Afya ya akili

Afya ya akili Naandika Kuhusu afya ya akili ya mwana damu na changamoto anazopitia pia makala zote zinaelekeza kub

Hadithi UKINIPA SISEMISehemu ya kwanza                                                                                  ...
19/01/2023

Hadithi UKINIPA SISEMI
Sehemu ya kwanza "Hapana Klinika mimi Siwezi kufanya Hivyo hata siku Moja naomba Basi Muogope Mungu. Utafanyaje Vitu k**a hivyo wakati Unajua kabsa malengo yangu ni yapi ambayo nataka kuyafikia. Kwanza kitu k**a hiki hukupaswa kuniambia kabsa maana siyo mahara pake na nilishaapa sitaweza kufanya kitu k**a hiki hata siku moja maana ni kinyume na maadili ambayo nasomea" Nilimwambia Klinika huku nikiwa natetemeka maana kitu ambacho alikuwa anakitaka kutoka kwangu ilikuwa hakiwezekani kabsa. Kwanza Mimi Mwenyewe sikuwa tayari Kufanya kitu k**a kile hata siku Moja pili kitu ambacho klinika alikuwa anahitaji Tufanye ilikuwa kinyume na Maadili ya shule ambayo nilikuwa Nasomea.

Upande Mwingine kwa kweli Nilikuwa nashangaa Sana kwa Mwanamke Mzuri k**a Klinika Kusomea Usister maana asilimia kubwa ya Wanafunzi wa Seminari Hususani wanaosomea Usister huwa na Sura ambazo Siyo za Kuvutia Sana. Upande wa Klinika kwa kweli yeye alikuwa na Sura ya Kuvutia Sana ambayo Ukimwangalia kwa Makini na ukiwa mwanaume Kamili lazima Moyo utatamani kuongea neno Juu yake. Akiwa Kidato cha Kwanza Seminari ya deshi aliweza Kusababisha Mapadri wawili kutolewa cheo cha Upadri kutokana na kushindwa Kuvumilia hatimaye kutembea nae.

Siyo Mapadri tu pia hata Waseminari (Wanafunzi wakiume wanaosomea Upadri) Wengine walikuwa Wanafukuzwa hususana shule ambayo nilikuwa nasomea mimi. Shule nyingi za Seminari huwa zinatenganishwa yani Wanaume Tofauti na Wanawake tofauti ila Shule ambayo nilikuwa ninasomea Mimi ilikuwa Shule Moja kubwa ambayo sawa ilikuwa Imegawanywa mara mbili Wanawake tofauti na Wanaume tofauti lakini ilikuwa Ndani ya Uzio mmoja. Hivyo Kwa Uzuri ambao alikuwa nao Klinika kwa kweli Waseminari wengi walijikuta wanasahau kile ambacho kilikuwa kinawaleta pale Shuleni na kukuta wanavunja amri ya sita ya Mungu na hatimae Wakik**atwa wanafukuzwa.

Upande wa Klinika yeye alikuwa hafukuzwi hata Ikitokea kuwa mkak**atwa Mnafanya Ugoni basi aliyekuwa anafukuzwa alikuwa ni Mwanaume. Hii ilitokana na baba yake alikuwa tajiri sana pia alikuwa Mchungaji. Uzuri wa Klinika kwa kweli Hata mimi Ulikuwa unanitesa Sana na Kutamani Kuvunja amri ya sita ila kila nilipokuwa Nakumbuka Mazingira ambako nimetokea Nilikuwa naapa sitaweza kufanya kitu Kigumu k**a Hicho.

Ugumu wa Maisha ya Nyumbani ambayo ulipelekea hadi Kubadilisha Dini kutoka Uislamu hadi Kuwa Mkristo aliyekolea hatimae Kuchukuliwa na Wazungu na kwenda kuanza kusomea Upadri ndio ulinifanya kupinga kile kitu ambacho klinika alikuwa anakitaka kutoka kwangu. Laiti k**a Mama yangu angelikuwa na kazi yeyote hususani hata angekuwa Mwalimu basi kwa Uzuri ambao alikuwa nao Klinika kamwe nisingeweza kuendelea Kuvumilia. "Hapana naomba Usiseme hivyo Sam Unaweza kunifanya nikawa kichaa, kwa kweli tangia nizaliwe sijawahi kumpenda Mwanaume k**a ninavyokupenda wewe.
Sawa Najua k**a Hapa Tulipo hiki kitu ni kinyume kabsa na Hairusiwi kufanya lakini naomba Nipe hata Mara moja. Najua itakuwa Vigumu kwako kufanya kitu k**a hiki maana Utakuwa Umevunja sheria nyingi sana, moja utakuwa Umevunja Sheria ya Mungu na Dini pia utakuwa umevunja sheria za kipadri ila tafadhari naomba nipe kidogo. Naapa Sam UKINIPA SISEMI kweli kabsa siwezi kumwambia Mtu yeyote zaidi hii siri itabaki kuwa yako na yangu. Nakupenda Sana Sam kila Muda nakufikilia wewe na Maisha yangu yatakuwa Magumu bila Kunipa hicho kitu "Aliongea Klinika huku akiwa serous kabsa.

Yani Maneno ambayo alikuwa anaongea Klinika yalikuwa yakijinga lakini kwa Upande wake yalikuwa yanakaribia hadi kumtoa Machozi. Yale Maneno ya Kliniki kwa kweli yalinifanya hadi nilianza kutokwa na Machozi maana katika Maneno ya kipumbavu ambayo nilihisi Klinika aliwahi kuongea yalikuwa yale.
****†††††*****

"Mwanangu hakuna jinsi na hali ya Mama yako nazani Unaijua, Wakati baba yako anakufa alinipa kazi tatu tu. Kazi ya Kwanza aliniambia kuwa nikulee katika maadili mema ya misingi ya Dini ya Kiislamu, kazi ya pili aliniambia nihakikishe nakupatia elimu bora ya Duniani na elimu ya Akhellah na kazi ya Mwisho alinipa nihakikishe nakufunza kuishi maisha vizuri na watu.

Mwanangu kazi ya kwanza na yapili nahisi naelekea kushindwa. Mwanangu nazani unajua unaenda kumaliza Mwaka haujaenda shuleni kutokana na Hali Ngumu ya Maisha. Moyo wangu unaniuma Sana maana kile ambacho alikiongea baba yako kabla ya kufa leo tunaenda kukivunja. Leo hii nakubadilisha Jina lako kutoka Ibrahimu na utakuwa Unaitwa Samweli ili Mwanangu usome. Kuna Wezangu Wamekuja na Wamevutiwa na akili yako uliyo nayo hivyo wanakuchukua na kukupeleka kwenye shule yao ya Seminari kwa ajili ya Kukusomesha na baadae utakuwa padri.

Najua hata wewe hupendi kubadilisha Dini kutoka Dini ya baba yako na mama yako na kwenda dini ya Kikristo lakini hakuna jinsi. Mwanangu unachotakiwa kuelewa Dini zote ni Dini za Mungu na hakuna Dini nzuri na Dini mbaya hivyo Nakuomba ukubali Ombi langu na Kesho utakuja kuchukuliwa na kupelekwa kwenye hiyo Shule kwa ajili ya kuanza Masomo yako.

Naombe Ukienda kule kazana Kusoma Mwanangu ili Uje kunisaidia Maisha yangu Mwanangu. Hivyo nimeamua kwenda kinyume na matakwa mawili ya baba yako ili Mwanangu usome na kuwa na Maisha Mazuri sitaki Mwanangu Uje uishi maisha k**a ambayo Tunaishi sasa hivi. Maisha ambayo yalipelekea hata baba yako kufa kinyama"Nilikumbuka Maneno ambayo alikuwa anaongea Mama yangu kabla ya kuondoka kuja shuleni kwa kweli sikutaka hata kumuona Klinika.

Nilichofanya nilianza kuondoka pale huku moyo Ukiwa unaniuma na Machozi yakiwa yananitoka. Kuondoka pale siyo kwamba nilikuwa simpendi klinika ila Moyo wangu Ulikuwa unaniuma maama k**a ningesubutu kufanya hovyo nisingekuwa na Sifa ya kusomea Upadri tena. Ingawa Nyuma dini yangu nilikuwa muislamu ila kwa Muda Ule nilikuwa tayari Mroma Mzuri sana na ambaye alikuwa anaijua dini vilivyo. Tayari kwenye Maisha yangu mapenzi nilikuwa nimeshaweka X###x. Yani ingawa Nilikuwa na hisia kali tu za kimapenzi lakini nilisha weka sitakuja kulala na Mwanamke hadi nakufa K**a Sheria za Dini ambazo zilikuwa zinataka.

Wakati nikiwa naondoka pale cha ajabu na kilichozidi kunichanganya Klinika alinifuata na kunishika mkono. Kitendo cha Klinika kunishika Mkono wake ilifanya Mwili wangu kusisimka mbaya. Klinika mungu alimjalia kuwa na mikono laini ambayo ilikuwa na Ubaridi flani hivi. Hata aliponishika Raha ya ajabu ilianza kunijia. "Sam Narudia tena Tafadhari naomba Usinifanyie hivyo Naapa kwa jina la Mungu wangu UKINIPA SISEMI wala hakuna mtu yeyote atakayejua. pia Sam Hii sura yako kwa kweli hupendezi hata kuwa padri maana utawatesa wanawake wengi sana. Hivi kwa nini umeamua kujifunga Hivi Sam"Aliongea Klinika huku akizidi kunivuta ili nimsogelee.

Lile swali la Klinika kwa kweli lilinish*tua sana maana Nakumbuka siyo yeye tu ambaye alishawahi kuniambia kitu k**a Hicho. Nakumbuka Siku Moja nilikuwa nimetoka Uwanjani Kufanya Mazoezi hata Sister Magreth aliwahi kuniita na Kuniambia Maneno k**a hayo. Hivyo Kusikia kwa maneno tena hayo kwa Mwanamke mzuri k**a Klinika kwa kweli ilibidi nish*tuke maana mimi nilikuwa Nasikia tu naambiwa Mzuri lakini uzuri wenyewe nilikuwa siuoni. Sasa Kwa Mwanamke Mzuri na Mrembo k**a Klinika kuniambia hivyo kweli nilianza kuamini k**a Mimi nilikuwa ni Mwanaume Mzuri.

"Klinika Kwa Lugha nzuri yakipole k**a mang'ati anakamua Mziwa naomba niachie Mkono niondoke. Hicho kitu ambacho unakiomba kwa kweli hakiwezi kutokea hata Siku moja. Hivi Unajua mimi hadi kuwa hapa nimepitia mangapi. Klinika unataka na Mimi nifukuzwe Shuleni k**a Frank, Mandewa ulivyosababisha wakafukuzwa. Naomba haja zako za umalaya zisinifanye mimi nikakosa kile ambacho nataka. Klinika lengo langu mimi ni Kusoma na kuwa Padri mzuri na Sijaja hapa kusomea ngono mbona Umeng'ang'ania hivi UKINIPA SISEMI hiyo ndio njia unatumiaga kuwarubuni wanaume ili wakupe alafu wafukuzwe shule?" Nilimwambia Klinika na kuanza kuondoka maana niliona nikiendelea kukaa pale moyo ni nyama unaweza kunishawishi nikaingia pabaya.
ITAENDELEA.......

LIKE NA SHARE TUENDE SAWA HII IPO MNAKULA UTAMU HADI MWISHO

07/01/2023

Kheri ya Mwaka mpya kwenu Nyote

17/10/2022

Anxiety /wasiwasi
Je unajua kuwa na wasiwasi kupita kiasi ni ugonjwa na una madhara kwa Afya ya akili .
Usisahau kutembelea kurasa wetu kwa ajili ya kupata dondoo zitakazo kusaidia kuimarisha afya yako ya akili na k**a una changamoto karibu

17/10/2022

"Ukileta mwenzako na mwenzako akawaleta wenzake, baada ya week unakuwa millionea, kila mwaka utasafiri kwenda espain na dubai, gharama zote unalipiwa na kampuni"😃😃😃

Hivi sio vitu vya kucheka jamani tuwasaidien watu wanatapeliwa sana kupitia hii michezo.🤷🏽‍♂️

"Good Morning Millionea"

Jinsi ya kununua unatuma pesa 10,000/= kwenda namba 0784095085 jina ni Ezekiely halafu unatuma ujumbe ukisema kitabu na ...
22/10/2020

Jinsi ya kununua unatuma pesa 10,000/= kwenda namba 0784095085 jina ni Ezekiely halafu unatuma ujumbe ukisema kitabu na njia unayotaka kutumia baada ya hapo utapata kitabu ndani ya dakika tano na utakua huru kupiga simu kwa namba zilizo mwisho wa kitabu kwa msaada zaidi

Hiki ni kitabu kinachohusiana na namna bora ya kuondoa stress na sonona kwa watu wa rika zoteJinsi ya kununua unatuma pe...
22/10/2020

Hiki ni kitabu kinachohusiana na namna bora ya kuondoa stress na sonona kwa watu wa rika zote
Jinsi ya kununua unatuma pesa 10,000/= kwenda namba 0784095085 jina ni Ezekiely halafu unatuma ujumbe ukisema kitabu na njia unayotaka kutumia baada ya hapo utapata kitabu ndani ya dakika tano na utakua huru kupiga simu kwa namba zilizo mwisho wa kitabu

Wanawake wengi wanaojifungua wamekua wahanga wa msongo wa mawazo na sonona baada ya kujifunguaHali hii imekua ikiongezek...
22/10/2020

Wanawake wengi wanaojifungua wamekua wahanga wa msongo wa mawazo na sonona baada ya kujifungua

Hali hii imekua ikiongezeka siku baada ya siku na takwimu zinaonyesha kati ya wanawake 7 mmoja hupata haya magonjwa baada ya kujifungua

Baada ya kuona katika jamii hali hii inaongezeka nimeamua kuandika kitabu kinachoelezea jinsi ya kukabiliana na hii changamoto baada ya kujifungua katika sehemu ya tatu na ya nne ya kitabu hichi utapata mwanga wa nini ufanye, endapo hutaelewa kwa wateja wote walionunua kitabu wataweza kuwasiliana na madaktari wa akili moja kwa moja ili kupata ufumbuzi wa matatizo yanayowapata.

Kitabu kinauza kwa punguzo na bei ni 10,000/- baada ya wateja 50 wa mwanzo bei itakua 15000 na utatuma kwa 0784095085 halafu utatuma message yenye jina na njia utakayo hitaji kutumiwa kitabu na utapata kitabu ndani ya dakika tano.

21/10/2020
Kushikilia vitu kunaleta uharibifu mkubwa kuliko kuacha vikaenda.
21/10/2020

Kushikilia vitu kunaleta uharibifu mkubwa kuliko kuacha vikaenda.

Unapokumbana na changamoto ambayo unaona huna wa mtu wa kumwambia ni muda sahihi wa kupata ushauri wa kitaalamu kuhusu t...
21/10/2020

Unapokumbana na changamoto ambayo unaona huna wa mtu wa kumwambia ni muda sahihi wa kupata ushauri wa kitaalamu kuhusu tiba maongezi ambayo itakuwezesha kupata suluhisho sahihi la changamoto unazopitia

Jambo muhimu zaidi kuimarisha utashi wako ni kujitolea kufanya hivyo!
18/10/2020

Jambo muhimu zaidi kuimarisha utashi wako ni kujitolea kufanya hivyo!

KWANINI MSONGO WA MAWAZO HUSABABISHA UZITO MKUBWA NA KITAMBIKuongezeka ovyo kwa uzito,kitambi na nyama uzembe ni tatizo ...
18/10/2020

KWANINI MSONGO WA MAWAZO HUSABABISHA UZITO MKUBWA NA KITAMBI

Kuongezeka ovyo kwa uzito,kitambi na nyama uzembe ni tatizo linalohusiana na ,msongo wa mawazo. Msongo wa mawazo unabadili jinsi mafuta yanavohifadhiwa ndani ya mwili kwa sababu ya kubadilika kwa vichocheona kemikali mbalimbali zinavyozalishwa na mwili pale ambapo unakuwa na stress. Kwa mfano tafiti zinasema kuwa stress kupitiliza husababisha uzalishaji wa protini inayoitwa betatrophin ambayo ni kizuizi kwa vimeng’enya ambvyo huvunjavunja mafuta yaliyohifadhiwa kwenye mwili.

Jambo gani la kufanya tumia namba zilizo katika bio upate ufumbuzi.

Address

Virtual Private Box 255756222185 Iringa
Iringa
51113

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Afya ya akili posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to Afya ya akili:

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram