31/01/2020
Tunapenda kuwataarifu kwamba kumefunguliwa kliniki mpya ya ushauri wa magonjwa ya upasuaji ndani ya Mtwara Mjini maeneo ya Shangani Magharibi barabara ya Masandube jirani na hosteli za Mama Mpini.
Kliniki hii inaongozwa na Daktari Bingwa wa magonjwa ya upasuaji kutoka Ulaya nchini Poland Dr. Jank ambaye aliwahi kufanya kazi zaidi ya miaka 25 katika hospitali ya Nyangao mkoani Lindi.
Tunasaidia katika matatizo yafuatayo:-
1. Magonjwa ya tumbo yasiyoeleweka k**a vile maumivu ya tumbo kwa muda mrefu, kujaa kwa tumbo, kuharisha, kushindwa kupata choo, kutapika na uvimbe tumboni
2. Matatizo katika njia ya mkojo k**a vile kushindwa kupata mkojo, kutokwa na mkojo bila kujizuia, maumivu katika njia ya mkojo, kutokwa na damu au usaha katika njia ya mkojo, maumivu katika kibofu cha mkojo au figo.
3. Matatizo katika njia ya haja kubwa k**a vile kutokwa na damu au usaha katika njia ya haja kubwa, maumivu wakati wa kujisaidia haja kubwa, uvimbe katika njia ya haja kubwa k**a vile bawasili n.k
4. Mabadiliko mbalimbali katika ngozi k**a vile uvimbe usiokuwa wa kawaida, kutokwa na damu katika ngozi bila sababu, vidonda sugu au fistula, kucha zinazoota vibaya mfano kujichimbia
5. Matatizo yatokanayo na kuumia/ajali k**a vile maumivu ya muda mrefu, ulemavu, kushindwa kutumia miguu au mikono naada ya ajali.
6. Matatizo sugu ya uti wa mgongo k**a vile maumivu ya mgongo, shida kukunja mgongo au shida ya kutembea.
Kwa mawasiliano zaidi piga namba 0623140254