17/07/2023
KULA CHUMA HICHO
NINI HASWA MAANA YA UPENDO.
Date: October 9, 2017Author: Hosea P. Gambo Jnr.6
Shalom watu wa Mungu;
Leo napenda tukajifunze maana halisi ya neno upendo. Sisi vijana tunatumia sana neno upendo. Love….
I love you!
Biblia katika kitabu cha Marko12:29-31 inasema upendo ni “amri ya kwanza”. Katika kitabu cha Mathayo 22:36-40 biblia inasema upendo ni “amri kuu”. Tunaona upendo ni kitu cha msingi sana katika maisha yetu ya ukristo.
Upendo?
Biblia inasema “upendo ni Mungu” 1Yoh.4:8b; 16. Biblia inaendelea kusema katika upendo Mungu anakaa ndani yetu nasi ndani yake. Mungu anakaa ndani yetu katika Roho mtakatifu (1Yoh.3:24).
Point: Kuwa na upendo ndani yako ni kuwa na Mungu ndani yako.
Mungu ni mtakatifu; hivyo aliye na Mungu ndani yake naye ni mtakatifu. Upendo hutuongoza katika mema yote.
Neno la Mungu linasema; 1Yoh.3:18 tusipende kwa ulimi wala kwa neno, bali kwa tendo na kweli. Tusipende kwa midomo; kwamba unamtangazia mtu kuwa unampenda; unatongoza! bali mwenye upendo wa dhati anaonesha katika matendo.
Advertisements
REPORT THIS AD
Vijana wengi wamepotea kwa kudhania kitofauti matendo yanayoashiria upendo. Wengine wamedhania uzinzi; lakini hapo wameangukia katika kifo au dhambi. Biblia inasema tena, 2Petro2:13-14 kuna watu ambao wasiokoma kutenda dhambi, wenye macho yajaayo uzinzi, wenye mioyo iliyozoezwa kutamani… wana wa laana!
Kumbe wapo ambao wanadhani wanapenda kumbe wanatamani tu; wana wa laana! hao ni hatari kwa karamu yenu ya upendo. Wanatamani zinaa na anasa zote; hawakufai kwa kuwa hao watakutenganisha na Mungu wako, yaani watauondoa upendo ndani yako. Haleluya!
Upendo ni kutenda matendo mema. Biblia inasema tupatapo nafasi tuwatendee mema watu wote, Galatia 6:9-10. Tena Neno la Mungu linasema, utawezaje kumpenda Mungu usiyemwona wakati unamchukia ndugu yako unayeishi naye?
Biblia inasema Marko12:31 mpende Bwana Mungu wako;
1.kwa moyo wako wote,
2.kwa roho yako yote,
3.kwa akili zako zote na
4.kwa nguvu zako zote.
Sehemu ingine Yesu anasema nilipokuwa mgonjwa hamkuja kuniona; nilipokuwa na kiu hamkuninyesha maji; nilipokuwa na njaa hamkunilisha… Mlivyokuwa mnawatendea wale ndugu ndivyo mlinitendea.
Point: ili kumpenda Mungu; kwa moyo wote, kwa akili zote na kwa nguvu zote hatuna budi kufanya hivyo kwa ndugu zetu tunaoishi nao.
Luk10:30-37 tunakuta mfano alioutoa Bwana Yesu; mtu mmoja aliyekuwa akisafiri kutoka Yeriko kwenda Yerusalem aliangukia mikononi mwa wanyang’anyi, vibaka, majambazi… Wakamnyanganya kila kitu hata nguo; walimpiga sana wakamtupa akiwa mahututi karibu kufa.
Alipita kuhani, akamwangalia akampuuza; akafuata mlawi akamwona akampuuza lakini alipita msamaria akamwona akamhurumia. Akamsaidia kwa moyo wake wote, kwa akili zake zote na kwa nguvu sake zote. Msamaria huyo alikuwa na upendo ndani yake; alikuwa na Mungu ndani yake, alikuwa na roho mtakatifu.
Tujitahidi wapendwa kuwa na upendo ndani yetu, kuwa na Mungu ili tuishi katika misingi imara ya wokovu. Mungu awabariki sana.
HAYA NI MAANDIKO TAJWA KATIKA MAKALA HII.
“Yesu akamjibu, Ya kwanza ndiyo hii, Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja; nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote. Na ya pili ndiyo hii, Mpende jirani yako k**a nafsi yako. Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi.” Marko 12 :29-31
“Mwalimu, katika torati ni amri ipi iliyo kuu? Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote. Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza. Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako k**a nafsi yako. Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii.” Mathayo 22 :40
“Mwalimu, katika torati ni amri ipi iliyo kuu? Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote. Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza. Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako k**a nafsi yako. Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii.” Mathayo 22 :36-40
“Yeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo.” 1 Yohana 4 :8
“Nasi tumelifahamu pendo alilo nalo Mungu kwetu sisi, na kuliamini. Mungu ni upendo, naye akaaye katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake.” 1 Yohana 4 :16
“Watoto wadogo, tusipende kwa neno, wala kwa ulimi, bali kwa tendo na kweli.” 1 Yohana 3 :18
“Naye azishikaye amri zake hukaa ndani yake yeye naye ndani yake. Na katika hili tunajua ya kuwa anakaa ndani yetu, kwa huyo Roho aliyetupa.” 1 Yohana 3 :24
“Wakipatikana na madhara, ambayo ni ujira wa udhalimu wao, wakidhania kuwa ulevi wakati wa mchana ni anasa; wamekuwa ni mawaa na aibu wakifuata anasa zisizo kiasi katika karamu zao za upendo, wafanyapo karamu pamoja nanyi; wenye macho yajaayo uzinzi, watu wasiokoma kutenda dhambi, wenye kuhadaa roho zisizo imara, wenye mioyo iliyozoezwa kutamani, wana wa laana;” 2 Petro 2 :13-14
“Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho. Kwa hiyo kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema; na hasa jamaa ya waaminio.” Wagalatia 6 :9- 10
“Yesu akajibu akasema, Mtu mmoja alishuka toka Yerusalemu kwenda Yeriko, akaangukia kati ya wanyang’anyi; wakamvua nguo, wakamtia jeraha, wakaenda zao, wakimwacha karibu ya kufa. Kwa nasibu kuhani mmoja alishuka kwa njia ile; na alipomwona alipita kando. Na Mlawi vivyo hivyo, alipofika pale akamwona, akapita kando. Lakini, Msamaria mmoja katika kusafiri kwake alifika hapo alipo; na alipomwona alimhurumia, akakaribia, akamfunga jeraha zake, akizitia mafuta na divai; akampandisha juu ya mnyama wake, akampeleka mpaka nyumba ya wageni, akamtunza. Hata siku ya pili akatoa dinari mbili, akampa mwenye nyumba ya wageni, akisema, Mtunze huyu, na cho chote utakachogharimiwa zaidi, mimi nitakaporudi nitakulipa. Waonaje wewe, katika hao watatu, ni yupi aliyekuwa jirani yake yule aliyeangukia kati ya wanyang’anyi? Akasema, Ni huyo aliyemwonea huruma. Yesu akamwambia, Enenda zako, nawe ukafanye vivyo hivyo.” Luka 10 :30-37