16/12/2025
Kunyonyesha ni njia ya asili ya uzazi wa mpango huitwa Lactational Amenorrhea Method (LAM). Ni njia salama na yenye ufanisi endapo vigezo maalum vitazingatiwa kikamilifu.
LAM ni njia ya kuzuia mimba inayotegemea kunyonyesha mara kwa mara na kwa ukamilifu, jambo linalozuia utolewaji wa yai (ovulation) kwa mama baada ya kujifungua.
Vigezo 3 muhimu vya LAM lazima vinazingatiwe, K**a ifuatavyo ;
1️⃣ Mtoto ana chini ya miezi 6
Baada ya miezi 6, mtoto huanza vyakula vya nyongeza hivyo ufanisi wa LAM hupungua.
2️⃣ Mama hajaanza kupata hedhi tangu ajifungue
Kutoka damu baada ya kujifungua (lochia) haichukuliwi k**a hedhi. Damu ya baada ya kujifungua kawaida hukoma kati ya week 6 hadi 8
Hedhi ikianza tuu mhimu mama akaanza kutumia njia zingine za uzazi wa mpango ambazo zitamkinga dhidi ya mimba zisizo tajarajiwa
3️⃣ Kunyonyesha kikamilifu (Exclusive or near-exclusive breastfeeding)
Hii ina maana:
Mtoto ananyonya mara nyingi mchana na usiku
Hakunywi maji, uji, maziwa mbadala au vyakula vingine
Hakai muda mrefu bila kunyonya (zaidi ya saa 4 mchana au saa 6 usiku)
Ufanisi wa LAM hufikia 98% ikiwa vigezo vyote vitazingatiwa kikamilifu
Ni sawa na baadhi ya njia za kisasa za uzazi wa mpango kwa miezi 6 ya mwanzo
Faida za LAM
✅Haina gharama
✅Haina homoni wala madhara
✅Hukuza afya ya mtoto (kinga, lishe bora)
✅Husaidia mama kupona haraka baada ya kujifungua
✅Hupunguza hatari ya kutokwa damu nyingi baada ya kujifungua
Mapungufu ya LAM
▪️Ni ya muda mfupi (miezi 6 tu)
▪️Haikingi dhidi ya magonjwa ya zinaa (STIs)
▪️Ufanisi hupungua haraka ikiwa mtoto hatonyonyeshwa mara kwa mara
▪️Inahitaji ufuatiliaji wa karibu wa hali ya mama na mtoto
Baada ya miezi 6 au kigezo kuvunjik Mama anashauriwa kuanza njia nyingine ya uzazi wa mpango (k**a kondomu, vidonge vinavyofaa kwa wanaonyonyesha, sindano, kitanzi n.k.)
Kunyonyesha ni njia nzuri ya asili ya uzazi wa mpango kwa muda mfupi, lakini inahitaji nidhamu na uelewa mzuri wa vigezo. Elimu kwa mama ni muhimu ili kuepuka mimba zisizotarajiwa.
Vipi wewe hedhi ili rudi baada ya mda gani...!?