18/04/2026
🎓✨ MKUTANO WA KWANZA WA MABALOZI WA AL-RAHMA✨🎓
Jana, tarehe 17-04-2025, kulifanyika mkutano wa kwanza wa wanafunzi Mabalozi wa Al-Rahma Schools waliomaliza Kidato cha Nne mwaka 2025.
Mkutano huu muhimu ulifanyika katika ukumbi mkubwa wa mikutano wa Shule ya Al-Rahmah, Mkurangapwani, ambapo wanafunzi walipata fursa ya kukutana, kubadilishana mawazo, na kuweka mikakati ya pamoja kwa ajili ya safari yao mpya ya uwakilishi na uongozi.
🌟 Tukio hili limeweka msingi imara wa mshikamano, uwajibikaji, na kuendeleza maadili mema ya Al-Rahma Schools katika jamii.
📍 Mahali: Al-Rahmah Schools, Mkurangapwani
📅 Tarehe: 17 Aprili 2025