Njombe RRH

Njombe RRH Ukurasa Rasmi wa Hospitali ya
Rufaa Mkoa wa Njombe
59017 Ramadhani -Njombe
P. O Box 1044 Njombe

27/03/2026
Upatapo Taarifa hii tunaomba uisambaze iwafikie wengine.Tunaomba ushirikiano wako, kuwapata ndugu zake.
26/03/2026

Upatapo Taarifa hii tunaomba uisambaze iwafikie wengine.

Tunaomba ushirikiano wako, kuwapata ndugu zake.

Jopo la Madaktari kutoka Idara ya Magonjwa ya Akina Mama na Uzazi likiongozwa na Daktari Bingwa, Emmanuel Mafwiri, wamef...
26/03/2026

Jopo la Madaktari kutoka Idara ya Magonjwa ya Akina Mama na Uzazi likiongozwa na Daktari Bingwa, Emmanuel Mafwiri, wamefanikiwa kutoa vimbe mbalimbali (Multiple Mayoma) katika Mji wa Uzazi kwa mwanamke anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 31 (jina limehifadhiwa) mkazi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe baada ya kukaa na uvimbe huo kwa takribani miaka 2.

‎Mafanikio ya Upasuaji huo ni sehemu ya uratibu wa Kambi ya Madaktari Bingwa na Bingwa Bobezi inayoendelea katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe kwa siku ya nne sasa.

‎Akizungumza baada ya Upasuaji huo Dkt. Mafwiri amewaasa wanawake wenye changamoto zenye uvimbe na masuala mbalimbali yanayohusu uzazi kuendelea kujitokeza katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe kwakuwa Kliniki za kibingwa zinazoendelea zitabaki kuwa endelevu.


18/03/2026

Tunawakaribisha sana

Uwepo wa Kambi ya Madaktari Bingwa na Bingwa Bobezi, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe, kuanzia tarehe 23 Machi hadi ...
12/03/2026

Uwepo wa Kambi ya Madaktari Bingwa na Bingwa Bobezi, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe, kuanzia tarehe 23 Machi hadi 27 Machi 2026

Wananchi wa Mkoa wa Njombe na mikoa jirani, nyote Mnakaribishwa
06/03/2026

Wananchi wa Mkoa wa Njombe na mikoa jirani, nyote Mnakaribishwa

Karibu kila Siku za Wiki kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa uweze kukutana na Madaktari Bingwa katika Maeneo mbalimbali ikiwem...
24/02/2026

Karibu kila Siku za Wiki kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa uweze kukutana na Madaktari Bingwa katika Maeneo mbalimbali ikiwemo

➡️ Ubingwa katika Upasuaji wa Mifupa

➡️ Ubingwa katika Magonjwa ya Watoto

➡️ Ubingwa katika Magonjwa ya Ndani

➡️ Ubingwa katika Upasuaji wa Jumla

➡️ Ubingwa katika Magonjwa ya Wanawake na Uzazi

➡️ Ubingwa katika Tiba ya Pua, Koo na Sikio

➡️ Ubingwa katika Dawa za Usingizi na Ganzi salama.

AUGUSTINO SANGA ACHAGULIWA MWENYEKITI MPYA TUGHE, NJOMBE RRHWanachama wa TUGHE, Tawi la Njombe RRH, wamechagua Uongozi m...
19/02/2026

AUGUSTINO SANGA ACHAGULIWA MWENYEKITI MPYA TUGHE, NJOMBE RRH

Wanachama wa TUGHE, Tawi la Njombe RRH, wamechagua Uongozi mpya hapo jana Februari 18 katika ngazi mbalimbali.

Augustino Sanga amechaguliwa kuwa Mwenyekiti, Irene Kayombo kuwa Katibu.

Pia wamechaguliwa viongozi wa Kamati za Wanawake ambapo Mwenyekiti wake ni Monique Eliut Kimbago, huku Katibu wake akiwa Nuru Msanga.

Wengine walioteuliwa ni wajumbe 15 na mwakilishi wa walemavu na mwakilishi wa Vijana/Mwenezi wa tawi.

Tunawatakia Majukumu Mema.
"Mshik**ano Daima"

Timu ya Usimamizi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe (RRHMT) wametakiwa kusikiliza changamoto za watumishi walio ch...
12/02/2026

Timu ya Usimamizi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe (RRHMT) wametakiwa kusikiliza changamoto za watumishi walio chini yao na kuzitatua ili kujenga mahusiano mazuri na kujenga uwajibikaji mahali pa kazi.


‎Akizungumza na Timu ya Usimamizi wa Hospitali leo Februari 12, 2026 Bi. Kisa Mwamaso - Afisa Rasilimali Watu, kutoka Wizara ya Afya amesema ipo haja ya kuzingatia usiri wa taarifa/changamoto za watumishi wakati wa utatuzi ili kuwajengea imani dhidi ya viongozi wao.


‎Ameongeza kuwa changamoto za kuhama kwa watumishi kwa kiasi zinachangiwa na kukosekana kwa masikilizano mazuri baina ya viongozi na watumishi waliopo chini yao, hali inayosukuma kuhama na kutafuta suluhisho la matatizo yao mahali pengine.


‎Amewataka Viongozi na watumishi waliopo chini yao kufuata sheria na utaratibu wa Utumishi wa Umma kwa kusimamia maadili pamoja na kutatua changamoto za watumishi ili kuhakikisha watumishi waliopo chini yao wanafuata pia sheria hizo.


‎Mathalani; ameshauri watumishi wasisitizwe kufuata mnyororo sahihi wa mawasiliano,uvaaji unaofuata miongozo ya Utumishi wa Umma, kuepuka matumizi ya pombe na lugha isiyo na staha, kufika kazini kwa wakati, kutojihusisha na tabia zinazovunja sheria za nchi k**a rushwa.

‎TUNATAKA NJOMBE RRH IWE KINARA WA HUDUMA BORA, NYANDA ZA JUU KUSINI - BALOZI MPUMILWAMwenyekiti wa Bodi ya Ushauri, Hos...
06/02/2026

‎TUNATAKA NJOMBE RRH IWE KINARA WA HUDUMA BORA, NYANDA ZA JUU KUSINI - BALOZI MPUMILWA

Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe, Balozi Danford Mpumilwa amesema Bodi ya Ushauri na Timu ya Uendeshaji wa Hospitali (RRHMT) watashirikiana kuhakikisha Njombe RRH inaboresha huduma zake hadi kuwa Kinara wa huduma bora Nyanda za Juu Kusini. ‎ ‎ ‎

Balozi Mpumilwa ameyasema hayo leo Ijumaa, Februari 6, 2026 aliposhiriki Kikao cha Maandalizi ya Bajeti ya Hospitali kwa mwaka wa Fedha 2026/2027 kinachofanyika Halmashauri ya Mji Njombe. ‎ ‎

Amesema kuwa k**a Bodi wanao wajibu wa kuendelea kujenga mahusiano mazuri baina ya Taasisi, wananchi, na wadau wa maendeleo kwa kuwa sehemu ya Utatuzi wa changamoto ambazo zinaweza kuwa kikwazo cha kukwamisha utoaji wa Huduma bora, mathalani amesema Bodi imeanza mazungumzo na wadau mbalimbali kuhakikisha wanachangia katika utekelezaji wa Bajeti ya Hospitali ili iweze kuwa Bajeti inayotekelezeka.

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe, Dkt. Gilbert Kwesi amesema utekelezaji wa Bajeti pendekezwa utakwenda kutatua changamoto mbalimbali katika utoaji huduma k**a vile;- uimarishwaji zaidi wa huduma za Kibingwa kwa kuongeza manunuzi ya vifaatiba vya kisasa, Malipo ya Motisha na Stahiki za watumishi, kuwajengea uwezo watumishi na kuwapeleka masomoni, ukarabati wa miundombinu na Upanuzi wa Huduma za Tiba na Huduma saidizi.

Kikao cha Maoteo ya Awali kuiendea Bajeti ya Hospitali, kimefanyika kwa siku nne kikihusisha wakuu wa Idara na Vitengo, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe.

ELIMU YA BIMA YA AFYA KWA WOTE NI ENDELEVU – DKT. MFANGAMganga Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Juma Mfanga amesema kuwa Elimu ya...
27/01/2026

ELIMU YA BIMA YA AFYA KWA WOTE NI ENDELEVU – DKT. MFANGA

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Juma Mfanga amesema kuwa Elimu ya Bima ya Afya kwa wote inapaswa kuwa endelevu ili kuleta matokeo yaliyokusudiwa na serikali.

Akizungumza jana jioni Januari 26, katika Kikao chake na Menejimenti ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe, amesema kuwa ipo haja kubwa ya Uongozi wa Hospitali kupitia wakuu wa Idara na vitengo, kuwafikishia watumishi walio chini yao Elimu ya Bima ya Afya kwa wote, ili kuendana na kasi ya Utekelezaji wa mpango huo ambao umeanza rasmi hapo jana.

Miongoni mwa sababu zilizotajwa kuchangia uanzishwaji wa Bima ya Afya kwa wote ni pamoja na kuwezesha malengo ya kisera, k**a vile kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi yaani vifo vya mama na mtoto, kutengeneza uwiano katika utoaji huduma kwa kujumuisha makundi maalumu k**a vile Watoto, wajawazito, wasio na uwezo, na wazee;Ujumuishaji wa huduma za magonjwa yanayochangia/kusababisha vifo na madhara makubwa ya kiafya kwa haraka.

Menejimenti ya Njombe RRH ilipitishwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo utekelezaji wa Sheria ya Bima ya Afya kwa wote,namna mifumo ya TEHAMA itakavyotakiwa kufanya kazi kuanzia Ngazi ya Afya ya Msingi hadi Taifa kwa kusisitiza kuwa mifumo hiyo lazima iboreshwe na ikiwezekana uwepo mfumo mmoja ambao utasaidia kusomana kwa Taarifa kuanzia Zahanati hadi Hospitali ya Taifa, ikiwa ni agizo la Waziri wa Afya, Mhe. Mohamed Mchengerwa,kuimarisha upatikanaji wa huduma bora za Afya; mfano upatikanaji wa dawa za kutosha, kuimarisha mifumo ya Tiba mtandao (Telemedicine) pamoja na utaratibu wa Rufaa.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe, Gilbert Kwesi amesisitiza wakuu wa Idara na Vitengo kushusha elimu hiyo kwa watumishi waliopo chini yao, pamoja na kuagiza Mratibu wa Mafunzo na Tafiti kuandaa kipindi ambacho kitasaidia kutoa elimu kwa watumishi wote kuhusu Bima ya Afya kwa wote.

Kupitia Bima ya Afya kwa wote Kaya yenye watu wasiozidi sita (6) wataweza kufaidika na huduma ya matibabu kwa gharama ya 150,000/= kwa mwaka.

Address

Mgodechi/Ramadhani Njombe Mjini
Njombe
59107

Telephone

+255678888654

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Njombe RRH posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to Njombe RRH:

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram