25/05/2021
*Siku za hivi karibuni magonjwa yasiyoambukiza-NCDs yameshamiri sana* ....
>Matatizo ya akili
>Uzito mkubwa(overweight)
>insomnia (kukosa usingizi)
>Migraine /severe headache (kipanda uso/ maumivu makali ya kichwa)
>premature aging
>kisukari
>Anemia
>matatizo ya figo,moyo
Sababu znazotajwa ni nyingi ikiwemo *mfumo wa maisha* . Lakini stress ( msongo wa mawazo) ukitajwa k**a sababu kuu.
Stress zinapokuwa nyingi mwili huzalisha kwa wingi homoni ambayo hutumika kupambana na msongo wa mawazo.
Homoni hii huitwa cortisol ama stress hormone.
Uzalishwaji mwingi wa homoni hyo ndiyo huleta matatizo tajwa hapo juu.
NINI UFANYE ILI KUZUIA MWILI USIZALISHE CORTISOL KWA KIWANGO KIKUBWA?
Mwili sio mkaidi, mara nyingi huitikia na kutii sheria za maisha yako.
Katika kukabiliana na stress ambazo husababisha uzalishwaji wa cortisol fanya yafuatayo:
1. PATA USINGIZI WA KUTOSHA
Wataalam wanashauri tulale masaa 8, usingizi mzuri husaidia mwili kupumzika na kuufanya uwe active.
Vile vile husaidia kupunguza mawazo.
2.FANYA MAZOEZI KWA KIASI SAHIHI.
Mazoezi ya viungo husaidia sana kushusha kiwango cha cortisol pamoja na stress. Lakini pia huupa mwili ukak**avu na kuunguza kalori mwilini.
3.PATA MUDA WA KUFURAHIA MAISHA.
Tenga muda ambao utautumia ktk kujichangamsha aidha kwa kusikiliza mziki unaoupenda kutoka kwa waimbaji unaowapenda au kwa kufanya vitu ambavyo ni hobi yako.
4. CHAGUA WATU SAHIHI WA KUAMBATANA NAO.
Sio kila mtu anafaa kwa kila mtu, haimaanishi ni mbaya ila tu hamucope/hamclick pamoja.
Epuka watu wachonganishi, wambea, wagombanishi...bwana hawa watu watakuongezea tu stress.
Epuka watu watakaoku "pressurize", mfano unajijua hali yako ya kiuchumi basi usiambatane na watu ambao wao hawapitwi na fashion. Kwamba wakisikia gucci wamelaunch mkoba mpya basi atakuja kukuambia mkanunue ilhali wewe vyuma vimekaza hapo unajikuta unaingia katika aidha madeni.
Epuka watu wasiokuelewa! Rafiki mzuri ni yule anayetambua ubinadamu wako ambae hatakuhukumu wala kukunyanyapaa kwa madhaifu wako.
5. CHEKA/ TABASAMU KADRI UWEZAVYO.
Hii ni moja ya therapy/ tiba ya mambo mengi sana.
Jizoeshe kutabasamu hata pale mtu atapokuoneshea makasiriko yake kabla hujamjibu ama kumtamkia neno.
Tabasamu liwe utangulizi wa kila jambo ufanyalo.
Unapoamka asubuhi anza kwa kutabasamu.
Kucheka ama kutabasamu huchochea uzalishwaji wa dopamine (happy hormone) pamoja na serotonin (feel good hormone) .
Waliwahi kusema wazungu kwamba "smile is the makeup anyone can wear"
Tabasamu halilipiwi chochote wala TRA hawana tozo la kicheko wala tabasamu kwahyo jiachie tu kiongozi.
6. FANYA IBADA.
Sali/swali, omba kila wakati na uamini yupo yeye ambaye anakupigania ktk hali zote unazopitia. Weks tumaini kwa muumba wako kwamba hatokuacha ujaribiwe zaidi ya uwezo wako. Uonapo mambo yanakuwa magumu , ongea na Mungu kwa njia ya sala na maombi.
Imba mapambio, nyimbo za sifa na kuabudu badala ya kukaa kujikunyata na mawazo.
8. KUNYWA MAJI YA KUTOSHA
Jitahidi kuhydrate vya kutosha, usiogope kubanwa mkojo, maji ni tiba nzuri sana.
9. JALI MAISHA YAKO / MIND YOUR OWN BUSINESS
Achana na maisha ya watu, acha kufuatilia vitu havikuongezei ktk maisha yako. Una yako ya kufuatilia una uchumi wa kuuongeza, una afya ya kuijali etc.
10. SAMEHE/ACHILIA MAMBO YAPITE
Chuki humuumiza zaidi yule mwenye kuibeba kuliko yule mwenye kuchukiwa.
Umebeba makasiriko, chuki, visasi vya miaka buku jero, for what then?
Uache mwili na roho vipumue, kuna faida kubwa sana katika kusamehe.
Magonjwa mengi husababishwa na chuki, unaharibu mfumo wa hormone kwa kuhold grudges, unazeeka mapema kwa kujinunisha nunisha, una umwa mgongo na joints kwa kujibesha lawama.
Unaenda hospital unaambiwa hawaoni tatizo,ushameza dawa debe zima hadi serikali inalalamika upungufu wa dawa .
Hebu *SAMEHE* upone!
*Don't let impending stress affect the quality of your life.*
*Don't allow your body to produce too much cortiso* l.
Tunajali Afya Yako