AFYA NI UHAI

AFYA NI UHAI health

AFYA YA UZAZI WA MWANAMKE (HORMONE IMBALANCE) " Suluhisho"Mvurugiko wa homoni za mwanamke ni kitendo cha kuongezeka au k...
27/01/2022

AFYA YA UZAZI WA MWANAMKE

(HORMONE IMBALANCE)
" Suluhisho"

Mvurugiko wa homoni za mwanamke ni kitendo cha kuongezeka au kupungua kwa vichochezi katika mwili wa mwanamke pale anapo pata hedhi, hivyo kufanya mwili kubadilika. Mvurugiko huo huathiri kila mwanamke kwa zaidi ya 80%. Asilimia kubwa ya wanawake mabadiliko huanza kati ya miaka 40 na 50, lakini pia kukosekana kwa usawa wa homoni huweza kuonekana mapema zaidi, kuanzia miaka 14.

Mabadiliko haya asilia hutokea wakati wa balehe, hedhi, ujauzito, kabla na baada ya ukomo wa hedhi. Mvurugiko wa homini kwa mwanamke huweza kuchangiwa kutokuwepo na usawa katika homoni zifuatazo Estrogen, Progesterone na Testosterone. Kupungua au kuzidi kwa homoni hizi kupelekea mvurugiko wa homoni kwa mwanamke.

VYANZO VYA MVURUGIKO WA HOMONI

Mvurugiko wa homoni ni tatizo linalowakumba wanawake wengi kwa sasa, hii ni kutokana na maisha wanayoishi, elimu finyu waliyonayo juu ya afya zao na kutokula kulingana na makundi ya damu. Vyanzo vya kuvurugika kwa homoni ni:
👉Uwepo wa sumu mwilini
👉Unbalanced Lifestyle (mfumo mbovu wa maisha)
👉Umri ukienda sana
👉Kukoma kwa hedhi
👉Kutofanya mazoezi, na kutokulala masaa anayostahili kwa siku
👉Uzito mkubwa
👉Mabadiliko ya mazingira au hali ya hewa
👉Msongo wa mawazo
👉Kula vyakula visivyo endana na Blood Group
👉Upungufu wa lishe mwilini
👉Matumizi ya njia za kisasa za uzazi wa mpango
👉Utoaji wa mimba
👉Family History (Upungufu au ongezeko ya homoni ya progesterone na Estrogen)
👉ongezeko ya homoni ya Androgen (Kuota ndevu, sauti k**a mwanaume)
Bara (Ethnicity): Wanawake wa Afrika wengi wana hili tatizo la ongezeko ya Homoni ya Estrogen, ndiyo maana wana maumbile makubwa

3. DALILI ZA MVURUGIKO WA HOMONl

Mfumo wa homoni ni muhimu sana kwa afya ya ubongo na mili yetu. Husaidia kuzuia magonjwa yasiyo ambukizi kadri umri unavyo songa mbele. Baadhi ya dalili zinazoweza kuonekana kwa mtu mwenye changamoto ya mvurugiko wa homoni ni k**a vile:

- Ukavu ukeni
- Maumivu wakati wa tendo la ndoa
- Kutoa jasho usiku
- Maumivu chini ya kitovu wakati wa hedhi
- Upungufu wa hamu ya tendo la ndoa
- Mabadiliko ya siku za hedhi na kupata hedhi kwa muda mrefu unaozidi siku 7. (heavy bleeding, au kujaza pedi moja kwa saa moja)
- Kukosa hedhi kwa muda mrefu, na kutoa damu yenye mabonge mabonge wakati wa hedhi
- Uchovu wa mara kwa mara
- Hasira za mara kwa mara
- Kukosa usingizi
- Homa za usiku na Kizunguzungu cha mara kwa mara
- Mzio wa vyakula (Allergie), kuchagua chagua vyakula
- Ongezeko ya tumbo na nyama uzembe
- Kuharibika kwa ngozi (chunusi, vipele… n.k)
- Maumivu ya viungo
- Upungufu wa nywele kichwani.
- Kusahau sana (kukosa kumbukumbu)
- Kupata hedhi wakati wa ujauzito (progesterone ikiwa imezidi)
- Kutokupata hedhi (balehe) adi umri wa miaka 20 na kuendelea
- Mwili kutokukua, kuonekana k**a binti mdogo, na kutokukua kwa via vya uzazi
- Msongo wa mawazo na kukosa kujiamini
- Kusinyaa na kupauka kwa ngozi wakati wa siku za hedhi na wakati wa utumiaji wa njia za uzazi wa mpango
- Maumivu ya kichwa mara kwa mara
- Kuwa na tabia ya hamaki (kukosa utulivu)
- Kutokupata choo kwa wakati
- Misuli hudondoka

4. MADHARA YA MVURUGIKO WA HOMONl

Pamoja na dalili nyingi tulizoziona tungependa wanawake waelewe vitu vifuatavyo hutokea iwapo atatumia njia za kisasa za uzazi wa mpango. Njia hizo husababisha saratani ya kizazi, CD4 kushuka, sehemu ya uke kuwa baridi, huchangia kwa 50% kufanyiwa upasuwaji (operation) wakati wa kujifungua, huathiri mtoto atakayezaliwa, huathri ubongo (inapunguza uwezo wa kufikiria), kutokwa na majimaji yenye harufu mbaya ukeni na magonjwa ya mara kwa mara.

Ukiendelea kubaki na dalili tajwa hapo awali kwa muda mrefu, kinga ya mwili itashuka kwa kiasi kikubwa na kusababisha madhara mengi k**a yafuatayo:

👉Kutoshika ujauzito kwa muda mrefu
👉Mimba kuharibika mara kwa mara;
👉Kukosa mtoto au Ugumba
👉Maumivu wakati wa tendo la ndoa
👉Kuwa na tabia na maumbile ya kiume
👉UTI (Urinary Tract Infection) ya mara kwa mara
👉Kuzeeka mapema
👉Kuziba kwa mirija ya uzazi
👉Saratani
👉Uvimbe kwenye uzazi wa mwanamke (Fibroids and Cysts)

Kwa ushauri na Tiba Wasiliana nasi; -WhatsApp 0769044226
- call 0782711079

*UGONJWA WA PID* (Pelvic Inflammatory Disease)au Maambukizi Katika Mfumo wa Uzazi waMwanamke.Magonjwa ya zinaa ndio saba...
07/01/2022

*UGONJWA WA PID* (Pelvic Inflammatory Disease)
au Maambukizi Katika Mfumo wa Uzazi wa
Mwanamke.
Magonjwa ya zinaa ndio sababu kuu ya
wanawake kupata maambukizi katika mfumo wa
uzazi yani (PID). Mwanamke 1 kati ya wanawake 8 walipota PID katika wakati wowote ndani ya maisha yao hupata tabu kushika mimba

*(PID) NI NINI?*
PID ni maambukizi katika mfumo wa uzazi wa
mwanamke na mara nyingi husababishwa na
magonjwa ya zinaa k**a gonorrhea na
chlamydia ila kuna aina ya maambukizi mbali na
magonjwa ya zinaa yanaweza kusababisha
maambukizi ya PID.

*JE! MWANAMKE HUAMBUKIZWAJE PID?*
Kuna njia kadhaa ambazo mwanamke anaweza
kuambukizwa PID. Njia hizo ni pamoja na:
- K**a una ugonjwa wa zinaa na haijatibiwa
- Kufanya ngono zembe isiyo salama (yani kulala
na wanaume tafauti tafauti)
- Kuwa na mpenzi ambaye ana wanawake wengi
nnje
- K**a umekuwepo na historia ya PID hapo
nyuma
- Maambukizi ya njia ya uzazi hasa kipindi mara
baada ya kujifungua (au postpartum period)
- Maambukizi ya njia ya uzazi mara baada ya
kutoa mimba kwa njia zisizo salama (post
abortion) au mara baada ya mimba kutoka
(miscarriage)
- Kutumia vipandikizi vya ndani ya mfuko wa
uzazi (IUCD) k**a njia mojawapo ya uzazi wa
mpango
- Kuambukizwa kupitia damu iliyo na vimelea vya
PID
- Kutumia (Vaginal Dauche)

*UTAJUAJE UKO NA (PID)?*
Zipo dalili kadhaa za ugonjwa huu wa PID.
Miongoni mwa dalili hizi ni:
- Mwanamke kuhisi maumivu ya tumbo hasa
maeneo ya chini ya kitovu
- Kupata maumivu ya mgongo
- Mwanamke kupata utoko mchafu sehemu za
siri. Utoko huu huambatana na harufu mbaya.
- Kuhisi maumivu wakati wa kukojoa
- Kupata maumivu au kutokwa na damu wakati
wa tendo la ndoa
- Kutoka damu bila mpangilio wakati wa hedhi
- Kupata homa
- Kupata damu innje ya siku zako zako za-
kawaida kupata damu ya hedhi
- Wakati fulani kuhisi kichefuchefu k**a
mwanamke mja mzito na kutapika

*VIPIMO VYA PID*
Hakuna vipimo maalum kudhibitisha mwanamke
ameathirika ila Dactari hujua mwanamke
ameathirika baada ya kuchukua historia ya
muhusika na kufanya vipimo vingine k**a:
- Kuchunguza mkojo ili kufahamu k**a mgonjwa
ana mimba. Kipimo hiki ni muhimu hasa kwa
mwanamke aliye katika umri wa kuzaa au
mwenye uwezo wa kubeba mimba
- Uchunguzi wa mkojo kwenye darubini ili
kutambua aina za vimelea vinavyomletea
mgonjwa uambukizi. Aidha mkojo huweza
kuoteshwa katika maabara kwa ajili ya kutambua
aina nyingine za vimelea viletavyo uambukizi huo.
- Kupima damu kwa ajili ya kuchunguza jinsi aina
mbalimbali za chembe za damu zilivyoathiriwa na
uambukizi huo au k**a kuna mwingiliano na
magonjwa mengine yaliyojificha. Kipimo hiki kwa
kitaalamu huitwa (Full Blood Picture).
- Kuchukua utando unaozunguka shingo ya uzazi
na kuuotesha kwa ajili ya utambuzi wa aina za
vimelea viletavyo maambukizi hayo. Kipimo hiki
huitwa (Cervical culture)
- Aidha ni muhimu pia kufanya vipimo vingine kwa
ajili ya utambuzi wa magonjwa yaambukizwayo
kwa njia ya kujamiiana, k**a vile virusi vya
ukimwi na kisonono.
- Mgonjwa pia anaweza kufanyiwa ultrasound ya
nyonga ili kuangalia k**a kuna athari yeyote
katika mfumo wake wa uzazi.

*JE PID INAWEZA KUTIBIWA?*
Jibu ni ndio k**a itagunduliwa mapema inaweza
kutibiwa na ikaisha, ila ieleweke k**a tayari
ilikuwa imeharibu njia za uzazi uharibifu ule
haiwezi kurekebishwa. Kila mara ukichelewesha
kutibu PID ndivyo itaharibu mfumo wako wote wa
uzazi sasa ni muhimu ukiona mojawapo wa dalili
nilizozitaja utembelee daktari ili upate tiba. Hata
k**a utatibiwa na zile dalili zikapotea hakikisha
kila mara unashauriana na daktari wako na
ukipata mume mwingine ni muhimu umueleze ili
mpate matibabu msi-ambukizane mara kwa
mara. Ijulikane k**a ulikuwa na PID awali
inaweza kurudi mara kwa mara.

*MATIBABU*
Mara mgonjwa anapogunduliwa kuwa
ameathiriwa na ugonjwa huu, dawa za jamii ya
antibayotiki huweza kutumika kwa ajili ya kuua
vimelea vya ugonjwa .
Ieleweke pia mara nyingi ugonjwa hujirudia mara
kwa mara k**a mwanamke atapewa tiba na
mume asitibiwe. Na k**a maambukizi imekuwa
sugu inabidi muathiriwa amueleze daktari ili
apate kutumia anti-biotics kwa mda mrefu kuliko
kawaida. Lakini muhimu sana mwanaume apewe
dawa wakati mwanamke anatibiwa. Ikiwa
mwanamke peke yake atapata tiba pindi atakapo
lala na mwanaume yule yule maambukizi
yatarejelea.
*MADHARA YAKUTO-FWATA MATIBABU*
- Maumivu ya mfuko wa uzazi wakudumu
- Utapata ugumu wa kushika mimba
- Ectopic pregnancy (mtoto kuwa innje ya mfuko
wa uzazi)
- Kuziba kwa njia ya uzazi

*JINSI YA KUZUIA MAAMBUKIZI*
Kuna njia kadhaa za kuzuia maambukizi katika
mfumo wa uzazi. Njia hizi ni pamoja na:
- Njia hakiki ya kujizuia na maambukizi haya ni
kuwacha ngono zembe na kufanya ngono salama
- Kuwahi kuwaona wataalamu wa afya mara dalili
za ugonjwa huu zinapoanza kujitokeza au pindi tu
unapogundua kuwa mwenzi wako ana dalili za
magonjwa ya zinaa au anatembea na wanawake
wengine
- Kufanya vipimo mara kwa mara hasa vya
mfumo wa uzazi, pamoja na vipimo vya
maambukizi ya magonjwa yanayosambazwa kwa
njia ya ngono (STI) khususan ugonjwa wa
chlamydia ufanyie vipimo kila mwaka mara 1
- Kutofanya ngono mara baada ya kujifungua,
mimba kutoka au mara baada ya kutoa mimba ili
kuhakikisha njia ya shingo ya uzazi imefunga
vema.
Ahsante.

Kwa ushauri zaidi na Tiba wasiliana nasi;
- WhatsApp 0769044226
- call 0782711079

Address

Tanga

Telephone

+255769044226

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when AFYA NI UHAI posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram