Tunza afya yako

Tunza afya yako Tunatatua changamoto za magonjwa mbalimbali kwa kutumia virutubisho lishe.

17/07/2022

CHANGAMOTO YA KUVIMBA KWA TEZI DUME NA SULUHISHO.

MAWASILIANO; +255755717906

Wanaume wote wapo kwenye hatari ya kupata magonjwa ya tezi dume na hasa wanapofikia umri wa miaka 50.

Kutanuka kwa tezi dume:Prostate Enlargement

Hii ni hali ambapo tezi dume huongezeka ukubwa. Zaidi ya theluthi ya wanaume wote walio juu ya miaka 50 wana dalili za kuvimba kwa tezi dume. Haijajulikana kwa uhakika ni kwa nini tezi dume huwa kubwa zaidi kadri umri unavyoongezeka, lakini kukua huku si dalili ya kansa na wala hakuongezi uwezekano wa kupata kansa. Hili si tatizo kubwa sana la kiafya.

Tezi dume iliyoongezeka ukubwa huleta msukumo juu ya mrija wa mkojo na kibofu cha mkojo hali ambayo inaweza kuathiri namna mkojo utakavyotoka.

DALILI YA TEZI DUME ILIYOVIMBA.
1.Shida katika kuanza kukojoa au kuubana mkojo
2.Mtiririko dahifu wa mkojo
3.Kukojoa kwa shida
4.Kujisikia kuwa hujamaliza mkojo
5.Mkojo kuendelea kudondoka kwa muda mrefu baada ya kumaliza
6.Hali ya kujisikia kukojoa mara kwa mara au ghafla
7.Kuamka mara nyingi zaidi usiku kwa ajili ya kwenda haja ndogo
8. Pressure ya Mkojo kua ndogo

Kwa baadhi ya wanaume, dalili zinaweza kuwa ndogo ambazo hazihitaji tiba. Kwa wengine, zinaweza kuwa kubwa na kuathiri maisha yao. Wanaume hupatwa hofu kuwa kuvimba kwa tezi dume kunashahabihiana na upataji wa kansa ya tezi dume. Hii siyo kweli kwani uwezekano wa kupata kansa wa mtu mwenye tezi iliyovimba hauzidi ule wa mtu asiye na tatizo hili la tezi.

Sababu ya kuongezeka ukubwa wa tezi dume haijajulikana, lakini wataalamu wengi wanaamini kuwa inahusiana na mabadiliko katika homoni yanayotokea umri wa mtu unapokuwa mkubwa.

MADHARA YANAYOWEZA KUTOKEA KUTOKANA NA KUVIMBA KWA TEZI DUME/ BENIGN PROSTATE ENLARGEMENT NI;

1.maambukizi kwenye njia ya mkojo – UTI, kutokana na kuwa wadudu k**a bakteria waliomo kwenye njia ya mkojo hawataweza kusukumwa nje wakati wa kukojoa, .
2.Mkojo kushindwa kabisa kutoka
3.Madhara kweny kibofu na figo
4.Upungufu wa Nguvu za kiume, na kushindwa kuhimili tendo
5.Kansa ya Tezi dume
6.Huweza kusababisha kupoteza maisha K**a utashindwa kutibu tezi dume

MATIBABU
mara nyingi wenye changamoto hii wamekuwa wakitibiwa hospitalini kwa njia ya upasuaji na kupata matoeo mazuri kwa mda mfupi ila baada ya hapo changamoto hii huwarudia tena na kisababisha madhara mengine makubwa zaidi.
Ila kuna njia nyingie ya matibabu ya kuvimba kwa tezi dume bila upasuaji wowote kwa kutumia virutubisho lishe visivyo na kemikali na maranyingi njia hii imewasaidia wengi na tatizo kutojirudia tena kwa ushauri +255755717906

UKWELI KUHUSU BAWASIRI NA TIBA YAKEMshauri +255755717906Bawasiri ni mojawapo ya matatizo ambayo mara nyingi inapotokea h...
29/06/2022

UKWELI KUHUSU BAWASIRI NA TIBA YAKE

Mshauri +255755717906

Bawasiri ni mojawapo ya matatizo ambayo mara nyingi inapotokea humfanya muathirika kuwa na aibu kuelezea au kwenda hospitali ili kupata tiba.

BAWASIRI NI NINI?
-Bawasiri ni Ugonjwa unaotokana na kuvimba/kupasuka kwa mishipa ya dawa sehemu ya haja kubwa na kupelekea kuota kwa kinyama/Uvimbe ambao ndio huitwa Bawasiri.

Sababu kubwa ya mtu kupata Bawasiri ni Mgandamizo sehemu ya haja kubwa ambapo mgandamizo huo hupelekea kupasuka/kuvimba kwa mishipa midogo midogo ya damu aina ya veins sehemu ya haja kubwa hivyo hupelekea kuota kwa kinyama,miwasho,maumivu makali na kutoa damu

Ugonjwa huu umekuwa ni ugonjwa hatari kutokana na tabia za wagonjwa kuficha kutokana na aibu ya tatizo lenyewe lilipo au kuhofia jamii kumtazama tofauti kwa sababu jamii nyingi hasa za afrika mashariki zinaamini kuwa ugonjwa huu ni mkosi mkubwa.

DALILI ZA MTU MWENYE BAWASIRI
1.📎kupata muwasho mkali katika eneo la juu la haja kubwa
2.📎kujitokeza kwa kinyama/vinyama eneo la haja kubwa
3.📎kutokewa na kiuvimbe katika tundu ya haja kubwa
4.📎kupata kinyesi chenye damu
5.📎kupata maumivu makali wakati wa kujisaidia
6.📎 Kupata maumivu ya tumbo/kiuno hasa Bawasiri inapofikia hatua mbaya

AINA ZA BAWASIRI⤵️
-Kuna aina 2 za Bawasiri k**a ifuatavyo⤵⤵⤵⤵:
1⃣. BAWASIRI YA NJE
Ni kuota kinyama sehemu ya nje ya haja kubwa ambapo kinyama huwa nje hata k**a hujaenda kujisaidia haja kubwa.
2️⃣.BAWASIRI YA NDANI
Ni kuota kinyama sehemu ya ndani ya haja kubwa mara nyingi huambatana na maumivu makali na damu na kinyama hutoka wakati wa kujisaidia haja kubwa.

Bawasiri ya ndan ina hatua NNE ambazo ni:⤵⤵⤵⤵:
1. HATUA YA KWANZA
Katika hatua hii mtu hujihisi maumivu makali,miwasho pamoja na kutokwa damu wakati wa kujisaidia na kinyama hakionekan wakati wa kujisaidia.
2. HATUA YA PILI
Hii hutokea wakati wa haja kubwa na kurudi yenyewe punde baada ya kujisaidia
3.HATUA YA TATU
Hii hutokea wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kurudisha ndani yeye mwenywe ama inaweza kurud yenyewe baada ya muda
4. HATUA YA NNE
Hii ni bawasiri inayotoka na huwa ngumu kurudi baada ya kujisaidia.

VISABABISHI/MAMBO YANAYOWEZA KUSABABISHA MTU KUPATA BAWASIRI
1.🖇️ Uzito kupita kiasi(Overweight)
2.🖇️ Ujauzito
3.🖇️ Unywaji pombe
4.🖇️ Kukaa sana sehemu ngumu
6.🖇️Kujisaidia Choo Kigumu.Sababu za kujisaidia choo Kigumu ni:
-Vidonda vya TUMBO
-Ngiri/Hernia
-Ulaji duni
-Kuwa na acid mwingi tumboni
7.🖇️ Kula sana nyama nyekundu
8.🖇️ Presha ya kupanda
9.🖇️ Kula sana pilipili
10.🖇️ Kula udongo(Wajawazito na watoto wadogo)
11.🖇️ Kujisaidia kwenye vyoo vya kukaa
12.🖇️ Kuharisha kupita kiasi.
13.🖇️ Kufanyakaz ngumu/kunyanyua vitu vizito

MADHARA/ATHARI ZA BAWASIRI
1.📎Upungufu wa damu mwilini
2.📎Kutokwa na kinyesi bila kujitambua
3.📎kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa
4.📎kupungukiwa nguvu za kiume
5.📎kupungukiwa na uwezo wa kufanya kazi kutokana na maumivu
6.📎Kupata tatizo la kisaikolojia
7.📎Kutopata ujauzito
8.📎 Mimba kuharibika
10.📎 Kupata kansa ya utumbo ( Colorectal cancer)
11.📎 Mwili kudhoofika

NJIA ZA KUJIKINGA DHIDI YA BAWASIRI
1.📎Kula mboga za majani na nafaka zisizo kobolewa kwa wingi
2.📎kunywa maji mengi lita 2.5 hadi 3 kwa siku
4.📎Punguza kukaa chooni kwa muda mrefu, kunaweza kuongeza shinikizo katika njia ya haja kubwa.
5.📎 Acha kunywa pombe
6.📎Punguza kula nyama nyekundu
7.📎Punguza matumizi ya pili pili.
8.📎Jitibie vidonda vya tumbo
9.📎 Jitibie Ngiri
10.📎 Dhibiti uzito wako
11.📎 Jiepushe/punguza kunyanyua vitu vizito mara kwa mara

MATIBABU YA UGONJWA WA BAWASIRI
Kuna matibabu aina mbili katika kutibu ugonjwa wa Bawasiri:
1.📎 MATIBABU YA KISASA
-Matibabu ya kisasa yanahusisha matibabu ya Hospital ambapo tiba kubwa ya Bawasiri kwa hospital ni kufanyiwa upasuaji mdogo ( minor surgery) kwaajili ya kuondoa kinyama. Changamoto kubwa ya matibabu haya ni kwamba asilimia kubwa ya wagonjwa wanaofanya upasuaj wa tatzo hili tatizo hujirudia kwasababu upasuaji huondoa athari ya tatzo na si mzizi wa tatizo yaani ni sawa na kukata mti kisha ukaacha mizizi bila shaka mti huo utachipua na kumea tena.Lakini pia Upasuaji wa Bawasiri huwa na maumivu makali sana na uponaji wa kidonda hufika mpaka miezi miwili,hali hii ya kukaa na kidonda kwa muda mrefu kunaweza kupelekea kupata Kansa ya utumbo ( Colorectal Cancer).

2.📎 MATIBABU KWA NJIA ASILI
-Matibabu haya yanahusisha utumiaji wa dawa zinazotokana na mimea dawa.Dawa hizi Hutibu Bawasiri bila kufanya upasuaji na huweza kuleta matokeo ya haraka kwa mgonjwa endapo atatumia dawa huku akijitahid kujiepusha na visababishi vyote vinavyopelekea mtu kupata Bawasiri. Endapo unachangamoto hii wewe au ndugu au rafiki tiba ipo hivyo usisite wala usiogope zungumza.

MVURUGIKO WA HOMONI (HOMONAL IMBALLANCE)Mshauri +255755717906Kuvurugika kwa homoni za k**e ni suala pana linalojumuisha ...
26/06/2022

MVURUGIKO WA HOMONI (HOMONAL IMBALLANCE)

Mshauri +255755717906

Kuvurugika kwa homoni za k**e ni suala pana linalojumuisha vyanzo vingi, k**a mtindo wa Maisha (lifestyle), umri kwenda, sababu za kimazingira k**a msongo wa mawazo. Sababu zote hizi zinaathiri uzalishaji na ufanyaji kazi wa vichocheo ama homoni zako.

Mvurugiko wa homoni za mwanamke ni hali ya kuongezeka au kupungua kwa vichocheo katika mwili wa mwanamke pale anapo pata hedhi, hivyo kufanya mwili kubadilika.

Asilimia kubwa ya wanawake mabadiliko huanza kati ya miaka 40 na 50, lakini pia kukosekana kwa usawa wa homoni huweza kuonekana mapema zaidi, kuanzia miaka 14. Mabadiliko haya asilimia kubwa huanza kutokea wakati wa balehe, hedhi, ujauzito, kabla na baada ya ukomo wa hedhi.

Hii husababishwa na kutokuwepo na usawa katika homoni zifuatazo Estrogen, Progesterone na Testosterone.

Napenda niseme tu kwamba moja ya sababu kubwa iliyonigusa kuandika elimu hii juu ya kuvurugika kwa homoni za k**e ni ukubwa wa tatizo. Kwani tatizo hili limekuwa ni tatizo ambalo kila mwanamke analo na wengi wao wametumia kila mbinu ya kuondoa tatizo na wameshindwa.

VYANZO VYA MVURUGIKO WA HOMONI

•Uwepo wa takamwili nyingi na sumu mwilini
•Unbalanced Lifestyle (mfumo mbovu wa maisha)
•Umri ukienda sana
•Kukoma kwa hedhi
•Kutofanya mazoezi
•Uzito mkubwa
•Mabadiliko ya mazingira au hali ya hewa
•Msongo wa mawazo
•Upungufu wa lishe mwilini
•Matumizi ya njia za kisasa za uzazi wa mpango
•Utoaji wa mimba
Family History (Upungufu au ongezeko la homoni ya progesterone na Estrogen)
Ongezeko la homoni ya Androgen. Progesterone na Testosterone. Kupungua au kuzidi kwa homoni hizi kupelekea mvurugiko wa homoni kwa mwanamke.

DALILI
- Ukavu ukeni
- Maumivu wakati wa tendo la ndoa
- Maumivu chini ya kitovu wakati wa hedhi
- Upungufu wa hamu ya tendo la ndoa
- Mabadiliko ya siku za hedhi na kupata hedhi kwa muda mrefu unaozidi siku 7. (heavy bleeding, au kujaza pedi moja kwa saa moja)
- Kukosa hedhi kwa muda mrefu, na kutoa damu yenye mabonge mabonge wakati wa hedhi
- Uchovu wa mara kwa mara
- Hasira za mara kwa mara
- Kukosa usingizi
- Homa za usiku na Kizunguzungu cha mara kwa mara
- (Allergie), kuchagua chagua vyakula
- Ongezeko ya tumbo na nyama uzembe
- Kuharibika kwa ngozi (chunusi, vipele… n.k)
- Maumivu ya viungo
- Upungufu wa nywele kichwani.
- Kusahau sana (kukosa kumbukumbu)
- Kupata hedhi wakati wa ujauzito (progesterone ikiwa imezidi)
- Kutokupata hedhi (balehe) adi umri wa miaka 20 na kuendelea
- Mwili kutokukua, kuonekana k**a binti mdogo, na kutokukua kwa via vya uzazi
- Msongo wa mawazo na kukosa kujiamini
- Kusinyaa na kupauka kwa
ngozi wakati wa siku za hedhi na wakati wa utumiaji wa njia za uzazi wa mpango
- Maumivu ya kichwa mara kwa mara
- Kuwa na tabia ya hamaki (kukosa utulivu)
- Kutokupata choo kwa wakati

MADHARA

Ukiendelea kubaki na dalili tajwa hapo awali kwa muda mrefu, kinga ya mwili itashuka kwa kiasi kikubwa na kusababisha madhara mengi k**a yafuatayo:
-Kutoshika ujauzito kwa muda mrefu
-Mimba kuharibika mara kwa mara
-Kukosa mtoto au Ugumba
-Maumivu wakati wa tendo la ndoa
-Kuwa na tabia na maumbile ya kiume
-Kuzeeka mapema
-Kuziba kwa mirija ya uzazi
-Uvimbe (Fibroids and Cysts)

SULUHISHO
Zipo dawa ambazo hutolewa na maranyingi huleta matokeo chanya kwani wengi wao huona dalili zilizowafanya wagundue wana tatizo hilo hazipo tana na kuhisi wamepona na baada ya muda shida hiyo huwarudia maana homoni bado hazijarudi katika mpangilio wake.
Hivyo basi kwa kupata suluhisho lakudumu zipo bidhaa asilia ambazo zitakusaidia katika mpangilio wa homoni zako na kuondoa tatizo hilo

23/06/2022

Address

Igoma
Mwanza
11367

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Tunza afya yako posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram