24/08/2025
JE Nimsamehe mke wangu Baada ya Usaliti?
Huu ni ushuhuda binafsi, labda pia ni sababu ya Mimi kuwa na hii page, Nilioa miaka 20 iliyopita, kwa ndao nzuri tu ya Kanisani, Baba na Mama yangu walikuwa watumishi wa Mungu, wafanya kazi wa Serikali. Mimi nilikuwa nimemaliza chuo, na nilikuwa na Uchumba wa miaka mi 2 wa chuo, nilipomaliza nikamsaidia Mchumba wangu mambo madogo madogo naye ak**aliza.
Tulifunga ndoa za furaha na baada ya mwaka tulipata Mtoto wa Kwanza, miaka mi 5 baada ya ndoa nilik**ata mawasiliano ya mke wangu na X wake, ambaye ni wa kutoka high school ( Keshaoa ), Haikuwa na ushahidi sana, kwamba alilala naye, nikamsamehe.
Miaka 10 baadaye, nilimshika tena na yule mwanaume na wengine wawili tena ( Ma X ) Jumla wa watatu, sikusema kitu, ila nilidhamiria kumuacha, maana ilikuwa k**a surprise, nilikaa kwa maumivu mwaka mmoja tena kujiandaaa kuondoka kwa amani!
Ninachotaka kusema ni nini ?
1. Ukithibitisha mke kakusaliti hasa na X wake, ndugu yangu mwanaume, ondoka, usikae kabisa, maana kuna mambo mawili, la kwanza umempa ujasiri kwamba una samehe, la pili ; Anakuwa mjanja zaidi.
2. Ukikaa, unajipunguzia mda wako wa kutoka mapema na kuanza upya, Mimi ningeondoka miaka mitano tu nikiwa kwenye ndoa na watoto wawili, lakini nilikuwa kuondoka nikiwa na miaka 48 na watoto wa tatu ( Hasara zaidi )
3. Mwanmke akishaanza kukusaliti, anapokea order na maelekezo kutoka kwa mwanaume anayeshiriki naye, wewe unabaki kuwa mtoaji tu, ila Heshima, na hisia zote ni kwa mtu asiya na msaada wowot ?
Ndugu yangu, mwanaume mwenzangu, ingawa sio rahisi kuondoka, ila jipe mda, kwa amani kabisa, Jipange upya na uondoke, huna haja ya kufia humo ndani kwa maumivu, na hasira na kudhuru mtoto wa watu!