01/02/2022
DALILI 10 ZA HATARI KATIKA UUME WAKO,
(KATIKA MFUMO WA KIZAZI).
Kuna dalili 10 ambazo hutakiwi kuzipuuza kabisa iwapo ukiziona katika uume wako.
1. Uume kutodinda (kutosimama) wakati wa asubuhi, ukiona hali hii usipuuze kabisa ewe mwanaume.
Hii ni dalili mojawapo ya upungufu wa nguvu za kiume, damu kutozunguka vizuri katika uume wako.
Mwanaume rijali ni lazima alfajiri uume usimame, tena unakuwa mgumu haswa, usipuuze ukiona tofauti.
2. Ukifika mshindo (kileleni), mbegu za kiume hazitoki, humwagi mbegu za kiume, usiipuuze hali hii.
Kuna tatizo la kiafya ambapo unapofika mshindo, badala ya mbegu za kiume kutoka nje, zinaenda kwenye kibofu cha mkojo.
Kuna njia mbili za kuitambua hali hii, njia ya kwanza ni kutoona manii (mbegu za kiume) baada ya kufika kileleni.
Njia ya pili ni kukojoa mkojo mzito, mithili ya wingu zito, ni kwa sababu ya manii zilizoenda kwenye kibofu cha mkojo.
3. Maumivu makali uume unaposimama, ambapo hudumu zaidi ya masaa manne.
Hii inaweza kusababishwa na hali mbili, kwanza kabisa ni kujeruhika kwa mishipa ya damu.
Pili ni mishipa ya damu kuziba, na hivyo damu kujaa katika uume bila kutoka kwa urahisi na kupelekea maumivu.
Ukiona dalili hii ya maumivu uume unaposimama, wasiliana na mtaalamu wako wa afya mapema.
4. Usaha kutoka katika mrija wa mkojo ambapo hali hii inaweza kuambatana na maumivu.
Hii inaweza kuwa ni dalili ya kisonono, na hutokea muda mfupi baada ya kupata maambukizi.
Kisonono ni ugonjwa wa zinaa, hivyo k**a umefanya ngono isiyo salama basi unaweza kukumbana na hali hii.
Ukiona usaha unatoka katika uume wako, muone mtaalamu wako wa afya haraka sana akusaidie.
5. Muwasho mkali katika bomba au njia ya mkojo, utaona muwasho ndani ya uume katika njia ya mkojo.
Hii inaweza kuwa ni dalili ya fangasi katika mrija wa uume, ndio maana unapata muwasho mkali.
Unaweza kutamani kukuna, lakini haiwezekani kwa sababu muwasho unatokea kwa ndani.
Hapa unafuu ni kuminyaminya uume wako, ndio utaona muwasho unapungua kwa kiwango fulani.
Ukiona dalili hii, onana na mtaalamu wako wa afya mapema akusaidia, usipuuze hali hii.
6. Uvimbe, kutoka damu katika uume, uchafu usio wa kawaida kutoka, maumivu au ngozi kuharibika.
Kuna saratani ya uume, japo ni tatizo ambalo haliwapati wanaume wengi sana, ila ipo kwa baadhi.
Ukiona dalili zisizo za kawaida k**a nilivyoorodhesha hapo juu, onana na mtaalamu wako wa afya mapema.
7. Kuota vinyama kuzunguka uume au sehemu ya mavuzi, hii nayo sio hali ya kupuuza iwapo ukiiona.
Onana na mtaalamu wako wa afya mapema iwapo ukiona hali hii katika uume wako.
8. Kufika kileleni mapema, au kumwaga mbegu za kiume mapema, kabla hata dakika tatu hazijaisha.
Hali hii inaweza kutokana na kukosa uzoefu wa tendo la ndoa, ugonjwa au tatizo katika saikolojia yako.
9. Uume kupinda, hali ya kuzaliwa nayo au kutokea wakati umri unavyozidi kuongezeka.
Uume kupinda inaweza kupelekea maumivu wakati wa tendo la ndoa au kumuumiza mpenzi wako.
Ukiona hali hii, ni vyema ukaonana na mtaalamu wako wa afya aweze kukusaidia mapema.
10. Kidonda katika kichwa cha uume wako, hii pia ni dalili ambayo hutakiwi kuipuuza uonapo.
Hii inaweza kuwa dalili ya kaswende, ugonjwa wa zinaa ambao huchelewa kuonekana tangu uambukizwe.
K**a una upungufu wa nguvu za kiume na changamoto nyengine za mfumo wa kizazi Wasiliana Nasi kwa
kupata ushauri na elimu zaidi ya kiafya,
WhatsApp +255694099982