07/01/2024
PRESHA YA KUSHUKA: SABABU, DALILI, ATHARI NA TIBA
MADHARA YA PRESHA YA KUSHUKA.
Presha ya kushuka ni kuwa na presha ya damu chini ya 90/60mmHg.
Presha ya chini huweza kuleta madhara na hata kifo, ila wakati mwengine huweza kutokea bila ya mtu kufahamu na bila madhara.
Presha ikiwa ndogo damu haifiki kwenye viungo muhimu k**a vile ubongo, figo na hata kwenye misuli ya moyo.
Kutokufika kwa damu katika sehemu hizi nyeti maaana yake ni kwamba hewa safi, chakula na virutubisho vingine havifiki kwenye viungo hivi.
Hivyo sehemu hizi huweza kudhurika kwa kukosa hewa au, kukosa nishati au kuzidiwa na uchafu.
Mtu anaweza kupata madhara kwenye figo, ubongo na hata moyo wenyewe. Pia presha ya kushuka inaweza kusababisha kuganda kwa damu kwenye mishipa mikubwa ya damu.
Hivyo ni muhimu kuhakikisha presha ya damu yako iko katika kiwango sawa kwa afya yako. Presha ya kawaida kwa watu wengi ni takriban 120/80 mmHg.
Watu wanaweza kuwa na presha iliyoshuka bila dalili yeyote.
Chukua tahadhari kwa mgonjwa ambaye amelala kwani presha inaweza kushuka bila yeye au unayemhudumia kutambua.
Namna pekee ya kufahamu kiwango cha presa na kuchukua hatua za tahadhari ni kupima tu.
SABABU ZA PRESHA KUSHUKA
Presha inaweza kushuka kwasababu mbalimbali.
1-Kusimama ghafla;
2-Kusimama kwa muda mrefu;
3-Magonjwa k**a vile kisukari, moyo kutanuka, magonjwa katika mishipa ya damu, magonjwa ya ini;
4-Hali ya hewa-joto kali sana au baridi kali sana;
5-Kupungua kwa maji mwilini kwasababu ya kuharisha au kutapika;
6-Kutokuwa na maji ya kutosha mwilini-kwasababu hunywi maji ya kutosha.
AINA ZA PRESHA YA KUSHUKA
Aina za presha za kushuka zimegawanyika katika makundi matatu kulingana na wakati inatokea au ukali na madhara yake
1-Presha ya kushuka kwasababu ya kusimama ghafla;
2-Presha ya kushuka sababu ya kusimama kwa muda mrefu;
3-Presha ya kushuka iliyo kali – hii husababishwa na maambukizi makali kwenye ugonjwa, kuvuja damu nyingi.
Ni zipi dalili za presha ya kushuka?
Mara nyingi hutoweza kuonesha dalili zozote wakati presha imeshuka.
Hatahivyo, presha inaposhuka na kuathiri upelekaji wa damu katika ubongo mtu anaweza kuwa na dalili zifuatazo:
Presha ikishuka utajisikia kizunguzungu, kichwa chepesi, unaweza kuanguka na kupoteza fahamu, kuhisi uchovu ambao wakati mwingine huathiri shughuli zako za kila siku.
Presha kushuka ghafla na kwa muda mfupi
1-Kusimama kwa haraka,
2-Kusimama muda mrefu,
3-Kutokwa na damu nyingi k**a vile wakati wa hedhi (kwa baadhi ya wanawake),
4-Kuvuja damu nyingi baada ya kuumia,
5-Mlo- mara nyingi ikitokea umekula kiasi kukubwa cha chakula na chenye wanga mwingi,
6-Mshtuko k**a vile kupokea habari ya kusikitisha
Presha ya damu kushuka kwa muda mrefu
Vinavyoweza kusababisha presha kuwa chini kwa muda mrefu au wakati wote:
1- Mtu mwenyewe kuwa na presha ndogo. Mwili wa watu k**a hawa huwa imeshazoea presha hii.
Lakini kabla ya kusema hii presha ni ya kawaida kwa mtu fulani, inabidi afanyiwe vipimo kuhakikisha hakuna kitu kinachosababisha presha kuwa chini.
2-Magonjwa ya moyo-misuli ya moyo kutanuka,
3-Ugonjwa wa Mishipa ya damu kutanuka
4-Kuwa na magonjwa ya homoni k**a vile kuwa na homoni ya thyroid kidogo kwenye damu.
5- Ugonjwa wa Kisukari – kwasababu kisukari huathiri mishipa ya fahamu yenye kazi ya kuratibu presha katika mishipa ya damu.
6- Athari ya dawa – kuna dawa ambazo hushusha presha. Dawa hizi ni mahususi kwa matibabu ya presha.
Wakati mwengine kuna watu ambao hupata mzio (allergy) wakitumia dawa fulani.
7-Mzio (allergy) husababisha presha kupungua. Mtu anapopata mzio moja ya mabadiliko yanayotokea kwenye mwili ni kutanuka kwa mishipa ya damu. Kutanuka kwa mishipa ya damu husababisha kupungua kwa presha.
Fahamu Presha Yako!
Fahamu kiwango cha presha yako ya damu na chukua hatua stahiki mapema unapotumia kipimo cha chenye teknolojia ya hali ya juu.
Presha ya kushuka ina tiba?
Ni mara chache ambapo mtu atahitaji tiba ya presha ya kushuka.
Ikiwa tiba itahitajika basi hutegemea kilichosababisha presha ishuke.
Lengo la tiba ni kupandisha presha kwa kiwango hitajika. Presha ya kawaida kwa binadamu wengi ni kuanzia 100-139/ 60-89 mmHg.
Huduma ya kwanza: K**a tulivyoona presha ya kushuka inaweza isiwe na shida kiafya. Lakini presha inaposhuka ghafla mtu huitaji huduma ya kwanza.
Ikatokea mtu ameanguka baada ya kuwa amesimama kwa muda mrefu, au anapokuwa anasimama basi:
1-alazwe chini na anyooke huku mkiendelea kutafuta sababu ya yeye kuanguka.
Ikibainika ni kwasababu presha ilishuka, kwa kulala kunaweza kurudisha presha yake kuwa sawa.
2-Mpatie ORS-Hichi ni kwanywaji ambacho ni mchanganyiko wa chumvi. Mtu hutumia kinywaji hiki k**a amepungukiwa maji mwilini kutokana na maradhi mbalimbali k**a vile yanayosababisha kuharisha na kutapika.
3-K**a hakuna ORS utampatia maji anywe. Unaweza kuchangaa kiwango kidogno cha chumvi na sukari (chukua tahadhari kwa mgonjwa wa kisukari). 1/4 ya kijiko cha chai kinatosha kwa lita moja ya maji.
4-Mlambishe chumvi-Chumvi itamshaidi kupandihsa presha na kuzuia maji yasitoke kwenye mishipa ya damu
MUHIMU
Kupima tu ndiyo njia PEKEE ya kufahamu presha ya mtu. Ni muhimu kuwa na kipimo cha presha ili kuokoa maisha hali k**a hiii ikitokea nyumbani.
Ninawezaje kuepuka presha ya damu kushuka?
Baada ya kuhakikisha kwamba umetibu magonjwa yanayosababisha presha yako ishuke chukua hatua hizi ili kujikinga na uwezekano wa presha kushuka.
1-Kunywa maji kiwango kinachotakiwa ukizingatia umri, afya yako, uzito, hali ya hewa na aina ya kazi zako.
Fahamu Kiwango cha maji ya kunywa kwa siku
2-Simama taratibu unapoamka kutoka kwenye kukaa
3-Usisimame muda mrefu, pumzika kwa kutembea tembea au kunja kunja misuli ya miguu, au tembea tembea
4-Fahamu shinikizo la damu kila unapotaka kunywa dawa. Ikiwa unaendelea na matibabu ya shinikizo la juu la damu – presha ni muhimu kupima shinikizo lako la damu kabla hujameza dawa
Asante.
Comment, Share and Like ili kupata taarifa ya Elimu ya Afya