23/10/2025
Homa ya Ini Ugonjwa Hatari Kuliko HIV (UKIMWI)
JE WAJUA? Mgonjwa wa homa ya ini akigundulika kuwa na maambukizi sugu, huanza kutumia dawa zile zile za kufubaza virusi vya HIV โYaani ARV.! ๐ฑ
Ndiyo Na maanisha vidonge vya ARV..
Wengi tunajua kuhusu UKIMWI, lakini je, umewahi kusikia kuwa Homa ya Ini (Hepatitis B) ni hatari zaidi ya HIV? ๐ณ
Hepatitis B ni mojawapo ya aina 5 kuu za virusi vya homa ya ini, lakini aina hii ni muuaji wa taratibu, huua ini lako kimya kimya bila hata kujua.
Leo nakupa elimu muhimu mno, ambayo inaweza kuokoa maisha yako au ya mpendwa wako.
Soma hadi mwisho, unaweza kuwa mkombozi wa familia yako..!
Tuanzie hapa, Hepatitis B ni Nini?
Ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vinavyoitwa Hepatitis B Virus (HBV).
Mara baada ya kuingia mwilini, virusi hivi hushambulia ini haraka sana, na kuleta madhara ya ghafla au ya muda mrefu...
Ikiwa hautapata matibabu mapema, ugonjwa huu unaweza kupelekea...
โณ Kufeli kwa Ini (Liver failure)
โณ Saratani ya Ini,
โณ Liver Cirrhosis (Ini kukak**aa na kufa taratibu)
Na baya zaidi...?
Huu ugonjwa hauna dalili za haraka, lakini unakutafuna kimyakimya hadi ujekugundua Ni umechelewa...
Njia za Maambukizi ya Hepatitis B
Virusi vya Hepatitis B huambukizwa kwa njia ya....
โณ Damu
โณ Jasho
โณ Mate
โณ Shahawa
โณ Maji maji ya uke
NB: Hata kugusana na damu ya mtu mwenye maambukizi bila kinga ni hatari kubwa...
Dalili za Hepatitis B โ Hatari Kimya Kimya..!
Dalili huanza kuonekana kuanzia mwezi mmoja hadi miezi minne baada ya maambukizi.
โณ Maumivu ya tumbo
โณ Mkojo mweusi
โณ Uchovu usioelezeka
โณ Homa kali
โณ Maumivu ya viungo
โณ Macho na ngozi kuwa na rangi ya manjano (Jaundice)
Lakini kumbuka, wengine hawana dalili kabisa, lakini wanawaambukiza wenzao bila kujuwa...
Na fahamu utaniuliza, Tiba ya Hepatitis B..?
Ikiwa ni ya muda mfupi (acute HepatitisB..)
โณ Mara nyingi huondoka yenyewe.
โณ Unahitaji kupumzika, lishe bora na maji ya kutosha kusaidia mwili kupambana na virusi...
Ikiwa ni ya muda mrefu (chronic Hepatitis B)
โณ Utahitaji tiba maalum ili kuzuia madhara zaidi na kulinda wengine usiwaambukize.
โณ Dawa zinazotumika ni sawa na zile za kufubaza virusi vya HIV (ARVs)...
Chanjoโ Kinga ni Bora Kuliko Tiba
Usingoje kuugua! Chanjo ya Hepatitis B ipo, salama na inafanya kazi vizuri sana...
Hupatikana kwa mfumo wa sindano tatu...
โณ Sindano ya Kwanza, baada ya kupima na kuthibitika huna maambukizi...
โณ Sindano ya Pili, baada ya mwezi mmoja...
โณ Sindano ya Tatu โ Baada ya miezi 6, kutoka sindano ya kwanza...
NB: Ikiwa unafanya kazi hospitalini, kliniki, kwenye saluni au unachora tattoo โ Chanjo hii ni lazima kwako!
Jitunze, Lindana, Elimisha Wengine.!
Usikae kimya na elimu hii โ Sambaza ujumbe huu kwa ndugu zako, marafiki wa karibu
Hebu tusaidiane kupunguza mzigo wa homa ya ini nchini mwetu.
โณ Fanya vipimo
โณ Pata chanjo
โณ Elimika na elimisha wengine
Imetolewa kwako na Dr nkindwa | Afya Kiganjani ๐ฒ๐ฉบ Elimu bora ya afya kwa watu wote...๐ซก