21/10/2025
Semina ya Kiroho ni moja kati ya mambo muhimu katika Maadhimisho ya Wiki ya Kumbukizi ya Mt.Gaspar Del Bufalo
Kuanzia jana tarehe 20/10/2025 siku ya Ufunguzi wa Maadhimisho hadi leo, Fr.Henry Nilla C.P.P.S kutoka Nyumba ya Malezi Miuji Dodoma ameongoza semina ya kiroho kwa wafanyakazi wa Hospitali ya Rufaa na Mafunzo St.Gaspar-Itigi pamoja na wafanyakazi wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi St.Gaspar .
SIKU YA PILI YA HUDUMA ZA AFYA YA MAADHIMISHO YA WIKI YA MT.GASPAR,St. Gaspar Referral and Teaching Hospital
HUDUMA ZITAKAZOTOLEWA BURE WAKATI HUU WA MAADHIMISHO NI PAMOJA NA-
1. KUWAONA MADAKTARI NA MADAKTARI BINGWA (FREE CONSULTATION)
2. KUPATA VIPIMO VYA AFYA KWA MAGONJWA YA KISUKARI,SHINIKIZO
LA DAMU(PRESHA), MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI NA HALI YA LISHE (BMI)
3. KUFANYIWA UCHUNGUZI WA AFYA YA KINYWA NA MENO NA KUNG’OA JINO LILILOHARIBIKA
4. KUPATA HUDUMA YA MENO BANDIA
TAREHE 21/10/2025, HUDUMA NYINGINE ZITAKAZOTOLEWA KWA BEI NAFUU NI;-
• KUREKEBISHA MPANGILIO WA MENO
• HUDUMA BOBEZI YA KINYWA NA MENO KWA WATOTO
• HUDUMA YA UPASUAJI WA UVIMBE KATIKA USO,TAYA,KINYWA NA MENO
• KUREKEBISHA MIFUPA YENYE
MAJERAHA YALIYOSABABISHWA NA AJALI KATIKA USO
HUDUMA HIZI ZITATOLEWA KUANZIA TAREHE 20 HADI 22 OKTOBA 2025, SAA 3:00 ASUBUHI HADI SAA 10:30 JIONI, WAKATI HUDUMA ZA KINYWA NA MENO ZITAENDELEA MPAKA TAREHE 23 OKTOBA
KWA MAELEZO ZAIDI PIGA NAMBA +255 755 454 040
Pia unaweza kutembelea Mitandao yetu ya Kijamii-stgasparhospital
ya Wilaya ya ManyoniItigi DcWizara ya Afya TanzaniaWizara ya Afya TanzaniaOfisi ya Rais - TamisemiItigiTv ItigiTvWizara ya Elimu, Sayansi na TeknolojiaHumanitas University