22/01/2026
NJIA RAHISI ZA KUTUNZA NA KUIMARISHA AFYA YA MACHO
🥕 1. Matunda na Vyakula Bora kwa Afya ya Macho
Kula mara kwa mara vyakula hivi:
• Karoti – zina Vitamin A, husaidia kuona vizuri usiku
• Machungwa, ndimu, mapera – Vitamin C, hupunguza uchovu wa macho
• Parachichi – hulinda macho dhidi ya uharibifu
• Mboga za majani mabichi (spinachi, mchicha) – hulinda retina
• Samaki (dagaa, sato) – Omega-3, hupunguza ukavu wa macho
👉 Epuka sana sukari nyingi na mafuta mengi – huathiri afya ya macho.
💊 2. Dawa na Virutubisho (Supplements)
Tumia tu kwa ushauri wa mtaalamu:
• Vitamin A, C, E + Zinc – kwa kuimarisha macho
• Omega-3 capsules – kwa watu wenye macho makavu
• Matone ya macho (artificial tears) – kupunguza ukavu na muwasho
⚠️ Usitumie dawa bila kupima macho au bila ushauri wa daktari.
👓 3. Matumizi Sahihi ya Miwani
• Va miwani yenye kipimo sahihi baada ya kupima macho
• Tumia blue-cut lens k**a unatumia simu/kompyuta muda mrefu
• Va miwani ya jua (UV protection) ukiwa juani
• Safisha miwani kila siku kwa kitambaa maalum