17/05/2022
USOMAJI WA NYOTA
JUMANNE 17/5/2022
NDOO (K, W) 20/1 - 19/2
Uko tayari kwa mambo makubwa na yaliyo bora zaidi. Ni wakati wa kuona kwamba changamoto zako zote za hivi majuzi zimekuwa zikikusaidia kukua kiakili. Haukukusudiwa kukwama katika siku za nyuma ulikuwa ukiota tu maisha yako yajayo ambayo unakusudiwa kuyaishi.
MBUZI (J, V) 22/12 - 19/1
Ikiwa umekuwa ukiomba kitu yaani kufanya maombi juu ya kitu fulani, maombi yako yanakaribia kujibiwa. Roho iko nyuma ya mgongo wako na iko karibu kukuletea jambo lako kuu ulilokuwa ukilitaka. Ni kitu ambacho umekuwa ukikitamani. Nyota kwa sasa zinajipanga kwa ajili yako. Nasikia kutakuwa na mshangao (surprise) mzuri sana!
SAMAKI (L, X) 20/2 - 20/3
Barabara iliyo mbele yako inaweza kuonekana na kuwa ukungu sana kwa sasa, lakini kuwa na wasiwasi na mashaka hakutabadilisha matokeo ya kile kitakachokuja. Chukua hatua hizo mbele ambazo umekuwa ukizimaanisha kuzichukua na kuzifanya na uache kuruhusu uwoga ukurudishe nyuma.
PUNDA (A, M, Y) 21/3 - 20/4
Chochote ambacho kimekusudiwa kwako, kitakuwa kwako kukipokea. Chochote ambacho hakikusudiwa kwako, basi jua kuwa kitu bora zaidi kinakuja mahali pake. Huu ni msimu ambapo yale ya zamani ambayo hayakufai yanatolewa nje na kuingizwa mengine mapya ambayo utayafurahia na unayolingana nayo kulingana na hadhi yako ya sasa. Karibisha mabadiliko na uyapokee vizuri!
NG'OMBE (B, N, Z) 21/4 - 20/5
Kuna mtu anakuja maishani mwako na uhusiano huu na mtu huyu utasababisha fursa za kifedha kuingia kwako. Hii inaweza kuwa inakuja kupitia mazingira ya kazi au mahusiano. Unaweza ukajikuta unaishia katika uhusiano wa kimapenzi au wa kingono na wao au wanaweza kushik**ana juu ya kitu ambacho nyote wawili mnakipenda k**a vile shughuli za ubunifu, mambo ambayo mnayoyapendelea yenye ushabiki wenu. Huyu ni mtu mpya, mtu ambaye unakaribia kukutana naye au umewahi kumsikia lakini hujawahi kukutana naye. Huyu ni mtu ambaye utashirikiana naye vyema kiwema kabisa.
MAPACHA (C, O) 21/5 - 21/6
Mtu fulani unayeshughulika naye amekukatisha tamaa na anakufanya uhisi k**a wewe ndiye huna akili. Huenda ukahitaji kubadilisha mbinu zako na kuanza kuangalia upya chaguzi nyingine au fursa mpya kwa sababu inaonekana kuwa hawatokuja kubadilika, na inaonekana wamejipanga kutobadilika kwa sababu wanataka kupigania kile wanachofiiri kuwa ni sawa kwao. Hawaoni walichokosea. Huwezi kumfanya mtu aelewe hoja yako. Unahitaji kujiuliza ikiwa bado itafanikiwa na kuleta maelewano kati yenu au la!
KAA (D, P) 22/6 - 22/7
Kitu kizuri kinakuja kwako njia ya maandishi kwa ajili yako kabla ya mwezi huu kuisha iwe ujumbe wa kawaida kwenye simu (SMS), WhatsApp, barua pepe, n.k. Haya ni mawasiliano yanayohusu pesa lakini kwa wengine hii ni kutokana na mapenzi ambayo inaonekana hujazungumza nao kwa muda mrefu. Baadhi yenu mna watu wawili tofauti wanaotuma ujumbe kwa wakati mmoja.
SIMBA (E, Q) 23/7 - 22/8
Kitu ambacho umekuwa ukikingoja na kukipangilia hatimaye kiko karibu kufika, na kinakuja muda wowote kuanzia sasa. Chochote hicho kinachokuja kina uwezo wa kukufanya uwe na furaha. Kinaonyesha ni jinsi gani umekuwa ukikiombea, hivyo endelea kuwa na nia thabiti na hakika kinafanikiwa. Inahisi k**a hili linaweza kuwa jambo la kwanza zuri ambalo halikukutokea kwa muda, na linaweza hata kuhisi k**a ni mwanzo wa siku bora zaidi, na ndivyo itakavyokuwa.
MASHUKE (F, R) 23/8 - 22/9
Umekuwa ukiomba hivi majuzi miujiza itokee hali ibadilike Mambo yawe mazuri zaidi sasa mambo yanakuwa mazuri na wala hupokei bahati hizo zote kwa bahati nzuri tu bali unapokea mambo mazuri kwa sababu unastahili. Bidii yako inakulipa sasa.
MIZANI (G, S) 23/9 - 22/10
Usitumie muda mwingi kuwa na wasiwasi juu ya nini kitatokea endapo utashindwa. Unalindwa juu ya chochote kile kitakachotokea. Kadri unavyoshughulikia vitu pole pole, ndivyo utakavyofanikiwa zaidi. Usipende kukurupuka au kuharikisha vitu.
NG'E (H, T) 23/10 - 22/11
Unakuja katika uwezekano usio na mwisho yaani kila kitu kwako kitakuwa kinawezekana! Roho inakufungulia milango mingi sasa hivi. Utaanza kuona miujiza katika maisha yako na pande zote zinazokuzunguka. Njia hizi zinafunguliwa mahususi kwako kwa wakati huu. Utakuwa katika mshtuko kwa kushangazwa na baadhi ya mambo jinsi yatakavyokuwa yakitokea ila ni kiuzuri tu sio kiubaya usije ukaogopa.
MSHALE (I, U) 23/11 - 21/12
Unawavutia watu wa kabila la roho yako (soul tribe) yaani watu unaoendana nao kwenye kila kitu hususani kwenye malengo yako. Ninakuona ukifanya kazi na wengine na kuna uwezekano mkubwa wa kushirikiana nao katika siku za usoni. Wengi wenu mtakuja kwenye miunganisho yaani kuungana na watu mnaofanya kazi katika lengo moja.
WhatsApp, Call
https://chat.whatsapp.com/C0GZ4Dtgow0Ges8ZEBM64n