katika mwili wa mwanamme huyu humfanya asiwe na nguvu, ashindwe kutuliza mawazo kwenye jambo alifanyalo na apoteze hamu ya kufanya mapenzi.

Matatizo Katika Mfumo Wa Homoni
Tumeshaona kwamba upungufu wa homoni inayoitwa testosterone unasababisha kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa. Matatizo mengine katika mfumo wa homoni huchangia tatizo hili. K**a thyroid haitoi homoni za kutosha, tatizo hili huweza kutokea ingawa mchango wa thyroid katika tatizo hili ni mdogo sana. Thyroid ni kiungo cha kuzalisha homoni kilichopo katika eneo la shingo.
Tatizo hili linaweza kutokea pale homoni zinapozalisha kitu kinachitwa prolactin kwa kiwango kikubwa mno na kukisambaza ndani ya mfumo wa damu. Hali hii kiutaalamu huitwa hyperprolactinaemia.

Matatizo Ya Kiafya
Matatizo ya kiafya ya muda mrefu husababisha kupungua kwa hamu ya kufanya tendo la ndoa. Matatizo ya moyo ya muda mrefu, kuwa na kisukari kwa muda mrefu, kansa ya muda mrefu na hali ya kuwa na unene wa kuzidi kiwango ni baadhi tu ya matatizo yanayochangia tatizo hili.

MATIBABU YA TATIZO LA KUKOSA HAMU YA KUFANYA TENDO LA NDOA KWA WANAUME
Kuna mambo ambayo unaweza kuyafanya kuongeza na kudumisha hamu ya kufanya tendo la ndoa. Tatizo hili halijapatiwa dawa za kwenye mahospitali isipokuwa pale unapogundulika kuwa una kiwango kidogo cha testosterone ambapo utaandikiwa namna ya kukiongeza kiwango chako. Fanya yafuatayo kuongeza hamu yako ya kufanya mapenzi.
1. Tafuta mchezo ambao unaweza kushiriki au fanya mazoezi k**a vile ya kutembea au kukimbia. Kila siku ufanyapo mazoezi yako jaribu kila siku kufikia kiwango cha juu zaidi ya kile ulokwisha kifikia.
2. Inasaidia kufahamu kuwa ni asilimia 40 hadi 50 ya matendo ya ndoa mnayoyafanya yatawaridhisha wote wawili. Kukosa kumridhisha mwenzio iwe changamoto ya kukufanya ufanye utafiti na utundu wa kuboresha tendo mtakapokutana tena.
3. K**a nilivyodokeza hapo juu, jaribuni kwa pamoja kujadili jinsi ya kuboresha namana yenu ya kushiriki katika tendo la ndoa kila mmoja akieleza kile ambacho angependa afanyiwe. Inasaidia kusoma maandishi kutoka sehemu mbalimbali na kutazama mikanda mbalimbali.
4. Kufanya tendo kwa kush*tukiza inapendeza wakati fulani. Lakini hili kidogo linaweza kuwa si zuri ukizingatia majukumu ya kila siku ya maisha ya sasa, si rahisi kupata muda wa kutosha wa kustarehe na mpenzi wako. Kuwa na mpango na ratiba ni bora zaidi na inasaidia kuleta hamu mtu anapokisubiri kitu kilichopangwa siku fulani na muda fulani – fikiria unaposubiri mechi kubwa ya timu yako. Mletee zawadi mpenzi wako, weka muziki mororo ulikuwa unaupenda siku zile, zimisha simu na hakikisha kuna mazingira ya utulivu na ukimya.
5. Hamu huongezeka inapoona kitu kipya. Ukienda na mwenzi wako kwenye sherehe nje ya nyumba yenu, utapata fursa ya kumwona mkeo kwa namna nyingine. Utaweza kuuona uzuri wake na yeye pia atakuona wewe kwa namna nyingine. Wote mtakumbuka vitu ambavyo kila mmoja wenu vilimvutia kwa mwenzie

MATIBABU YA TATIZO LA KUKOSA HAMU YA KUFANYA TENDO LA NDOA KWA WANAUME KUPITIA VYAKULA ASILI

Historia yetu inaonesha kuwa kwa kipindi kirefu, wanawake na wanaume wamekuwa wakitumia chakula kumvutia mpenzi. Mara nyingine chakula hicho kinakuwa kinaongeza hamu ya kujamiiana na kuna wakati ni harufu au ladha ya chakula hicho ndiyo inayokufanya kupata hisia hizo. muonekano wake, ladha yake unapokila, uhaba wake.

ASALI
Pamoja na utamu wake, asali ina nafasi kubwa ya kuongeza hamu ya kujamiiana kwakuwa ina aina zote za madini ya Vitamin B, ambayo ndio yanasaidia sana kuupa mwili nguvu.

Unaweza kula vijiko kadhaa kila siku, wengine huichanganya wakiwa wanaotengeneza keki, kuipaka kwenye mkate au chakula chochote.

SHAYIRI

Maji ya shayiri asubuhi au jioni yanasaidia kuongeza hamu ya kujamiiana. Shayiri madini ya L-arginine yanayoongeza homoni za testosterone, pia ina wingi wa kundi la Vitamin B. Shayiri huuzwa bei nafuu na ni njia rahisi sana ya kuongeza msukumo wa damu, jambo ambalo hutokea unapofanya mapenzi. Shayiri inapotumiwa kwa muda mrefu inasaidia kupunguza uwezekano wa kupata matatizo ya kusimama kwa uume.

PARACHICHI

Wataalamu wa masuala ya mapenzi wanasema kuwa parachichi linaingia kwenye kundi hili kwakuwa umbo lake linafananishwa na maumbile ya mwanaume au mikunjo katika mwili wa mwanamke na kwamba ulaini wake na jinsi linavyotoa majimaji huongeza hisia za mapenzi. Yanaweza kuliwa yenyewe au kwa kuchanganywa kwenye vyakula vingine.

Yana kiwango kikubwa cha mafuta na vitamin E vyenye kazi ya kuongeza msukumo wa damu, hivyo kuongeza kiwango cha utengenezwaji wa testosterone. K**a hutaki kutumia parachichi kwa kazi hii, basi litakusaidia kwa kung’arisha ngozi kutokana na madini ya vitamin E.

MBEGU ZA MABOGA

Mbegu za maboga zina wingi wa madini ya tyrosine (aina mojawapo ya asidi aina ya amino inayosaidia kuchangamsha mwili). Mbegu hizi pia zina virutubisho vingi vinavyosaidia kuongezeka kwa msukumo wa damu mwenye viungo vya uzazi.

Unaweza kuzioka kwenye oveni, kuzisaga au kula kwa kuzichanganya na vyakula vingine, ikiwamo asali pia – ili kuongeza faida zaidi.

TIKITI MAJI
Wataalamu wanasema kuwa watu wengi hawajui jambo moja kuhusu tiketi: kwamba k**a ambavyo tiketi linaweza kukata kiu yako kwa wingi wa maji yaliyomo, ndio hivyo hivyo inavyoweza kukusaidia kwenye maswala ya kujamiiana. Utafiti umeonesha kuwa tunda hilo lina kiwango kikubwa cha viambata aina ya citrulline, ambayo ina kazi sawa na dawa aina ya Vi**ra kwa mwanaume.

TANGAWIZI
Tangawizi inafanya damu iende kwa kasi jambo linaloweza kusababisha mwili uweze kupata msisimko wa kimapenzi kirahisi sana. Pia inasaidia kuboresha mfumo wa usagaji wa chakula, jambo linalosaidia sana kukufanya ubaki kuwa na hamu ya kufanya mapenzi k**a umekula chakula kingi.

CHOCOLATE

Wataalamu wanasema kuwa dawa pekee ya ukweli kwenye maswala ya mapenzi ni cocoa. Cocoa inachochea uzalishaji wa homoni zinazofanya ujisikie vizuri aina ya serotonin na dopamine, na ina kemikali aina ya phenylethylamine, inayotengenezwa kwa wingi kwenye ubongo unapoingia mapenzini. Cocoa inafanya kazi hii hasa inapochanganywa na chokoleti kwakuwa inayeyuka kirahisi na kuleta hamasa ya kimapenzi mdomoni. Kwakuwa chokleti ni nzuri unapoila—na inafanya tujisikie vizuri baada ya kuila—zawadi inayomfanya mtu apate hisisa nzuri siku zote lazima itapendwa.

MATIBABU YA TATIZO LA KUKOSA HAMU YA KUFANYA TENDO LA NDOA KWA WANAUME CHINI YA UONGOZI WA GREEN HEALTH CONSULTATION CENTER

Mpendwa msomaji K**a una tatizo la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa na umejaribu njia hizo hapo juu bila kupata mafanikio ya kukuridhisha,tunakukaribisha ofisini kwetu ilala,Dar es salaam pia unaweza kutuandikia Ujumbe wa Meseji katika Namba na email zetu ili upate maelezo na ushauri zaidi 0767282485,WhatsApp 0715913492
Green health consultation center tuna Dawa za kuongeza hamu ya tendo la ndoa na Dawa za kila ugonjwa karibu sana tuweze kukuponya tatizo lako
Mpendwa msomaji nashukuru Kwa kuchukua muda wako kufatilia makala zetu za afya tunasema ASANTE NA MUNGU AKULIPE KHERY PIA IKIWA UNA MAONI AU USHAURI TUANDIKIE UJUMBE KUPITIA EMAIL AU NAMBA ZETU HAPO CHINI
KUSOMA ZAIDI MAKALA MBALIMBALI ZA AFYA TEMBELEA
Glob yetu.
Makala hii imeandaliwa na kuandikwa na uongozi wa green health consultation .cont 0767282485

08/07/2017

Hii ni kwa wadada ,,,,,
acha kuteseka na maumivu makali ya tumbo wakati wa hedhi ...acha kuhangaika na mzunguko usioeleweka rudisha Homoni zako katka mpangilio ulio sahihi,,,Umeshindwa kushika mimba karibu nitakusaidia.

nitafute nikupatie dawa ya Asili isiyo na kemikali iliyotengenezwa kwa mimea ya asili,,,,,, Jipatie Soy utatue matatizo yako..

08/07/2017

habari wapedwa wasomaji wa page yangu ..
tunaendelea kuwakaribisha kujipatia bidhaa zetu za asili zinazotibu Magonjwa Mbalimbali,,,
wenye kusumbuliwa na figo,tezi dume,upungufu wa nguvu za kiume, Mzunguko wa hedhi haueleki,,,, Karibuni sana

09/04/2017

Habari wapenzi wasomaji wa blog yangu .. polen na majukumu ..
bado nawakumbusha ile dawa yetu inayoendelea kufanya maajabu hasa wa wanaume bado inapatika na watumiaji wanaleta majibu mazuri sana .. kiufupi dawa inafanya vizuri sana ..

mwambie rafiki yako ndugu jmaa waache kufumia vi**ra kuna dawa ya asili inafanya vizurii sana .. haisumbui bali inarudisha mufumo mzima wa damu,, na kurudisha msuli kuwa imara zaidi,
kwa wale walioadhhirika na punyeto karibuni sana ,,

0715913492
0767282485

19/02/2017

REJESHA HESHIMA YA NDOA YAKO SASA.
hakikisha unatuandikia kwa whatsap/text kwenye namba 0715913492.
TUMIA DAWA YA ASILI ILIYOTENGENEZWA KWA KIWANGO CHA HALI YA JUU
Je wewe ni miongoni mwa watu wenye matatizo haya:-
-Kwa kuuwahi kufika Kileleni
-Kutokuweza kurudia tendo la ndoa
-Kukosa hamu ya tendo la ndoa
-Kuto kuwa na uwezo wa kuhimili tendo la ndoa kwa muda mrefu.
~Matatizo ya Figo
~Upungufu wa mbegu za kiume /Mbegu dhaifu kutokana na upigaji punyeto na athari ya magonjwa k**a kisukari na vidonda vya tumbo
Jipatie dawa iliyotengenezwa kwa mimea aina ya butea superba ambayo ni mimea inayopatikana katika nchi za Thailand,china,India na Vietnam kwa bei nafuu kabisa. utatumia dawa ina vidonge sita vilivyotengenezwa kiasili na kuhifadhiwa katika ubora wa hali ya juu.
Dawa hii itakusaidia,
~Husafisha na Kuongeza utendaji wa kazi wa figo.
~Huongeza nguvu za kiume.
~Huongeza namba za mbegu za uzazi za kiume.
~Husawazisha mzunguko wa damu Kwenye uume.
~Huongeza nguvu na hamu ya tendo la ndoa.
~Huongeza nguvu za mbegu za kiume kupenya katika yai la mwanamke.
ni vizuri kulike page na kushare na marafiki pindi usomapo makala hii ili tuweze kuwafikia watu wengi zaidi popote Tanzania.

23/01/2017

Ugonjwa wa kifafa ni nini?

Huu ni ugonjwa amabao unasabababishwa na seli za mishipa ya fahamu zilizopo kwenye ubongo kutoa umeme[impulses] mwingi kuliko kawaida kwenda kwenye misuli na sehemu zingine za mwili, na kusababisha mtu kupata dalili k**a vile kuishiwa nguvu, kichwa kuuma, kuchanganyikiwa, mwili kukak**aa na hata kupoteza fahamu. Hali hii hujirudia mara kwa mara.

Ifahamike kuwa, aina ya kifafa inayojulikana sana mitaani ni ile ambayo mtu anakak**aa na kupoteza fahamu, japokuwa kuna aina za kifafa ambazo mtu hakak**ai wala kupoteza fahamu, k**a tutakavyoona hapo baadae.

mwaka 2013 ugonjwa huu uliua zaidi ya watu laki moja duniani, 80% wakiwa waafrika.

Mgonjwa huyu huweza kuanguka mara kadhaa kwa mwezi lakini anaweza asianguke kabisa k**a anafuata masharti na utaratibu mzuri wa matibabu…

Chanzo cha ugonjwa huu ni nini?

chanzo kikuu cha ugonjwa huukwa watu wengi hua hakifahamiki lakini baadhi ni moja ya sababu za kuugia kifafa.

Kurithi; familia na koo zingine zinakua na ugonjwa huu hivyo watoto na wajukuu huzaliwa tayari na ugonjwa huu.

Kuumia kichwa: ajali zinazohusisha kuumia kwa kichwa huweza kusababisha kuumia kwa mishipa ya fahamu na mtu kuugua kifafa.

Magonjwa mengine; kuna magonjwa mtu akiugua maishani mwake baadae huweza kupata kifafa kwasababu magonjwa hayo yanavyoharibu mfumo wa ubongo.. mfano homa ya uti wa mgongo kitaalamu k**a meningitis.

Uvimbe kwenye ubongo: matatizo ya uvimbe kwenye ubongo k**a kansa huweza kusababisha mtu kuugua kifafa.

Kiharusi; huu ni ugonjwa ambao husababishwa na damu kushindwa kupita vizuri kwenye ubongo au kupasuka kwa mishipa ya damu ya ubongo hali hii husababisha mtu kupooza nusu ya mwili wake na huweza kuugua kifafa baadae.

Matatizo wakati wa kuzaliwa: wakati mwingine mototo huzaliwa kwa shida sana kwa njia ya kawaida kiasi kwamba kichwa chake hubanwa sana wakati wa kupita na hali hii huweza kumsababishia kifafa kwanzia utotoni.

Matatizo ya utengenezaji wa mtoto tumboni; wakati mwingine ile miezi mitatu ya kwanza ambayo mtoto ndio anapata viungo tumboni huweza kutokea kasoro kwenye mfumo wa fahamu za kwenye ubongo na kumfanya apate kifafa akizaliwa.

Magonjwa ya uzee yanayoathiri ubongo; kuna magonjwa huharibu ubongo wakati wa uzee na magonjwa haya huweza kusababisha kifafa kipindi hicho.

Kuna aina mbili kubwa za kifafa…

1)Primary generalized seizures

Hii ndio aina ya kifafa ambayo inafahamika sana mitaani; na inahusisha mgonjwa kuk**aa, na kupoteza fahamu, pamoja na dalili zingine k**a vile kutoa povu mdomoni, na kujisaidia haja kubwa na/au ndogo bila kujitambua akishikwa na hali hiyo.

Pia wengine hupatwa k**a na wazimu au kuchanganyikiwa kwa muda kabla au baada ya kushikwa na hali hiyo.

2)Partial seizures

Aina hii ya kifafa ni ile ambayo haihusishi muhusika kupoteza fahamu na kukak**aa!! Bali hushikwa na hali fulani k**a ya bumbuwazi kwa dakika kadhaa; Wengine huwa na dalili zisizoeleweka za mara kwa mara k**a vile kusihiwa nguvu, kizungu zungu, kichwa kuuma sana (bila sababu ya kiafya inayojulikana), na kadhalika. Aina hizi za kifafa ziko nyingi, na dalili hutofautiana kwa kadri ya aina ya kifafa!!

vipimo vinavyofanyika kugundua kifafa…

Ugonjwa huu unaweza kutambulika kwa daktari kuchukua historia ya dalili zinazomkabili muhusika tu(hakuna kipimo ambacho kinaweza kutambua kifafa kwa asilimia 100); Kuna kipimo kinachopima jinsi ubongo unavyotoa taarifa za umeme (ELECTROENCEPHALOGRAM-EEG), ambacho kinaweza kutambua kifafa, lakini kipimo hiki kinaweza kikaonekana kuwa hakina shida, na bado mtu akawa na tatizo hilo la kifafa. Hivyo basi, kifafa ni moja kati ya magonjwa machache ambayo kutambulika kwake kunategemea sana ujuzi na utaalamu wa daktari katika kuunganisha dalili za mgonjwa kuliko vipimo!!

Hata hivyo, mara nyingi nyingi mgonjwa hupimwa vipimo tofauti ili kuweza kujua chanzo cha ugonjwa… mfano
• Uwezo wa kufanya kazi figo
• Uwezo wa kufanya kazi maini
• Kupima maji ya uti wa mgongo
• Kupima Kaswende
• Picha ya ubongo mfano CT SCAN.
matibabu

K**a kawaida chanzo cha ugonjwa kikipatikana mgonjwa huanzishiwa matibabu lakini k**a mgonjwa alikua tayari ameshapata madhara kwenye ubongo kulingana na chanzo husika ataendelea kua na kifafa.

Ugonjwa wa kifafa hauponi kabisa, USIMALIZE FEDHA ZAKO KWA WAGANGA WA KIENYEJI naomba nisisitize hili, ukishaambiwa una kifafa au mgonjwa wako ana kifafa fuata utaratibu wa matibabu yaani kumeza dawa siku zote za maisha yako na kufuata baadhi ya masharti na utaishi maisha ya kawaida kabisa.

Matibabu yasiyo ya dawa wakati mgonjwa amek**atwa na kifafa:{non pharmacological treatment}
• Mzuie mgonjwa asijiumize kwa kuweka kitu laini chini ya kichwa chake, ondoa vitu vikali karibu yake k**a kisu, sindano au vyuma.
• Usilazimishe kitu chochote kwenye mdomo wa mgonjwa.
• Usimshike kuzuia mizunguko yake
• Weka kichwa alale anaangalia upande mmoja ili kutoa mate mdomoni.
• Kaa na mgonjwa mpaka degedege ziishe
• Usiweke chochote mdomoni kwa mgonjwa k**a dawa au chakula mpaka apate fahamu zake.
Mtu mwenye kifafa hali hii ya kuk**atwa na degedege za kifafa sio ya ajabu sana ila ukiona dalili hizi mkimbize hospitali..
• Degedege za kifafa zaidi ya dakika kumi
• Kutapika sana
• Kushindwa kuona vizuri
• Kupoteza fahamu
• Kichwa kuuma sana.
matibabu ya dawa..

Mgonjwa akishagundulika na kifafa ataanzishiwa dawa k**a carbamizapine, phenorbabitone au zingine za kifafa na atakua anameza kila siku ili kuzuia hali hiyo ya kuanguka na kuoteza fahamu na akifuata masharti ataishi maisha ya kawaida kabisa.

mambo yanayofanya kupata degedege za kifafa mara kwa mara..
• Kukosa usingizi kwa muda mrefu
• Mianga na miale ya disco
• Unywaji wa pombe
• Kuishiwa sukari mwilini wakati wa akisikia njaa kali.
• Kutomeza dawa k**a ilivyoelekezwa

07/11/2016

FAHAMU ATHARI ZA UGUMBA NA TIBA ZAKE.

Ugumba ni tatizo ambalo limekuwa likiikumba jamii zetu mbalimbali kwa muda mrefu sana, na kwa kiasi kikubwa wanawake wamekuwa wakitupiwa lawama kuwa wao ndio sababu ya kukosa mtoto! Ukweli ni kwamba tatizo hili la ugumba linaweza kusababishwa na mwanaume au mwanamke! Miaka ya hapa karibuni taizo hili limekuwa likiongezeka zaidi sehemu mbalimbali duniani ikiwemo na hapa nchini.

Tafiti zinaonesha asilimia 12 mpaka 28 ya wenzi duniani wanakadiriwa kuwa na tatizo la ugumba, na asilimia 40 ikisababishwa na wanaume, 40 wanawake na 20 ikiwa ni mchanganyiko wa matatizo kwa mwanaume na mwanamke. Njia mbalimbali za kutibu tatizo hili zimebuniwa na kusaidia watu wengi.

UGUMBA NI NINI?

Ugumba ni hali ya kutoweza kupata ujauzito kwa kipindi cha mwaka mmoja au zaidi kwa wenzi ambao wamekuwa wakifanya mapenzi bila kutumia njia zozote za uzazi wa mpango. Hali hii inaweza kutokea kutokana na mwanaume au mwanamke, ingawa baadhi ya watu wamekuwa wakidhani wanawake peke yao ndio ambao hupata tatizo hilo.

UTASA NI NINI?

Utasa ni hali ya mwanamke kutoweza kabisa kushika ujauzito au mwanaume kutoweza kabisa kusababisha ujauzito kwa mwanamke.

KUNATOFAUTI GANI KATI YA UGUMBA NA TASA?

Mtu tasa hana uwezo wa kupata mimba au kumpa mtu mimba kabisa, wakati mgumba ana uwezo wa kuja kupata mimba iwapo tatizo likaondolewa.

NINI HUSABABISHA UGUMBA?

Kuna sababu mbalimbali ambazo huweza kupelekea ugumba kwa mwanaume au mwanamke, tutaenda kuona baadhi ya sababu ambazo hujitokeza mara kwa mara.

WANAUME

Tatizo la ugumba kwa wanaume mara nyingi hutokana na kiasi kidogo cha mbegu za kiume, mbegu za kiume zinazoshindwa kutembea, mbegu za kiume zenye umbo lisislo la kawaida na kuziba kwa mijira ya mbegu za kiume.

Tatizo kwenye mbegu za kiume linaweza kutokana na;

Kuvuta sigara
Dawa k**a matumizi ya bangi kwa wingi,
Mionzi
Unywaji wa pombe
Kemikali k**a DDT, risasi (lead)
Kuziba kwa mirija ya kupitisha manii na shahawa; mbegu za kiume zinashindwa kupita.
Wanawake

Ugumba kwa wanawake mara nyingi hutokana na sababu kuu mbili ambazo ni;

Kuziba kwa mijrija ya kupitisha mayai
Ovari kushindwa kutoa mayai ya uzazi.
Mirija ya kupitisha mayai inaweza kuziba kutokana na;

Ugonjwa wa Pelvic Inflammatory Disease (PID) ambao unatokana kuwa na magonjwa ya zinaa yasiyotibiwa k**a kisonono na klamidia.
Utoaji mimba usio salama (unsafe abortions)
Upasuaji maeneo ya kiunoni
Ugonjwa wa endometriosis
Ovari kushindwa kutoa mayai ya uzazi inaweza kutokana na;

Umri mkubwa wa mwanamke, hasa miaka 35 – 40 na kuendelea.
Uvutaji wa sigara
Saratani ya Ovari
Mionzi
Ugonjwa wa Polycystic ovarian disease
Sababu nyingine za ugumba kwa mwanamke zinaweza kuwa;

Makovu katika mji wa uzazi kutokana na kutoa mimba.
Mabonge ya kizazi (fibroids)
Kuziba kwa shingo ya uzazi
Kulegea shingo ya uzazi
Kisukari
Matatizo ya tezi ya shingo
Kufanya mazoezi ya kupitiliza (excessive exercising)
Tabia Hatarishi

Tabia hizi huweza kuongeza uwezekano wa mtu kupata hali ya ugumba au utasa maishani mwake;

Kutoa mimba kiholela, hupelekea kuwa na makovu katika mji wa uzazi na kulegeza shingo ya uzazi.
Magonjwa ya zinaa yasiyotibiwa, hupelekea mirija kujaa maji au kuziba kwa makovu baada ya maambukizi kuisha.
Kufanya kazi kwenye mazingira yenye joto kali sana, hii huathiri zaidi wanaume. Hupelekea utengenezwaji wa mbegu ambazo ni chache au hazina nguvu za kutosha kurutubisha yai la mwanamke.
Uvutaji sigara
Vipimo Vya Kujua Ugumba

Vipimo mbalimbali vinapatikana ili kuwezesha kujua tatizo la ugumba linatokana na nini. Licha ya uwezo wa vipimo hivi, sababu ya ugumba katika asilimia 10 au zaidi ya watu wenye tatizo hili inaweza isijulikane kabisa. Ni vizuri kwa wenzi wote wawili wenye tatizo hili kuonana na daktati kwa ajili ya ushauri na vipimo.

Kwa wanaume hufanyika;

Kipimo cha manii (seminalysis) kuona k**a manii zipo za kawaida na kwa kiwango kinachoatakiwa. Manii huchukuliwa kwa kondomu maalum wakati wa kufanya mapenzi au kwa kupiga punyeto.
Homoni za kiume kwenye damu; kipimo hiki hupima homoni za testosterone na Follicle Stimulating Hormone(FSH) ambazo huusika katika utengenezaji wa mbegu za kiume.
Kwa wanawake kuna vipimo vingi ambavyo huweza kufanyika, vikiwemo;

Hysterosalpingography – hutazama mirija ya uzazi (falllopian tubes) k**a imeziba au la. Pia huonesha k**a tumbo la uzazi lina vivimbe.
Ultrasound – kipimo hiki huonesha k**a kuna vivimbe kwenye tumbo la uzazi, pia kwenye ovari k**a kuna magonjwa yanayoweza kusababisha ugumba k**a polycystic ovarian syndrome.
Homoni za k**e katika damu – kipimo hiki hupima homoni za oestrogen na Follicle stimulating hormone ambazo huuusika kwenye kuandaa yai la uzazi kutoka kwenye ovari na upandikizaji kwenye mji wa uzazi.
Endometrial biopsy – tishu za mji wa uzazi huchukuliwa kuchunguza k**a yai la uzazi limetoka. Pia huweza kuonesha k**a kuna saratani ya mji wa uzazi au vinyama kwenye mji wa uzazi.
Matibabu ya Ugumba

Sababu ya ugumba inapojulikana matibabu yanaweza kufanyika na hali hii ikaisha, ingawa wengine licha ya sababu kujulikana bado wanaweza kushindwa kupata watoto baada ya matibabu hayo. Hivyo, matibabu ya tatizo hili yanahitaji uvumilivu na uelewa kuwa wakati mwingine yanaweza yasiwe na mafanikio haraka au kabisa k**a tunavyotarajia. Kuna njia mbalimbali za kutibu ugumba, hizi zote zikijumuisha kuondoa tatizo linalosababisha mimba ishindwe kutunga au kusaidia mimba itunge.

Kuna njia za upasuaji hasa pale ambapo kuna vivimbe kwenye tumbo au mirija kuziba, dawa kwa ajili ya kusaidia mayai ya uzazi yatoke na teknolojia za kusaidia kuzaa (assistive reproductive technologies). Pia ushauri kutoka kwa mtaalamu wa afya ni sehemu muhimu ya matibabu, ukijumuisha siku ambazo ni rahisi mwanamke kushika ujauzito.

Upasuaji.

Mirija iliyoziba, vivimbe kwenye mji wa uzazi au kuta za uzazi kushik**ana huweza kutibiwa kwa njia za upasuaji. Matibabu haya husaidia kuongeza uwezekano wa wenzi kupata mtoto.

Dawa.

Matatizo ya ugumba yanayotokana na ovari kushindwa kutoa mayai ya uzazi huweza kutibiwa kwa dawa. Dawa hizi hutumika kuziwezesha ovari kutoa mayai ya uzazi ili yaywe tayari kurutubishwa. Mara nyingi huweza kusababisha kutoa mayai mengi katika mzunguko mmoja na kusababisha ujauzito wa watoto wengi (mapacha au zaidi) pale yanaporutubishwa.

Teknolojia za kusaidia kuzaa (assistive reproductive technologies).

Hizi ni njia za kitaalamu ambazo zinatumika kusaidia wenzi kupata ujauzito kutokana na tatizo kwa mwanaume au mwanamke. Njia hizi ni k**a Artificial Insermination na In Vitro Fertilization.

Artificial Insermination. Njia hii hutumika pale ambapo mbegu za kiume zipo kwa kiasi kidogo. Mbegu za kiume hukusanywa na kuingizwa kwenye mji wa uzazi kwa njia za kitaalamu.
In Vitro Fertilization. Njia hii hutumika hasa pale mirija ya mwanamke imeziba kabisa. Mayai na mbegu za kiume hukusanywa kitaaalamu na kisha yai kuchavushwa. Baada ya hapo yai lililochavushwa hupandikizwa kwenye mji wa uzazi.
Kuongeza uwezekano wa kupata mtoto na mwenzi wako, inashauriwa;

Acha kuvuta sigara.
Punguza vinywaji vyenye caffeine.
Kufanya mapezi siku 1 kabla ya yai kutoka (ovulation).
Kuacha kusafisha ukeni kwa kemikali (douching).
Njia za Kuzuia Ugumba

Pata matibabu ya magonjwa ya kisukari, tezi ya shingo(thyroid) na magonjwa ya zinaa k**a unayo.
Pata mlo kamili wenye virutubisho vya kutosha hasa mlo wenye mboga za majani na matunda kwa wingi.
Acha kuvuta sigara
Acha unywaji holela wa pombe
Tatizo hili huathiri wenzi wengi kisaikolojia kwa kuleta hasira, majuto, msongo wa mawazo na hata kusababisha mvurugano katika mahusiano yao. Katika nchi zetu za kiafrika, wanawake wamekuwa wahanga wakubwa wa tatizo hili. Ni vizuri wenzi washirikiane katika hili, kwa kupeana moyo na kufuatilia matibabu kwa pamoja. matibabu yanaposhindwa kabisa kuleta mafanikio, wenzi wanaweza kuasili mtoto/watoto k**a watakuwa na utayari.
0715913492 au 0767282485

Address

47
Dodoma

Telephone

+255715913492

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Hillary health care,Afya kwanza. posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to Hillary health care,Afya kwanza.:

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram

Category