13/11/2025
"Ni takribani week 2 sasa tangu nimpoteza mwanangu miaka 12 tu ..Alipigwa risasi siku ya uchaguzi tarehe 29 .. Nakumbuka siku hio tulikua ndani tukasikia milio ya risasi watu wakitawanywa wasiandamane basi ..Kwa bahati mbaya mtoto wangu alienda dirishani kuchungulia na yeye Alipigwa risasi hapo hapo..nilimkimbiza hospital lakini siku ya pili alipoteza maisha .. Kamwe siwezi kusahau polisi kitu walichomtendea mwanangu .hakua na hatia alikua ndani .. Pamoja na yote namuombea aendelee kupumzika Kwa amani 💔 Rip mwanangu Inna Lillahi wa inna ilayhi raji'un"