TFNC Tanzania

TFNC Tanzania Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from TFNC Tanzania, Nutritionist, Ilala.

Happy Karume Day
07/04/2026

Happy Karume Day

Tunawatakia Pasaka Njema
05/04/2026

Tunawatakia Pasaka Njema

TUNAKUTAKIA IJUMAA KUU NJEMA
03/04/2026

TUNAKUTAKIA IJUMAA KUU NJEMA

Leo Machi 27 2026, Wafanyakazi wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) wameshiriki katika kutoa maoni na mapendek...
27/03/2026

Leo Machi 27 2026, Wafanyakazi wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) wameshiriki katika kutoa maoni na mapendekezo kuhusu Kanuni za chakula zinazoandaliwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) k**a sehemu ya wadau muhimu katika eneo hilo.

Maoni na mapendekezo hayo yamehusisha kanuni za uuzaji na uhamasishaji wa chakula na bidhaa zilizoanishwa kwa ajili ya Watoto wachanga na wadogo za Mwaka (2026) Pamoja na kanuni ya Matangazo ya chakula na vipodozi kwa Mwaka (2026).

Akizungumza wakati wa kuendesha zoezi hilo la utoaji maoni hayo, Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi ya Chakula na Lishe Dkt. Analice Kamala, amesema maoni hayo yatawasilishwa k**a maoni ya Taasisi na yataenda kusaidia kuboresha rasimu ya kanuni husika kwa kuongeza vipengele muhimu ambavyo awali vilikuwa vinakosekana kwenye kanuni ya zamani.

VACANCY ANNOUNCEMENT
23/03/2026

VACANCY ANNOUNCEMENT

22/03/2026
TFNC, NBS, MUHAS NA IHI YATAMBULISHA B MRADI WA KUIMARISHA MFUMO WA UFUATILIAJI VIASHIRIA VA LISHE TANZANIA (MNBi-URT)Na...
18/03/2026

TFNC, NBS, MUHAS NA IHI YATAMBULISHA B MRADI WA KUIMARISHA MFUMO WA UFUATILIAJI VIASHIRIA VA LISHE TANZANIA (MNBi-URT)

Na, Mwandishi Wetu

Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) na Taasisi ya Utafiti Ifakara (IHI) kupitia ufadhili wa Gates Foundation, imebuni mradi wa Kuimarisha Mfumo wa Ufuatiliaji wa Viashiria vya Lishe Nchini kwa kutumia mabaki ya sampuli za tafiti na hospital katika kupima na kukadiria viwango vya aina ya upungufu wa vtamini na madini kwa wanawake waliom katika umri wa kuzaa.

Mradi huo utasaidia kukabiliana na changamoto za Uhaba wa takwimu za lishe hususani zinazohusu upungufu wa Vitamini na Madini nchini. Aidha mradi huu unatarajia kutoa taarifa za lishe kwa wakati, kwa gharama nafuu na kwa uendelevu kupitia mifumo mingine ya kisekta ya Afya na TAMISEMI ambayo tayari imesimikwa.

Akizungumza wakati wa kutambulisha mradi huo kwa Kamati ya kitaifa ya watalaam ya usimamizi na ushauri wa masuala ya lishe, iliyokutana tarehe 16 Machi 2026 katika Ofisi za Waziri Mkuu jijini Dodoma, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) Dkt. Germana Leyna, amesema mradi huo pia unatarajia kuimarisha uwezo wa maabara ya Taasisi ya Chakula na Lishe, kuchakata mabaki ya sampuli bila kupeleka nje ya nchi, sambamba na hilo mradi huu utagharamia upatikanaji wa ithibati za kikanda na kimataifa katika uchakataji wa sampuli za chakula na kibailojia.

“Kukamilika kwa mradi huu kutawezesha sekta, mikoa, halmashauri na taifa kwa ujumla kupanga mikakati na afua za lishe kwa kutumia takwimu na taarifa zinazozalishwa na mifumo ya nchi bila kutegemea ufadhili kutoka nje.” Alisema Dkt. Germana.

.tanzania .sbu

TUNACHANGIA Baadhi ya Wajumbe k**ati ya taifa ya Wataalam ya Usimamizi na Ushauri wa Masuala ya Lishe  wakichangia  na k...
16/03/2026

TUNACHANGIA

Baadhi ya Wajumbe k**ati ya taifa ya Wataalam ya Usimamizi na Ushauri wa Masuala ya Lishe wakichangia na kutoa maoni baada ya kuwasilishwa kwa taarifa za utekelezaji wa shughuli mbalimbali za lishe nchini.

Kamati hiyo imekutana leo tarehe 16 Machi 2026 katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Jijini Dodoma, kujadili na kufanya tathmini ya utekelezaji wa shughuli za lishe nchini ikiwemo Mpango Jumuishi wa kitaifa wa masuala ya lishe pamoja na mikakati mingine ya kuboresha hali ya lishe nchini.

TUNAFUATILIA KWA MAKINIWajumbe k**ati ya taifa ya Wataalam ya Usimamizi na Ushauri wa Masuala ya Lishe  wakifuatilia kwa...
16/03/2026

TUNAFUATILIA KWA MAKINI

Wajumbe k**ati ya taifa ya Wataalam ya Usimamizi na Ushauri wa Masuala ya Lishe wakifuatilia kwa makini mawasilisho mbalimbali yanayohusiana na utekelezaji wa shughuli mbalimbali za lishe nchini, mara baada ya k**ati hiyo kukuta leo tarehe 16 Machi 2026 katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Jijini Dodoma, kujadili na kufanya tathmini ya utekelezaji wa shughuli za lishe nchini ikiwemo Mpango Jumuishi wa kitaifa wa masuala ya lishe pamoja na mikakati mingine ya kuboresha hali ya lishe nchini.

NAWASILISHAMkurugenzi wa Sera na Mipango ya Lishe wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Bi. Debora Charwe, akiwasilish...
16/03/2026

NAWASILISHA

Mkurugenzi wa Sera na Mipango ya Lishe wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Bi. Debora Charwe, akiwasilisha wasilisho la kuelekea mkutano mkuu wa Mwaka wa Wadau Lishe nchini kwa k**ati ya taifa ya Wataalam ya Usimamizi na Ushauri wa Masuala ya Lishe ambayo imekutana leo tarehe 16 Machi 2026 katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Jijini Dodoma, kujadili na kufanya tathmini ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za lishe nchini ikiwemo Mpango Jumuishi wa kitaifa wa masuala ya lishe pamoja na mikakati mingine ya kuboresha hali ya lishe nchini.

Address

Ilala

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 17:00

Telephone

0658990996

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when TFNC Tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram

Category