21/06/2025
⛪ 🇹 🇪 🇨 ⛪
Kanisa Katoliki nchini Tanzania limezuia rasmi kuwapa nafasi viongozi wa Kisiasa na Kiserikali kuongea, kutoa hotuba, Pongezi na kusalimia mbele ya waumini ndani ya Kanisa. Waraka wa kuzuia jambo hilo umetolewa na baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC).
Baraza la Maaskofu Katoliki nchini (TEC), limepiga marufuku viongozi wa serikali/kisiasa kuitwa mbele ya madhabahu/altare kuongea, kutoa hotuba, kusalimia au kusema chochote. K**a Misa imehudhuriwa na Rais, Waziri, Mbunge au kiongozi mwingine yeyote, Padre/Askofu anayeendesha ibada atatambua uwepo wake bila kumpa nafasi yoyote ya kuongea. Ikiwa kiongozi ana sadaka au neno la shukrani basi Katekista, Padre au Askofu atatoa shukrani hizo kwa niaba ya kiongozi husika. Roma locuta, causa finita est. Roma ikisema, mjadala umefungwa. Tumsifu Yesu Kristo
Viongozi wa kiserikali na kisiasa ni marufuku kutoa hotuba au salamu kanisani. Mwadhimishi atatambua uwepo wao bila wao kusema neno.
Huu ndiyo ukuu wa kanisa KATOLIKI.
Mwezi wa 8 Kanisa katoliki TANZANIA limetangaza itakuwa ni siku ya kuombea haki na siyo amani,kuombea haki kwa nchi