Annahnutritionpoint

Annahnutritionpoint Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Annahnutritionpoint, Medical and health, Njombe.

19/03/2026

Mambo ya kuzingatia unapoachagua diaper Bora Kwa ajili ya mtoto

1. Uwezo wa Kunyonya (Absorbency)
Diaper nzuri inapaswa kunyonya mkojo haraka na kuzuia unyevu kubaki kwenye ngozi ya mtoto. Hii husaidia kuepuka:
Vipele (diaper rash)
Harufu mbaya
Usumbufu kwa mtoto

2. Ulinzi Dhidi ya Kuvuja (Leak Protection)
Angalia diaper yenye:
Elastic nzuri pembeni
Kinga ya kuzuia kuvuja usiku kucha
Hii ni muhimu hasa kwa watoto wanaolala muda mrefu.

3. Urahisi wa Ngozi (Skin-Friendly)
Ngozi ya mtoto ni nyeti sana, hivyo chagua diaper:
Laini (soft)
Isiyo na kemikali kali
Inayoruhusu hewa kupita (breathable)

4. Ukubwa Sahihi (Right Size)
Ukubwa usio sahihi unaweza kusababisha:
Kuvuja (ikiwa kubwa sana)
Kubana na kusababisha alama au maumivu (ikiwa ndogo)
πŸ‘‰ Fuata uzito wa mtoto uliowekwa kwenye kifurushi cha diaper.

5. Faraja na Urahisi wa Kutumia
Diaper inapaswa:
Kuvalika na kuvuliwa kwa urahisi
Kumruhusu mtoto kucheza, kutambaa na kusogea bila usumbufu

6. Uwezo wa Kukaa Muda Mrefu (Long-lasting)
Diaper bora inaweza kukaa kwa masaa kadhaa bila kuhitaji kubadilishwa mara kwa mara, hasa usiku.

7. Bei na Ubora
Usichague kwa bei pekee. Mara nyingi:
Diaper za bei nafuu sana zinaweza kusababisha rashes
Bora kuchagua yenye ubora mzuri hata k**a ni ghali kidogo

Diaper bora ni ile inayomuweka mtoto wako:
βœ” Mkavu
βœ” Mwenye furaha
βœ” Bila vipele

predo baby diapers Ina sifa hizo zote
Chagua predo diapers Leo

Piga +255 769 807 303
Zanzibar na Dar es salaam
Kuwa wakala au kununua
Karibu
# babycare

16/03/2026

Mahitaji muhimu
1. Vitu vya Mama
Nguo za kujifungulia / nightgown rahisi kufungua mbele
Nguo za kubadilisha baada ya kujifungua (nguo laini na huru)
Chupi kubwa za pamba kadhaa
Pads za uzazi (maternity pads)
Soksi na slippers
Taulo
Bra ya kunyonyesha
Toothbrush na toothpaste
Sabuni, lotion, deodorant
Chupa ya maji na vitafunwa vyepesi
Simu na charger

2. Vitu vya Mtoto
Diapers za newborn
Baby wipes
Nguo za mtoto (body suits/rompers) 3–4
Swaddle / blanketi la mtoto
Kofia ya mtoto
Soksi za mtoto
Taulo ndogo ya mtoto
Mafuta au lotion ya mtoto

3. Nyaraka Muhimu
Clinic card / antenatal card
Kitambulisho (ID)
Bima ya afya k**a ipo

4. Vitu vya Ziada Vinavyosaidia
Sanitizer
Hair ties / head scarf
Plastic bag kwa nguo chafu
Pesa kidogo kwa mahitaji ya haraka

Usisahau kupack diapers za newborn

Nzuri Kwa ngozi nyeti ya mtoto mchanga
Zinanyonya unyevu wote kumuacha mtoto mkavu
Ulinzi Salama Kwa mtoto

Size zote zinapatikana
Kwa pack tofauti kutokana na mahitaji yako

Diaper kutoka predobaby ni chaguo Salama Kwa mama na mtoto
Mtoto mkavu=mama mwenye amani

Nimesahau nini hapo share na first time mom aione

13/03/2026

Usafi wa mtoto hauishii kwenye vyombo pekee.
Watoto hugundua dunia kwa kugusa na kuweka vitu mdomoni, hivyo ni muhimu kuhakikisha mazingira yote yanayomzunguka mtoto ni safi na salama.

Mtoto mwenye afya huanza na usafi wa vyombo, mazingira, na uangalizi wa mzazi. ✨

13/03/2026

Nina furaha kutangaza kuwa sasa mimi ni Ambassador wa Predo Baby 🀍

Bidhaa zetu:
β€’ Baby Diapers
β€’ Baby Pants
β€’ Adult Diapers
β€’ Baby Wipes
β€’ Hand Wash (harufu 7 tofauti)

Zinapatikana size zote.
Bei nafuu za kitanzania

A full package for baby care. πŸ‘Ά

πŸ“ž Call / WhatsApp: 0769807303
Follow

Mtoto mkavu = Mama mwenye amani.

Predo baby chaguo lako la wakati wotee

Watoto hawana sauti β€” mimi ni sauti yao.
Children ambassador🌈

12/03/2026

Anza clinic mapema ,tumia supplement zote utazopewa
Jifunze kupitia story ya ashura

Dislaimer:- this content is for educational purpose only

11/03/2026

Siku 1000 za mtoto ni kipindi muhimu sana katika maisha ya mtoto kinachoanza tangu mimba inapotungwa hadi mtoto anapofikisha miaka 2 (miezi 24). Kipindi hiki kinahusisha ujauzito wote pamoja na miaka miwili ya kwanza ya maisha ya mtoto.

Maana ya Siku 1000
Siku ~270: kipindi cha ujauzito (mimba)
Siku 365: mwaka wa kwanza wa mtoto
Siku 365: mwaka wa pili wa mtoto
Jumla yake ni takribani siku 1000.

Kwa nini siku 1000 ni muhimu?
Katika kipindi hiki:
Ubongo wa mtoto hukua kwa kasi sana.
Mwili wa mtoto huunda msingi wa afya yake ya baadaye.

Lishe bora na malezi mazuri hupunguza udumavu na magonjwa.

Mambo muhimu kuzingatia katika siku 1000

Lishe bora kwa mama kabla na wakati wa ujauzito
Kuhudhuria clinic mapema na mara kwa mara
Kujifungua salama hospitali
Kunyonyesha maziwa ya mama pekee miezi 6
Kuanza chakula cha ziada kuanzia miezi 6
Chanjo zote za mtoto
Upendo, mawasiliano na kucheza na mtoto
Faida za kuzingatia siku 1000
Mtoto hukua akili na mwili vizuri
Kupunguza udumavu (stunting)
Kupunguza vifo vya watoto
Mtoto kuwa na uwezo mzuri wa kujifunza baadaye.

10/03/2026

1. Maumivu ya tezi za matiti (Sore ni***es)
Sababu: Mtoto hayakanyonyi vizuri au latch si sahihi.
Suluhisho: Badilisha position ya kunyonyesha, tumia cream ya lanolin ikiwa inahitajika.

2. Maziwa kidogo au flow duni
Sababu: Kunyonyeshwa kidogo, stress, dehydration, au latch si sahihi.
Suluhisho: Nyonyesha mara kwa mara, kunywa maji ya kutosha, pata msaada wa lactation consultant.

3. Mastitis (uvimbe na maumivu ya tezi)
Sababu: Infeksheni ya bakteria kwenye tezi; huambatana na uvimbe, joto mwilini, na maumivu.
Suluhisho: Endelea kunyonyesha, tumia compress ya moto, na tafuta dawa k**a daktari atapendekeza.

4. Engorgement (matiti kujazwa sana na maziwa)
Sababu: Mtoto hakuonyonywa mara kwa mara.
Suluhisho: Nyonyesha mara nyingi, tumia compress ya joto au baridi kwa urahisi, k**a inahitajika kamulia maziwa kidogo.

5. Plugged ducts (miundo ya maziwa imeziba)
Sababu: Mtindo wa kunyonyesha au position isiyo sahihi.
Suluhisho: Massage tezi, nyonyesha mara kwa mara, tumia compress ya moto.

6. Choke au cough ya mtoto wakati wa kunyonyesha
Sababu: Mtoto anakunywa haraka au position si sahihi.
Suluhisho: Badilisha position, weka mtoto chini kidogo na utulize.

7. Thrush (fungal infection)
Sababu: Yeast inakua kwenye tezi au mdomo wa mtoto.
Suluhisho: Tiba na dawa inayofaa (daktari au pharmacist).

8. Ni**le confusion (mtoto anapendelea bottle)
Sababu: Kunyonyeshwa kidogo na kutumia bottle mara nyingi.
Suluhisho: Badilisha kati ya breast na bottle kwa ustadi, tumia paced bottle feeding.

9. Overactive letdown (mtiririko wa maziwa sana)
Sababu: Maziwa yanatoka kwa nguvu sana, mtoto anakata kuchukua.
Suluhisho: Badilisha position (situa mtoto juu kidogo), nyonyesha mara nyingi.

10. Fatigue & stress
Sababu: Kunyonyesha mara nyingi, usingizi mdogo.
Suluhisho: Pumzika kadri uwezavyo, pata msaada wa familia, nyongeza chakula bora na maji.

Usimuachishe mtoto kutokana na changamoto hizi tafuta msaada

10/03/2026

Ingredients
Avocado lililoiva
1 Tomato
1 Cucumber
Majani ya Lettuce
1 Carrot (hiari)
Kijiko 1 cha Olive oil
Juisi kidogo ya Lemon
Chumvi kidogo

πŸ₯— Namna ya Kuandaa
Kata Avocado vipande vidogo.
Kata Tomato na Cucumber.
Changanya na majani ya Lettuce.
Ongeza Carrot iliyokunwa.
Mimina Olive oil na juisi ya Lemon.
Changanya vizuri kisha kula.

βœ… Tip: Saladi hii ni nzuri kwa wajawazito, mama wanaonyonyesha na familia nzima kwa sababu ina virutubisho muhimu.

10/03/2026

Haki ya kuishi
Haki ya kupata jina na utaifa
Haki ya kupata elimu
Haki ya kupata huduma za afya
Haki ya kupata lishe bora
Haki ya kulindwa dhidi ya ukatili na unyanyasaji
Haki ya kuishi na kulelewa na wazazi au walezi
Haki ya kusikilizwa na kutoa maoni
Haki ya kucheza na kupumzika
Haki ya kutobaguliwa
Haki ya kulindwa dhidi ya ajira za watoto
Haki ya kulindwa wakati wa majanga au vita


rights

Child ambassador
Watoto Hawana sauti Mimi ni sauti yao

Address

Njombe

Opening Hours

Monday 08:00 - 20:00
Tuesday 08:00 - 20:00
Wednesday 08:00 - 20:00
Thursday 08:00 - 20:00
Friday 08:00 - 20:00
Saturday 08:00 - 20:00

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Annahnutritionpoint posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram