24/09/2025
UCHAFU UKENI (Vaginal Discharge)
Kutoka uchafu ukeni ni hali ya kawaida, ingawa kuna uchafu unaotoka ambao unaashiria uwepo wa maambukizi, hasa pale unapotoka mwingi kupita kiasi, wenye rangi ya njano au kijani na ukiwa na harufu isiyo ya kawaida, mfano harufu kali, au harufu k**a ya samaki.
Uke wa mwanamke hufanya kazi ya kutoa njia kati ya sehemu ya nje ya mwili na viungo vya uzazi vya ndani vya mwanamke.
Hali ya kawaida ya majimaji yaliyomo katika uke wa mwanamke huwa ni ya tindikali ili kuzuia maambukizi ya vijidudu wa kuleta maradhi.
Hali hii ya utindikali huletwa na bacteria waishio katika uke wa mwanamke.
Bacteria hawa ni wa kawaida na hawana madhara kwa mwili.
Uke ulio katika hali nzuri hutoa majimaji haya ili kujisafisha.
Majimaji haya yanayotengenezwa katika uke na kwenye eneo la cervix hufanya kazi ya kuondoa seli zilizokufa na bacteria waharibifu nje ya mwili na huu ndio uchafu wa kawaida ambao mwanamke hutoa ukeni.
Kutoa uchafu huu sehemu za siri ni njia ya kuusafisha uke na kuzuia maambukizi ya magonjwa.
Kitu cho chote ambacho kitaharibu uwiano wa utengeneaji wa majimaji haya ndani ya uke kinaweza kujenga mazingira ya maambukizi katika uke.
Kila mwanamke anapaswa kujichunguza kila siku ya maisha yake maeneo yake ya uzazi na matiti, vile vile kuichunguza nguo ya ndani aliyokuwa ameivaa siku hiyo k**a kuna uchafu wowote.
Kufanya hivi kunaweza kumsaidia kugundua kuwa ana tatizo la kiafya, kwani wapo baadhi ambao hawafahamu kuwa kila siku huwapo ute ute unaomtoka ambao ni hali ya kawaida.
Ute huo unaweza kuwa na ujazo wa nusu kijiko cha chai na huwa na harufu asilia ya uke na huwa na rangi nyeupe au kahawia mpauko k**a chai isiyokolea rangi bila kuwa na harufu mbaya.
Utokaji wa ute huo ni mojawapo ya njia ya uke kujisafisha kwa kutiririka pamoja na mabaki ya hedhi au takataka za mwili au zilizotoka nje ya mwili.
Ute huu huzalishwa na kuta za nyumba ya uzazi na huzifanya tezi za ukeni kushuka chini kutokana na kani ya nguvu za uvutano (gravity).
Uchafu wa kawaida ukeni (Normal vaginal discharge)
Wanawake wote hutoa uchafu ukeni, Kiwango cha uchafu unaotoka, rangi yake na harufu yake vitabalikabadilika kutoka kipindi kimoja hadi kingine kulingana na muda mwanamke aliopo katika mzunguko wake wa mwezi.
Uchafu huu utabadilika vilevile k**a ananyonyesha, atakuwa na hisia za kufanya mapenzi, atakuwa na mabadiliko ya lishe, anatumia madawa hasa ya mpango wa uzazi au atakuwa na ujauzito.
Kwa kawaida uchafu huu huwa usio na rangi, wenye rangi yenye weupe wa mawingu au njanonjano pale unapokaukia kwenye nguo. Unaweza kuwa na vijipande vidogovidogo na mara nyingine ukawa wa kunatanata.
Clear and watery
Uchafu usio na rangi huu ni wa kawaida, Hutokea muda wowote katika mwezi, unaweza kuwa mwingi baada ya kumaliza kufanya mazoezi.
Clear and stretchy
Wakati uchafu usio na rangi lakini unaovutika na kunatanata, mzito kidogo unapotoka, huashiria uchevushwaji (Ovulating). Huu huwa ni uchafu wa kawaida.
Uchafu wa Ukeni usio wa kawaida (Abnormal vaginal discharge).
Ishara Na Dalili za uchafu wa Ukeni usio wa kawaida.
Ukiona yafuatayo, ujue unaweza kuwa na tatizo la maambukizi ya vijijidudu vya maradhi katika uke wako:
🖋️Kutokwa na uchafu ukeni kunakoambatana na kuwashwa au vijipele.
🖋️Kutokwa na uchafu ukeni ambako ni endelevu na kwa kiwango kinachozidi kila siku.
🖋️Kusikia maumivu wakati wa kutoa haja ndogo.
🖋️Kutokwa na uchafu mweupe, mzito k**a jibini.
🖋️Uchafu wa kijivu/mweupe au njano/kijani unaotoa harufu mbaya.
MUHIMU;
TUNAFANYA KAZI KUPITIA ONLINE, HIVYO UAMINIFU NI KIPAUMBELE CHETU KIKUBWA, HATUNA MAWAKALA POPOTE, ILA TUNATUMA POPOTE KWA UHAKIKA NA UAMINIFU MKUBWA.
Kwa tiba zisizo na kemikali kwa maambukizi ukeni, wasiliana nasi kwa;
0769247626.