25/02/2021
*CHEMBE YA MOYO NI NINI* ?
Ni maumivu ya kifua hasa upande wa kushoto hutokea wakati unafanya kazi au hata k**a umekaa k**a ni yenye kukubuhu.
Maumivu haya huambatana na kutokwa jasho na kukosa hewa.
Pia maumivu haya huanzia upande wa kushoto na kuzunguka mgongoni hadi shingoni upande wa kushoto
Wengi huweza kueleza k**a vile kuna mtu kamkaba au k**a tembo kamkanyaga kifuani
*KISABABISHI KIKUBWA* .
Ni moyo kutopata damu ya kutosha na hatimaye kutopokea hewa ya oxygen na hatimaye seli za misuli ya moyo huanza kuathirika na hatimaye kufa na baada ya kufa huathiri utengenezaji wa umeme kwenye moyo kusukuma damu vizuri
Damu kutofika sehemu husika kwenye moyo kuna matatizo mengi lakini kwa watu wazima mara nyingi ni Mafuta mengi ya cholesterol mbaya yani LDL.
triglycerrides na pia inaweza kusababishwa na magonjwa ya shinikizo la damu ukubwani( *HYPERTENSIVE HEART DISEASES)*
Kunapokuwa na presha kubwa kwenye mzunguko wa damu, kunapunguza uwezo wa moyo kusukuma damu kwenda sehemu mbalimbali za mwili na hasa kabisa hata moyo wenyewe unashindwa kujilisha chakula cha oxygen maana unapata kizuizi cha kusukuma damu, vidonda vya tumbo pia uchangia kutokea kwa tatizo hili kwani ukiwa na matatizo kwenye mfumo wa chakula inaweza kuathiri na mfumo wa damu na mwisho kupata ugonjwa wa pressure
[ *Chembe moyo husababishwa na nini*
maumivu ya chembe ya moyo
Chembe moyo au kwa kitaalamu stable angina au angina pectoris, ni aina ya maumivu ya kifua yanayatokea baada ya kupungua kwa mzunguko wa damu kwenye moyo. Kupungua kwa mzunguko wa damu husababisha kukosa hewa safi ya oksijeni kwenye moyo. Maumivu hutokea baada ya mwili kufanya kazi flani ama pale unapopata msongo wa mawazo.
Mumivu haya ya chembe moyo husababisha mtu kukosa raha, kuhisi k**a kifua kimejaa na kubana kwa kifua eneo la katikati.
*Chembe Moyo Hutokea Wakati gani?*
Chembe ya moyo hutokea pale misuli ya moyo inapohitaji damu ya kutosha zaidi kuliko kawaida, mfano wakati unafanya mazoezi, au unapokuwa na msongo wa mawazo. Unapokua umetulia mfano umekaa kwenye kitu kiwango cha hewa ya oksijeni kinachohitajika ni kdiogo, lakini unapokuwa kwenye shughuli k**a kupanda mlima au kukimbia moyo unahitaji kiwango kikubwa cha hewa na ndio matokeo ya chembe moyo.
*Dalili za Chembe Moyo*
Pamoja na 👉maumivu na kubana kwa kifua dalili zingine za chembe ya moyo ni k**a
👉Kushindwa kupumua vizuri
👉Kupata kichefuchefu
👉Mwili kukosa nguvu na kupata ganzi
👉Kutokwa na jasho na
👉Msongo wa mawazo,(huu uambatana na kukosa furaha au kushtuka mara kwa mara na kujawa uoga mkubwa ulio hawa na Uzuni mkubwa sana
👉Mazingira na tabia Hatarishi Zinazopelekea kupata Chembe moyo
👉Kuwa na uzito mkubwa na 👉kitambi
👉Kuwa na historia ya kugua magonjwa ya moyo
👉Kuwa na kiwango kikubwa cha cholesterol au shinikizo la damu kuwa juu
👉Mgonjwa wa kisukari
👉Uvutaji wa sigara
👉Kutofanya mazoezi au kushugulisha mwili
👉Kula mlo mkubwa na
👉Mazingira ya joto kali au baridi kali
*Vipimo kwa ajili ya chembe ya moyo*
Kabla ya kufanyiwa vipimo daktari aatakuuliza kuhusu historia ya tatizo lakona kisha kufanya vipimo hivi
*Electrocardiogram* : kipimo hichi hufatilia umeme ndani ya moyo na kuchambua uwiano.
*Angiography* : Kipimo cha x-ray ambacho huchunguza mishipa ya damu na kupima mzunguko wa damu kwenye moyo.
Vipimo hivi vinasaidia kujua k**a moyo unafanya kazi vizuri na k**a mishipa ya damu inapitisha damu vizuri.
*Matibabu ya Mgonjwa wa Chembe moyo*
Matibabu kwa ajili ya chembe moyo yanahusisha, kubadili mtindo wa maisha hasa kwenye vyakula unavyo kula kila siku na vinywaji unavyo tumia kila aiku, dawa na wakati mwingine upasuaji. Hakikisha unafatilia ni kipindi gani unapata maumivu, punguza mazoezi makali sana.
Mtindo wa maisha
Mabadiliko ya mtindo wa maisha husaidia kupunguza hatari ya kupata chembe moyo. Mabadiliko haya yanahusisha kufanya mazoezi ya mwili mara kwa mara, kula lishe nzuri, na kuacha kuvuta sigara. K**a unashndwa kuacha sigara, karibu kuagiza dawa kwangu zitakusaidia kukoma kuvuta sigara.
Mabadiliko haya ya mtindo wa maisha yatakusaidia pia kuepuka magonjwa mengine k**a kisukari, shinikizo kubwa la damu, na kuondoa cholesterol mbaya.
Dawa
Dakatari anaweza kukuanzishia dawa ili kupunguza maumivu ya chembe moyo. Pia kutokana na kisababishi chako cha chembe moyo k**a shinikizo kubwa la damu, cholesterol au kisukari au vidonda vya tumbo, daktari wako George atakuanzishia dawa ili kutibu chanzo cha tatizo.
Upasuaji
Upausaji ( *angioplasty* ) mara nyingi hutumika kwa wagonjwa wa chembe moyo. Upasuaji hulenga kutanua njia ya damu kweye mshipa ili kuruusu damu kupita.
*Ushauri kwa Mgonjwa*
K**a unapata dalili hizi mara kwa mara, weka muda wa kwenda ufanye vipimo kujua chanzo cha tatizo lako. k**a tayari umefanya vipimo pamoja na dawa ulizopatiwa , nashauri kutumia virutubisho vya kukusaidia kuondoa mafuta machafu ili kuondoa mafuta mabaya,kusafisha mishipa ya damu na kuimarisha mzunguko wadamu kuelekea kwenye moyo ili utibu chembe moyo
Dr George's clinic ina dawa inayo itwa *NURTICAL CARE* ni maalumu KWA ajili ya kuondoa mafuta machafu mwilini na Gharama yake. Ni ya chini Sana kwa mawasiliano zaidi kupata huduma hii 0658330156
*SISI TUNATIBU ILA MUNGU ANAPONYA*