13/08/2025
Habari samahani naombeni ushauri, hapa nilipofikia naona nimefika mwisho kabisa nahitaji akili mpya kuvuka hapa, mimi nilioa mwanamke miaka minne iliyopita, alikuwa mwanamke mzuri tu, mpole na mstaarabu, na kwa bahati nzuri nilienda kuoa nyumbani kwetu, tulifunga ndoa halali kabisa na nashukuru nilimkuta na usichana wake, kwa hilo nampongeza sana.
Ninaishi Ukonga Dar es salaam kwa sasa, mwanzo ndoa yetu ilikuwa na amani lakini baada ya miaka miwili mwanamke alianza kubadirika, akawa hanisikilizi tena, ninachomkataza anakuwa mkaidi na mbishi, akawa anatoka sana nyumbani nikijaribu kumzuia anasema mimi ni mnyanyasaji, ikabidi niwe natumia kufosi akikataa namuadhibu kwa viboko au makofi.
Akanishtaki kwao na kwetu kuwa mimi nampiga namuonea na mambo mengi, nilipojaribu kuwaelewesha sababu walinioinga na kusema sipaswi kumpiga no matter what.
Basi kile kitendo kiliniuzi sana na sikufatilia nikamwambia lazima uniheshimu na kunitii kinyume na hapo lazima uchezee kichapo, wao wana ndoa zao na sisi hii ni ndoa yetu, kilq mmoja apambane na ndoa yake,
Nimejaribu kukuonya kwa mdomo lakini hukuwahi kunisikia je ulitaka nifanyeje? Nikuache tu mpaka siku utakapokunya kwenye sahani? Mwanamke akawa anagomba tu, maneno yanamtoka, anaweza kuongea kuanzia asubuhi mpaka jioni bila kuchoka.
Nikawa najiuliza hivi nimeoa sabufa au nimeoa binaadamu?.
Yote tisa ila tabia yake ya kuongea sana ndio ilikuwa no.1 katika tabia zote ambazo nilikuwa sizipendi, yaani anaongea wakati wote mpaka muda wa kulala, ile hali ilininyima amani kwa kiasi kikubwa sana, ikapelekea mpaka ninaporudi kazini nitafute pa kwenda angalau muda usogee sogee ndio nirudi nyumbani, na nilikuwa najitahidi kuondoka kabla hajaamka, nikaona k**a ile ndoa inaniboa, nikaona k**a niko kifungoni ndani ya nyumba yangu mwenyewe!.
Nikaja kugundua kumbe ana marafiki/shoga zake ndio wanamshauri vibaya na kumuharibu akili, ikabidi nikomae na hao shoga zake, nikamzuia katu katu asiwe na uhusiano nao, lakini kwakuwa sishindi nyumbani juhudi hazikuzaa matunda.
Wale shoga zake wakamwambia eti mimi nina mchepuko ndio maana namtesa, yaani walimwambia kuwa ninamtesa kwasababu tu ya kumzuia ukaribu nao, kumzuia tabia za kiburi na mdomo mrefu, kumzuia kutoka nyumbani bila uwepo wangu au ruhusa yangu, wakamwambia mengi, kwamba mimi ni mkoloni n.k
Ilifika time akajifungua mtoto, muda wote nyumba ilikuwa inajaa watu na wengine siwafahamu, kila nikitoka nikirudi nakuta makelele wanawake wanacheka sauti ya juu kisha wanagonga mikono.
Nikawa nakaa kimya tu nisionekane mbaya, kumbe baadhi yao ndio walikuwa wanamtafutia mabwana.
Niligundua hilo siku moja ambapo nilimkuta anaongea na simu na baada ya kusikia anaongea nilijificha, nikasimama mlangoni, sikusikia vizuri alichokuwa anaongea ila kuna maneno kadhaa yalinipa mashaka.
Nikafungua mlango ghafla na kuingia kabla hata ya salamu nikamwambia leta hiyo simu, akagoma kunipa, nilimtandika kibao kimoja mpaka nikasikia mkono unawasha, simu ikaanguka nikaichukua, kufungua hivi nakuta namba haina jina.
Kuchukua ile namba kupiga naambiwa namba hii haipo, nilichoka! Ikabidi nimuite yeye mwenyewe nikamwambia piga namba hii mbona naona hapa kwenye call log mmeongea dakika 3 halafu napiga namba hii hii naambiwa haipo, akajibu yeye hajui.
Kwa hasira nilizokuwa nazo, nilitaka kila kitu kiwe wazi, nikatoa laini nyingine ya tigo ambayo huwa siitumii sana nikaweka kwenye simu nikainunulia salio nikaanza kupiga ile namba lakini niliambiwa 'Namba hii haipo", nilishangaa sana, kivipi haipo na wakati ndio namba inayoonekana kwenye simu ya mke wangu? Ikabidi nichukue simu ya mke wangu nipige mwenyewe, ile namba iliita kwenye simu ya mke wangu na huyo mtu alipokea, nikaa kimya akaanza kuongea Haloo halooo sauti ni ya kiume, nikakata, nikapiga tena kwangu ila naambiwa namba hii haipo.
Nilipanga nitampigia huyo mtu kwa baadae, nikaenda kuoga nikala chakula, nikaenda chumbani kulala kwanza kupumzisha akili.
Simu sikumrudishia mke wangu, ilibidi nimpokonye simu kwa uchunguzi zaidi, ziliingia meseji nyingi za kipuuzi kutoka kwa mashoga zake nikawa nasoma napuuzia tu, nikapitia chatting nyingi, nilipoingia whatsapp nikakuta sms "Mbona unapiga hauongei baby au hiyo ng'ombe yako imesharudi?" Nilihisi ubongo umehama sehemu yake, nilipanic mpaka nikashindwa kulala, nilikataa nawaza kumkata mtu k**a slice za mkate, ila nikajituliza akili.
Niliview profile nikaona namba mbili tofauti, yaani ile unabonyeza profile ya mtu ili uone picha, namba, na bio yake, mimi niliona namba ziko mbili tofauti, ndio nikagundua kwanini ile namba nilipokuwa nikipiga naambiwa namba hii haipo.
Kumbe mke wangu alichukua namba ya bwana wake na wakati wa kui-save sehemu ya kuweka jina la muhusika aliweka namba nyingine ambayo haipatikani yaani badala ya kuandika Juma anaandika 0765*******, kwahiyo ukiona inaita utachukua hii namba inayoonekana k**a jina kumbe ni trick tu 😭😭😭, alifanikiwa kunigeuza mjinga.
Ili kufupisha stori ni kwamba nilijiridhisha kuwa anatembea na yule jamaa, nilichofanya nilimwambia jamaa amchukue mke wangu amuoe maana naona wamependana sana, siwezi kuendelea na mwanamke ambaye yuko kwenye upendo na mwanaume mwingine. Mi nikamchunia mazima, mke wangu alivyokuwa mjinga akanisusia mtoto akiwa na miezi 9, akimaanisha kuwa itashindwa kumlea hivyo nitalazimika kumrudisha.
Alipofanya hivyo nikasema huyu mwanamke hanijui kumbe, wiki hiyo hiyo nikahama nilipokuwa nakaa nikahamia pengine japo kodi ilikuwa bado ipo ya miezi k**a minne hivi, sikujali hilo, nikaondoka, nikatafuta housegirl ambaye alikuwa mmama mtu mzima, nikamchukua na mdogo wangu wa k**e nikaishi nao wakinilelea mwanangu, mpaka amekuwa hivi alivyo yule mwanamke alinisumbua sana kuomba msamaha, mameseji masimu, nikaamua kubadirisha namba.
Kuna sehemu nikikuwa najenga nyumba imekamilika mwaka huu mwenzi wa pili na tulishahamia ndio tunaishi hapa kwa sasa, sijui nani alimuomesha, mwezi wa 6 alikuja kunipiga goti nimsamehe kuwa atajirekebisha nikamwambia siwezi tena acha kujipendekeza kwangu sikutaki.
Sasa hivi amekuja na mbinu mpya kwamba anamtaka mwanae, nimpe mwanae la sivyo atanishtaki na nitashindwa kwa mujibu wa sheria.
Hivi huyu mwanamke anaweza kushinda kesi na kumchukua mtoto? Wakati alimtelekeza mwenyewe? Na je nitumie mbinu gani ili akate tamaa na maisha yangu na mwanangu, yaani simpendi hata kumuona tu, nikimuona au kumsikia moyo unaishiwa nguvu hapo hapo, nisaidieni ni ananikera to the maximum.