05/09/2023
KICHOCHO:
>Ni ugonjwa unaosababishwa na maambukizi ya vijidudu vya schistosoma. Vijidudu hivi vipo vya aina zaidi ya nne.
>Aina moja wapo inayoitwa schistosoma Haematobium ndiyo kwa kiasi kikubwa imekuwa ikipatikana katika mazingira ya nchi yetu.
>Aina hii hupatikana zaidi maeneo ya kanda ya ziwa na maeneo ya pwani mwa nchi yetu.
>Vijidudu hivi husambaa kati ya binadamu na konokono(aina ya bullinus) hususani kwenye uwepo wa maji yaliyotwama.
>Mara nyingi watu ambao hufanya shughuli zao katika mazingira ambayo maji yametwama huwa katika hatari ya kupata ugonjwa huu mf: kulima mpunga, kuogelea au Kutumia maji ya yaliyotwama (vidimbwi, bwawa n.k?) n.k hususani kwenye maeneo ambayo vijidudu hivi hupatikana.