21/10/2017
MTAJI MUHIMU ZAIDI MAISHANI
"Binadamu yeyote hupenda kuona akifanikiwa maishani mwake. Katika biashara kuna kitu kinaitwa mtaji, ili uanzishe biashara na kupata mafanikio,unahitaji mtaji. Utakubaliana na mimi kuwa kuna aina nyingi za mitaji lakini fedha ni mtaji unaothaminiwa sana, kila anayetaka kuanzisha biashara hujiuliza nipate wapi pesa k**a mtaji.
Leo nitakuambia mtaji uliobora zaidi kuliko fedha, huu ni mtaji ambao unapaswa kuutafuta kwanza hata kabla ya kutafuta mtaji uitwao fedha, mtaji huu si mwingine bali ni AFYA ILIYOBORA.
Afya iliyobora hujumuisha afya ya kimwili, kiakili, kijamii na kiroho. Pasipo kuwa na afya bora huwezi kutafuta mtaji aina ya pesa, unapaswa kuwa na mtaji wa afya ili upate nguvu ya kutafuta mtaji wa fedha. Ndio maana nadiliki kusema kuwa TAIFA LITAKALO WEKEZA ZAIDI KATIKA AFYA ZA WANANCHI WAKE, LITAPATA MAENDELEO MAKUBWA KULIKO TAIFA LILILOWEKEZA KIDOGO KATIKA AFYA ZA WANANCHI WAKE .
Pia kuwa na afya bora hakugonji kuletewa huduma bure za afya kwa kila mwananchi, bali afya bora huanza na mtu binafsi kuamua yeye mwenyewe kuwa msafi wa mwili na mazingira, kula mlo kamili,kufanya mazoezi,kuwa na kiasi kwa kila jambo, kulala katika neti n.k,hii itakufanya ujikinge na magonjwa mengi ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza.
Kinga ni bora kuliko tiba.
Pasipo kuwa na afya bora hakuna maendeleo. Tafuta kwa bidii kubwa mtaji uitwao AFYA BORA, kabla hujatafuta aina zingine za mitaji k**a fedha,maana afya bora ndio itakufanya ukamilishe mipango yako yote maishani.Watu waliofanikiwa duniani waliwekeza zaidi katika afya zao.
Jaribu kufikiria, endapo mgonjwa mahututi akipewa mtaji/pesa, itamsaidia nini hiyo pesa? , zaidi itatumika katika matibabu ila si katika kuwekeza kwa ajili ya maendeleo yake binafsi . mfano huu unatuwezesha tujue kipi ni muhimu zaidi kati ya pesa na Afya bora.
Mtaji ulio wa muhimu zaidi maishani ni afya bora kwa sababu mtaji huu hukufanya utafute mitaji mingine".
"Afya yako, mtaji wako ".
"Jali afya yako, ikujali pia" .
Asante sana kwa kusoma mada hii muhimu, endelea kufatilia mada zangu mbalimbali.
Dr. Obed Kabinza L, MD