26/07/2025
Leo tumefanya kikao cha kupanga tathmini ya mahitaji kwa ajili ya mradi wa ‘Focus on Youth, Not the Substance.’ chini ya Programu ya TangaYetu. Kikao kimewahusisha waelimishaji rika, viongozi wa jamii, wakufunzi, HR, Afisa Vijana wa Halmashauri ya Jiji la Tanga, pamoja na Dkt. Isack Rugemalila kutoka Wizara ya Afya. Tunalenga kuwafikia watu 1,000+ Jijini Tanga ili kubaini mahitaji ya jamii na kupunguza matumizi ya dawa za kulevya miongoni mwa vijana. DCEA