Dr. Abounabil

Dr. Abounabil There's nothing more important than our good health. That's our principal capital asset......

KUPIGA PUNYETO KWA MUDA MREFU, MADHARA NA TIBA YAKE:Kupiga punyeto kwa muda mrefu ni moja kati ya vyanzo vikuu vya tatiz...
10/03/2020

KUPIGA PUNYETO KWA MUDA MREFU, MADHARA NA TIBA YAKE:

Kupiga punyeto kwa muda mrefu ni moja kati ya vyanzo vikuu vya tatizo la la ukosefu wa nguvu za kiume. Asilimia kubwa ya vijana wenye tatizo la ukosefu wa nguvu za kiume, linasababishwa na upigaji wa punyeto kwa muda mrefu.

JINSI PUNYETO INAVYO SABABISHA UKOSEFU WA NGUVU ZA KIUME.

Unapopiga punyeto unakuwa unaiminya mishipa ya uume ambayo ndio inaufanya uume usimame. Matokeo yake unaifanya mishipa hiyo ilegee na kutokuwa na uwezo wa kusimama tena. Mishipa ya uume iliyo legea kutokana na upigaji punyeto, huleta madhara yafuatayo :

Huondoa uwezo wa mishipa ya uume kurelax. (Unapopata wazo la kufanya tendo la ndoa, mishipa ya uume ina relax , mishipa iki relax husababisha mishipa ya ateri kupanuka na kuruhusu damu kingie ndani ya mishipa ya uume na hatimaye kuufanya uume usimame na kuwa mgumu)
Mishipa ya kiume ikishindwa ku relax husababisha mishipa ya ateri kuziba
Mishipa ya ateri ikiziba, damu haiwezi kutiririka kuingia kwenye mishipa ya uume, na hata ikitokea damu imeingia ndani ya mishipa ya uume basi huingia kiasi kidogo sana tena kwa presha ndogo sana hivyo basi hata k**a uume utasimama basi utasimama ukiwa legelege sana

Mishipa ya uume ikishindwa kurelax basi haitakuwa na uwezo wa kuipush na kuiziba mishipa ya vena ambayo ndio hunyonya damu kutoka kwenye mishipa ya uume ulio simama. Matokeo yake basi, damu kidogo iliyo ingia ndani ya mishipa ya uume na kuufanya uume kusimama, hunyonywa na kutolewa nje ya mishipa ya uume ndani ya sekunde chache sana na hivyo kuufanya uume usinyae ndani ya muda mfupi sana.
Mishipaya uume kulegea
Uumekurudi ndani na kusinyaa na kuwa k**a uume wa mtoto
Tatizo la unene kupita kiasi : Tatizo la unene na uzito kupita kiasi ni miongoni mwa mambo yanayo sababisha upungufu wa nguvu za kiume. Unene kupita kiasi humuweka mtu katika hatari ya kupatwa na magonjwa k**a vile kisukari, presha, moyo na shinikizo kuu la damu. Na magonjwa ya kisukari, moyo,presha na shinikizo la damu husababisha upungufu na ukosefu wa nguvu za kiume, na hivyo kumuweka muhusika katika hatari kuu ya kupatwa na tatizo la ukosefu/upungufu wa nguvu za kiume.
Hivyo basi kwa wewe mwenye tatizo la unene na uzito kupita kiasi , pamoja na kutumia tiba ya nguvu za kiume, ni vyema ukafanya na mpango wa kupunguza unene na uzito wako.

Matatizo Katika mfumo wa Ubongo
Uume hauwezi kusimama bila ya kuwa na ushirikiano na ubongo. Ili mtu uume uweze kusimama, mtu lazima apate wazo la kufanya tendo la ndoa (UBONGO UNA HUSIKA HAPO ), akishapata wazo, ubungo hupeleka ishara kwenye mishipa ya fahamu iliyopo katika uti wa mgongo ambayo nayo hupeleka taarifa kwenye mishipa ya uume then uume usimama. Hivyo basi ili mtu aweze kuwa na uwezo wa kusimamisha uume wake ni lazima kuwa na mawasiliano mazuri na imara kati ya mishipa ya fahamu (ubongo), mishipa ya kwenye uti wa mgongo na mishipa ya kwenye uume. Bila ushirikiano kati ya vitu hivyo vitatu, uume hauwezi kusimama.

Magonjwa yanayoweza kuathiri ushirikiano kati ya mishipa ya ubongo na mishipa ya uume, yanaweza kusababisha kushindwa kusimama kwa uume.

Magonjwa hayo ni pamoja na kiharusi,kupoteza kumbukumbu (Alzheimer), multiple sclerosis pamoja na ugonjwa wa Parkinson.

Ni vyema mgonjwa akatibiwa kwanza magonjwa hayo kabla ya kuanza kutumia dawa ya nguvu za kiume. Kufahamu jinsi ya kujitibu magonjwa tajwa hapo juu kwa njia asilia,tafadhali tembelea

Mambo mengine yanayo sababisha ukosefu na upungufu wa nguvu za kiume, ni pamoja na maumivu & majeraha kwenye uti wa mgongo, chango la kiume , ngiri na matatizo katika homoni.

VIASHRIA VYA MTU MWENYE TATIZO LA UKOSEFU/UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME.

Mtu mwenye tatizo la ukosefu wa nguvu za kiume huwa na dalili zifuatazo ;

Kushindwa kabisa kusimamisha uume wake
Uume kusimama ukiwa legelege
Kuwahi kumaliza tendo la ndoa
Mwanaume kutokuwa na uwezo wa kufanya tendo la ndoa katika baadhi ya staili (Mara nyingi mwanaume huyu huwa na uwezo wa kufanya tendo la ndoa staili moja tu). Hapa mwanaume anakuwa na uwezo wa kufanya tendo la ndoa kwa staili ya “ missionary” pekee. Ikibadilishwa staili, mwanaume anakuwa hana tena uwezo wa kusimamisha uume wake japo katika hali ya u lege lege
Uumekuto kuwa na uwezo wa kusimama wenyewe bila kushikwashikwa ama kutomaswa kwa muda mrefu.
Uume kusinyaa ukiwa ndani ya mwanamke.
Uume kusinyaa, pindi inapotokea activity yoyote ya kiungo ama ogani nyingine ya mwanaume wakati wa tendo la ndoa. Kwa mfano, wakati wa tendo la ndoa, ikitokea mwanaume amekohoa au kupiga chafya, uume nao unasinyaa.
Uume kusinyaa mara tu baada ya kutolewa ndani ya uke (Kwa mfano k**a unafanya tendo la ndoa, halafu uume ukatoka nje, kitendo cha kuushika kuurudisha ndani, tayari unasinyaa)
Kutokuwa na uwezo wa kurudia tendo la ndoa.
Kupatwa na maumivu wakati wa tendo la ndoa.

VIASHIRIA VYA MWANAUME ASIYE NA TATIZO LA UKOSEFU WA NGUVU ZA KIUME.

Mwanaume asiye na tatizo la ukosefu wa nguvu za kiume, huonyesha ishara zifuatazo ;

Uume husimama ukiwa imara k**a msumari.
Hukaa kifuani kwa muda mrefu (Wastani ni kati ya dakika 20 hadi 45)
Huweza kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara tatu bila misuli ya uume kuchoka.
Huweza kufanya tendo la ndoa kwa staili yoyote ile.
Uume husimama wenyewe bila kushikwa shikwa wala kuwa stimulated kwa namna yoyote ile
Kwa ufupi anakuwa na uwezo wa kufanya na kukamilisha tendo la ndoa kwa uukamilifu mkubwa

Altabib Hijama Centre and Natural Therapy tumekuletea tiba ya uhakika ya asili isiyo na madhara kwa matumizi ya mwanadamu.
Kwa wale wote wenye matatizo ya kusinyaa kwa uume au kuwa lege lege au kitosimamisha kabisa, hii ni kwa ajili yao.
Dawa maalum ya kuchua dhakar iliyolegea na kuifanya iwe imara Na kusimama k**a msumari Na kufanya damu itiririke vyema kwenye uume Na kukufanya upate hamu zaidi ya tendo Na kurudia zaidi ya mara tatu ikiwa bado imesimama Na kufurahia ladha ya tendo.

Kuipata dawa hii piga simu namba 0778633366

02/03/2020

MIMBA KUHARIBIKA CHANZO NA SABABU, DALILI NA NINI UFANYE ILI KUZUIA ISITOKEE TENA

Somo hili ni refu na kwa hiyo limegawanyika sehemu kuu tatu
1- Dalili za mimba kuelekea kuharibikiwa
2- Chanzo na sababu za mimba kuharibika
3- Nini cha kufanya ikiwa huwa unapatwa na hali hiyo mara kwa mara.

SEHEMU YA KWANZA

Ni kawaida sana mimba kutoka au kuharibika bila kukusudia au bila wewe kujua k**a imetoka au inakaribia kutoka. Wakati mwingine hutoka tu bila sababu yeyote na hata k**a utapimwa na vifaa vya kisasa kabisa bado sababu za mimba kuharibika hazitajulikana. Ikiwa utajua ya kwamba mimba imetoka
CHAKWANZA ni vizuri kujua sababu ya mimba hiyo kutoka, hasa k**a imeharibika kwa mara ya pili na zaidi. Sababu zinaweza kuwa nyingi k**a vile utakavyo ona katika hatua zifuatazo hapo chini, kuna sababu za kijamii na kiafya. Sababu za kijamii zitafutiwe ufumbuzi kijamii, mfano mtu amelaaniwa (hapo k**a una amini katika dini) huwezi tena kupona kwa kutumia dawa, lazima ufunguliwe na kifungo hicho kwanza.
CHA PILI kupambana na icho kisababishi, baada ya kupima na kupata ushauri basi itakufaa sasa upate dawa au kufuata ushauri uliopewa, ukimaliza dozi rudi hospitalini kituo cha afya ili uweze kujua k**a umepona kabisa au la. Kunayo tabia ya watu wengi tu akisha maliza dozi ndio inakuwa basi anaendelea na Maisha yake, hapo unakuwa unakosea. Jitahidi kurudi hospital na kupima tena upate uhakika wa tatizo k**a limeisha au la. K**a halijaisha inakuwa rahisi kwa daktari kuchua vipimo vingine au kukupa dawa ingine.
CHA MWISHO ni kujaribu tena kubeba mimba, baada ya kuona mambo yote yako sawa, au sasa unaamini uko vizuri basi unajaribu tena kupata mimba. Zingatia siku zako za uzazi, na zingatia kupika vyakula vizuri ili mume wako apate nguvu ya kutoa mbegu nyingi na zenye afya njema. Usafi pia wa mwili na kitanda ni muhimu. Usinuke na kutoa harufu mbaya.
Mara nyingi swala la kwanza na pili watu huruka na kuendelea nakutafuta mimba. Zaman wakati vifaa na wataalamu walikuwa hakuna hiyo ilikuwa sawa lakini Siku hizi kuna vifaa ujitahid kutafuta sababu. Hii ni Kwa sababu pia uwezo wa wanawake kuzaa umepungua sana. Wanawake wachache wanazaa watoto zaid ya 6 hata wakitaka kuzaa wanajikuta hawawezi. Wengine wanachelewa kuolewa, kwa mana hiyo wanaanza kutafuta watoto wakati Mayai bora mengi yameishaisha.

DALILI ZA MIMBA CHANGA KUWA IMEHARIBIKA AU KWAMBA INAELEKEA KUHARIBIKA

Kwahiyo ukiona dalili zifuatazo basi jua mimba yako changa imetoka au inataka kutoka kimyakimya.
1- maumivu makali ya tumbo la uzazi (yanachoma)
2- kutoka uchafu k**a ugoro au damu ya bleed au mabonge ya damu.
3- kutoka na kitu k**a kinyama lakini chenye damu.
Note: unaweza tokwa na damu k**a matone hiyo inaweza isiwe mimba imetoka. Jaribu kupima tena na tena. Usipime Siku iyoiyo Kwa kuwa Homoni za mimba zinakuwa Bado zipo.
Cha msingi pia ni kupata ushauri ukikutwa na hali hiyo. K**a ulikuwa unajua una mimba basi dalili zifuatazo ni hatari na lazima zikupatapo uwahi hospital.
1- maumivu makali ya tumbo kichwa na mgongo wachini kwa pamoja au mara moja moja.
2- Mafua makali, kutapika sana, kuishiwa maji mwilini na kikohozi.
3- kupata damu ya bleed lakin yenye rangi tofauti na ya bleed.
4- kutokwa na uchafu unaomiminika kidogokidogo kutoka ukeni.
5- kupungua Kwa dalili za mimba, kujisikia kawaida na k**a imeharibika dalili zinakoma kabisa
Upatapo hizo dalili wahi kupata tiba hasa kupitia bidhaa bora kabisa na zenye uhakika tena kwa haraka. unaweza pata msaada.

Kwa msaada wa Tiba hizi Na magonjwa mengine mbalimbali
Wasiliana nasi kwa Whatsapp au piga simu namba 0778633366

Najua kuna watu wengi wamehangaika sana Na matatizo yanayosababishwa Na uzito pamoja Na unene uliopitiliza.Usikate tamaa...
01/03/2020

Najua kuna watu wengi wamehangaika sana Na matatizo yanayosababishwa Na uzito pamoja Na unene uliopitiliza.
Usikate tamaa maana matatizo yote yanatibika Na kuisha kabisa endapo utapata Tiba sahihi.

Karibu tukuhudumie.
Kwa maelezo zaidi piga au whatsapp
+255 778 633366

07/04/2019
19/03/2019

DALILI ZA VIDONDA VYA TUMBO:

Gesi tumboni.
Kiungulia.
Maumivu ya tumbo.
Choo kuwa kigumu na kutoka k**a cha mbuzi.
Maumivu ya chembe ya moyo.
Maumivu ya mgongo.
Kupata choo laini sana.
Chembe cha moyo kuwaka moto pindi unapokawia kula.
Kuchoka choka ovyo na uvivu uliopitiliza.
Ganzi.
Kuumwa kichwa.
Kukosa hamu ya kula.
Kukosa usingizi au kuwa na usingizi kupita kiasi.
Hasira.
Kukosa hamu ya mapenzi na kupoteza nguvu za kiume.
Msongo wa mawazo na kupoteza kumbu kumbu.

Kumbuka ukiwa ukiwa na dalili moja wapo k**a hii, usitumie vyakula k**a:-
Dagaa wadogo.
Maharage na jamii zote za kunde.
Karanga na maganda yake.
Nyanya zenye maganda na mbegu zake.
Maziwa mtindi.
Ndizi.
Pilipili.
Ukali wa aina yoyote.
Nyama nyekundu.
Soda.
Pombe.
Sigara.
Mafuta ya wanyama.
Kahawa.
Chipsi.
Mahindi.

Kumbuka vidonda vya tumbo vinatibika kabisa kwa kutumia dawa zitokanazo na mimea na matunda.
Wasiliana nasi

0778 633366
Ushauri bureeeee

Angalizo:
Si kila dalili miongini mwa dalili hizo ni lazima iwe ni vidonda vya tumbo
Vipimo pia vipe nafasi yake.

FAIDA ZA KITUNGUU MAJI KATIKA MWILIKitunguumaji ni aina ya mboga ya yungiyungi.Ni mboga yenye harufu kali inayochangamsh...
27/02/2019

FAIDA ZA KITUNGUU MAJI KATIKA MWILI

Kitunguumaji ni aina ya mboga ya yungiyungi.

Ni mboga yenye harufu kali inayochangamsha.

Kitunguu kimethibitikakisayansi kuwa na manufaa makubwa sana katika afya
ya mwanadamu.



Zifuatazo ni faida za kiafya zakitunguu maji.

1. Juisi ya Kitunguu Huua vijidudu vya
kifua kikuu.

Tafiti mbalimbali za kisayansizimethibitisha
kuwa juisi yakitunguu ina uwezo wa kuua vijidudu vinavyosababishamaradhi ya kifua-kikuu(Huua baada tu ya mgonjwa kunusa moshi wake)

2. Kitunguu maji huongeza hamu ya kula.

Kitunguu maji kikifanyiwa kuwa achari, ukali wake hupungua huongeza mno hamu ya kula.

2. Huupa mwili nishati na nguvu

Kitunguu maji kikiliwa kikiwa kimechomwa, huongeza nguvu na nishati mwilini na huimarisha misuli ya mwili.

3. Huufanya uso kunawiri

Kitunguu maji kikichomwa na kasha kuliwa huufanya uso kuwa mweupe, mn’gavu na wenye kunawiri.

4. Kitunguu maji huongeza hamu ya kula



5. Kitunguu husaidia kulainisha tumbo



6. Kitunguu husaidia kutibu tatizo la
kukosa haja kubwa



7. Kitunguu maji kikipikwa na kuliwa
pamoja na samli , husaidia kuongeza nguvu za kiume pamoja na kuboresha nguvu za kiume.



8. Kitunguu kikitengenezwa supu pamoja na nyama, huongeza hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake.



9. Kitunguu maji husaidiakutibu homa ya manjano.



10. Kitunguu maji husaidiakuvunja vijiwe tumboni



11.Kitunguu maji hutumika kutibu tatizo la kukosa hedhi kwa wanawake



12.Kitunguu maji kina utajiri wa Vitamini C ambayo husaidia kuzuia kukua kwa bacteria kwenye jeraha na kuongeza nishati kwenye mbegu za
kiume.



13.Kitunguu maji kina madiniya salfa,chuma
na vitaminambayo husaidia kutia nguvu
kwenye mishipa



14.Kitunguu maji husaidiakuwatibu wagonjwa wakisukari.



15.Kitunguu maji husaidiakutibu maradhi ya moyopamoja na kuimarisha mfumowa
mzunguko wa damu mwilini.



16.Kitunguu majikimethibitika kuwa vijiuasumu vyenye nguvu zaidi kuliko penesilini(penicillin)kwa hivyo hupoza kifuakikuu,kaswende(syphillis)na kisonono(gonorrhea),pamojana kuua vijidudu vingi vya hatari.



17. Hutibu tatizo la Pumu:
Kitunguu maji kikitumika pamoja na asali, husaidia kutibu tatizo la pumu.



17. Husaidia kutibu tatizo la Uvimbe wa pafu (Pneumonia )



18. Kituu maji husaidia kutibu tatizo la Saratani za aina mbalimbali.(Cancer):

19. Kitunguu maji husaidia kutibu vidonda
ndugu.

20. Kitunguu maji husaidia kutibu tatizo la
mvilio wa damu

21. Kitunguu maji husaidia kutibu majipu

22. Husaidia kutibu tatizo la Chunusi:

23. Husaidia kuondoa tatizo la Ukurutu (Eczema) kwenye ngozi.

24. Husaidia kutibu Saratani ya ngozi.

25. Husaidia kutibu matatizo ya figo.

26. Husaidia kutibu tatizo la Kikohozi kwa wakubwa na wadogo

27. Husaidia kutibu maradhi ya macho:
Kikohozi:

28. Husaidia kupunguza uzito wa mwili.

Kwa ushauri na tiba mbali mbali za magonjwa yanamsibu binadamu wasiliana nasi kwa simu au whatsapp 0778 633366

26/08/2018

Madhara ya kubana mkojo kwa muda mrefu
Thread starterreal G Start dateSep 4, 2017
real G
Real G
JF-Expert Member
Sep 4, 2017
#1
Watu wengi huvumilia mkojo kwa muda mrefu kutokana na sababu mbalimbali. Baadhi wanaweza wakawa katika eneo ambalo hawezi kwenda haja ndogo lakini wengine ni uzembe ambapo wengi utakuta anaangalia tamthilia hivyo hataki apitwe, au anaona akienda haja ndogo hadi arudi umbea unaopigwa utampita na hivyo anaamua kubana mkojo, hayo yote yana madhara kwa mwili wako.

Je! Wewe hukojoa mara ngapi kwa siku? Mbili?, Tatu? Tano? Kwa mujibu wa watalaamu mbalimbali, wamesema kuwa kila mtu anatakiwa kukojoa kila baada ya saa 4 hadi 6, lakini k**a utashikilia mkojo wako kwa muda zaidi, utakuwa uanajiweka kwenye hatari ya kukumbwa na matatizo mbalimbali.

Haya ni baadhi ya madhara yatakayokupata endapo utabana mkojo kwa muda mrefu zaidi;

1. Kujikojolea

Kwa mujibu wa Daktari Lauren Streicher akifafanunua hili alisema kwamba, mtu anapaswa kufikiria kibofu chake k**a p**o ambalo limejazwa maji kupitiliza. P**o hilo likatanuka hadi mwisho wake na kuwa zito, kadiri utakavyokuwa unazidi kuubana, ndivyo itakavyokuwa vigumu kwako wewe kutembea hadi chooni kabla hujajikojolea.

Itakuwa ni aibu kwa mwanamke mtu mzima kujikojolea eti kwa sababu hakwenda chooni kwa kunogewa na muvi au umbea ambapo pengine hauna faida.

2. Kulegea kwa misuli ya Pelvic

Misuli ya Pelvic hutumika katika kuzuia mkojo usitokea au kuuruhusu utoke katika kibofu cha mkono. Ukiwa na tabia ya kubana mkono kwa muda mrefu sana, misuli hii itachoka na hivyo kuacha kufanyakazi kwa usahihi. Hilo linapotokea unashindwa kuzuia tena mkojo wako sababu misuli imelegea na hivyo mkojo ukija unapita moja kwa moja.

Hivyo, epuka kuharibu misuli hiyo kwa kubana mkojo kwa vitu ambavyo sio vya msingi. Kila unapohisi mkojo nenda kakojoe kisha rudi, endelea na ulichokuwa unafanya.

3. Maumivu

Kwa kawaida unaposhikilia mkojo kwenye kibofu kwa muda mrefu, unapatwa na maumivu makali, lakini maumivu hayo hutokomea mara tu unapokwenda haja ndogo. Maumivu hayo yanaweza yakawa ni mfumo wako wa maisha k**a hutachukua tahadhari mapema.

Waswahili husema kuwa, tabia hujenga mazoea, na hivyo ndivyo itakavyokuwa kwa misuli ya mwili wako, ukizoea kubana mkojo kila mara, itakua ikiima kila mara.

4. Kutanuka kibofu

Basi tusema kwamba ukibana mkojo kwa muda mrefu, kibofu chako kinaweza kisipasuke kutokana na wingi wa mkojo lakini kikatanuka kuliko ukubwa wake unaotakiwa.

Tatizo la kutanuka kwa kibofu kutokana na kubana mkojo mara kwa mara ni kwamba mwili wako utakuwa haukupi taarifa kuwa unatakiwa kwenda kujisaidia. Hii ni kwa sababu umbo la kibofu limeongezeka. Taarifa hizo ambazo hutolewa na ubongo wakati kibofu kimejaa ni muhimu sana, lakini kibofu kikitanuka hutozipata.

Ni kweli wakati mwingine unaweza ukabanwa na mkojo na kuwa sehemu ambayo huweza kupata msaada ya kujisaidia, lakini epuka tabia hii kuwa mazoea.

Chanzo: Swahili Times

25/04/2017

TATIZO LA MIMBA KUTUNGA NJE YA MFUKO WA UZAZI (ECTOPIC PREGNANCY).. MPadmire

Mimba kutunga nje ya mfuko wa uzazi wa mwanamke au ectopic pregnancy ni tatizo ambalo limetokea kuathiri wanawake mbalimbali. Kwa kawaida, isipokuwa mara chache sana, mimba zitungazo nje ya mfuko wa uzazi hazina uwezo wa kukua kuwa mtoto kamili. Aidha, mimba hizi ni hatari kwa afya ya mama mjamzito kwa vile humfanya kupoteza damu nyingi na hatimaye kusababisha kifo.

Nini hutokea?

Kazi za mirija ya fallopian ni kusafirisha mayai kutoka katika kiwanda chake cha uzalishaji (o***y) mpaka kwenye mfuko wa uzazi (uterus). Utungisho wa yai la k**e (o**m) na mbegu ya kiume (s***m) hufanyika kwenye mirija hii.

Mara baada ya utungisho, misuli inayozunguka mirija ya fallopian ikishirikiana na vinyweleo vilivyopo ndani ya mirija hii husukuma kiinitete au yai lililorutubishwa kulipeleka kwenye uterus. Yai lililorutubishwa, au kiinitete, lifikapo kwenye uterus hujipachika katika mojawapo ya kuta zake kwa ajili ya kuendelea kurutubishwa, kukua taratibu na hatimaye kufanya mtoto.

Inapotokea misuli hii kushindwa kufanya kazi au vinyweleo hivi kukosekana, kiinitete hushindwa kusafirishwa kuingia kwenye uterus na hivyo hujitunga nje ya uterus kusababisha ectopic pregnancy. Karibu asilimia 1-2% ya mayai yaliyorutubishwa hutunga nje ya mfuko wa uzazi wa mwanamke.

Aidha, zaidi ya asilimia 95% ya mimba zinazotunga nje ya uterus hutokea kwenye mrija wa fallopian. Mimba zinazotunga kwenye mrija wa fallopian husababisha kiinitete (embryo) kujipachika katika kuta zake na hivyo kusababisha mishipa ya damu inayopita karibu na mrija wa fallopian kupasuka na damu kutoka kwa wingi hali ambayo isiposhughulikiwa mapema husababisha madhara zaidi na hata kifo.

Aina za Ectopic Pregnancy

Kuna aina kuu nne za mimba zinazotunga nje ya mfuko wa uzazi, nazo ni

1. Mimba zinazotunga kwenye mirija ya fallopian

2. Mimba zinazotunga nje ya uterus na nje mirija ya fallopian
3. Mimba zinazotunga ndani na nje ya uterus kwa wakati mmoja
4. Mimba zinazojirudia kutunga nje ya mfuko wa Uzazi

Mimba zinazotunga kwenye mirija ya fallopian

Sababu kubwa inayopelekea mimba kutunga kwenye mirija ya fallopian ni kushindwa kusafirishwa kwa kiinitete katika mirija hii hali inayotokana na mabadiliko katika hali ya mirija au uwezo duni wa mirija hiyo katika kusukuma kiinitete kuingia kwenye uterus kwa sababu ya ukosefu wa vinyweleo kutokana na magonjwa mbalimbali yanayoathiri muundo na maumbile ya mirija ya fallopian.

Mimba zinazotunga kwenye mirija ya fallopian huwa zina madhara makubwa zaidi kwa sababu eneo hili ni jembamba mno kuweza kuhimili ukuaji wa mimba na pia lina mishipa mingi ya damu inayopita karibu ambayo ipo hatarini kupasuka hivyo kupelekea mgonjwa kupoteza damu nyingi sana.

Mimba zinazotunga nje ya uterus na nje mirija ya fallopian

Baadhi ya mimba huweza kutunga kwenye kiwanda cha kuzalisha mayai (o***y), kwenye shingo ya uzazi (cervix) au ndani ya tumbo (intra-abdominal). Aina hii ya mimba ni chini ya asilimia tano ya mimba zote zinazotunga nje ya mfuko wa uzazi.

Mimba inayotungwa ndani ya tumbo (intra-abdominal) wakati fulani huweza kutoa mtoto aliye hai tofauti na aina nyingine za mimba zinazotunga nje ya uterus. Hata hivyo uzalishaji wake hufanywa kwa operesheni ingawa hakuna ushahidi wa kitabibu kuhusu suala hili mpaka sasa.

Madhara ya kutokea kwa upotezaji wa damu pamoja na maambukizi ni makubwa hivyo mara nyingi mimba za namna hii huitaji kushughulikiwa haraka ili kumuepushia madhara makubwa mama mjamzito.

Mimba zinazotunga ndani na nje ya uterus kwa wakati mmoja

Wakati fulani, mayai mawili yaliyorutubishwa kwa wakati mmoja hutokea kupandikizwa sehemu mbili tofauti. Moja likipandikizwa nje ya uterus na jingine ndani ya uterus. Katika aina hii ya ectopic pregnancy, uwezekano wa yai lililotungwa ndani ya uterus kukua na kutoa mtoto ni mkubwa sana.

Mimba zinazojirudia kutunga nje ya mfuko wa Uzazi

Wakati fulani hutokea kuwa, hata baada ya operesheni ya kuondoa mimba iliyotunga nje ya kizazi kufanyika, baada ya muda fulani seli za kiinitete huendelea kukua na kujitengeneza tena kufanya kusanyiko la seli k**a mimba nyingine. Hali hii huitwa mimba zinazoendelea kutunga nje ya mfuko wa uzazi au persistent ectopic pregnancy.

Nini husababisha mimba kutunga nje ya kizazi?

Katika mimba nyingi zinazotunga nje ya uterus, chanzo chake huwa hakijulikani. Hata hivyo kuna vihatarishi ambavyo humfanya mwanamke kuwa katika hatari ya kupata tatizo hili. Vihatarishi hivi ni pamoja na

1. Matatizo katika mirija ya fallopian

Magonjwa yanayoweza kusababisha hali hii ni pamoja na

Maambukizi katika mfumo wa uzazi wa mwanamke (PID)
Matumizi ya vitanzi vya kuzuia mimba (Intra-uterine contraceptive devices)
Kuoteana kwa tishu za uterus kwenye viungo vingine vya uzazi au endometriosis.
2. Uvutaji sigara

Uvutaji sigara kwa mwanamke una uhusiano mkubwa na utungaji wa mimba nje ya kizazi. Imeonekana kwamba wanaowake wanaopendelea kuvuta sigara mara kwa mara wana hatari ya kupatwa na tatizo hili mara tano zaidi ya wale wasiovuta kabisa. Hali hii husababishwa na nicotini iliyomo ndani ya tumbaku. Kwa kawaida nicotini huchochea kusinyaa kwa mirija ya fallopian hali iletayo kuziba kwa mirija hiyo na hivyo kufanya kiinitete kushindwa kupita kwenye mirija kuingia kwenye uterus na kufanya mimba kutunga kwenye mirija ya fallopian.

3. Upasuaji wa tumbo uliofanyika zamani

Operesheni yeyote inayohusu mirija ya fallopian inaongeza uwezekano wa mwanamke kutunga mimba nje ya uterus kwa vile mirija ya fallopian huwa imesinyaa kutokana na operesheni hiyo.

4. Matumizi holela ya baadhi ya dawa

Matumizi ya baadhi ya dawa zenye homoni husababisha kupungua kwa uwezo wa mirija ya fallopian kusukuma kiinitete kuelekea kwenye uterus na hivyo kuleta uwezekano wa utungaji wa mimba nje ya kizazi. Dawa hizo ni k**a dawa za kuzuia mimba zenye homoni za k**e za progesterone, na dawa za kusaidia uzazi aina ya clomiphene.

Dalili za ectopic pregnancy

Katika wiki za mwanzo za ujauzito, mimba iliyotunga nje ya uterus huwa na dalili sawa na za mimba ya kawaida. Dalili hizi ni pamoja na mwanamke kukosa hedhi, kujaa kwa matiti, kichefuchefu, na uchovu wa mwili. Hali hii hufanya ugunduzi wa mimba iliyotunga nje ya uterus kuwa mgumu katika hatua zake za awali.

Hata hivyo dalili ya awali ya kuonesha kuwa mimba imetunga nje ya kizazi ni kuwepo kwa maumivu makali na damu kutoka ukeni. Maumivu yanaweza kuwa kwenye nyonga, tumbo au wakati mwingine kwenye mabega au shingo (iwapo kiwango cha damu inayotoka kwenye mirija iliyopasuka ni kingi sana mpaka kugusa kiwambo cha hewa).

Maumivu haya huweza kuwa makali na yanayokata k**a kisu, na yanaweza kuwa upande mmoja zaidi wa nyonga ingawa si lazima yawe upande ulio na mimba.

Dalili nyingine ni pamoja na

Kizunguzungu na kuzimia kwa sababu ya kupoteza damu kwa wingi
Shinikizo la damu kuwa chini, na
Maumivu ya chini ya mgongo
Ugunduzi wa ectopic pregnancy

Mimba iliyotungwa nje ya kizazi huweza kugunduliwa kwa

Daktari kusikiliza historia ya mgonjwa na kufahamu dalili zake na kumfanyia uchunguzi wa mwili (physical examination).
Kufanya vipimo kadhaa vinavyoonesha kuwepo kwa tatizo hilo. Vipimo hivyo ni pamoja na
Kupima damu kwa ajili ya kuangalia kiwango cha homoni ya HCG
Kupima kiwango cha homoni ya progesterone ambayo kwa mama mwenye ectopic pregnancy huwa chini (chini ya 15ng/mls) zaidi ya mwenye mimba ya kawaida.
Ultrasound ambayo husaidia kutambua mimba ilipotungwa.
Matibabu ya Ectopic pregnancy

Matibabu ya mimba iliyotunga nje ya kizazi yaweza kuwa ya aina mbili, yale yasiyohitaji upasuaji, au yanayohitaji uangalizi na dawa na yale yanayohitaji upasuaji.

1. Matibabu kwa kutumia dawa:

Faida kubwa ya kufanya uchunguzi mapema ni kuwa inaongeza uwezekano wa kuokoa maisha ya mama, kuokoa mirija isipasuke na hivyo kuongeza uwezekano wa kupata mimba kwa njia ya kawaida siku za usoni. Iwapo, mimba bado ni ndogo sana na kiwango cha HCG bado kipo chini mno, daktari anaweza kushauri kusubiri huku akimfuatilia mgonjwa kwa ukaribu sana. Wakati mwingine, mwili huwa na uwezo wa kuifyonza mimba changa ndani kwa ndani na hivyo kuondoa hatari ya kuwepo kwa ectopic pregnancy.

Hali kadhalika, mama anaweza kupewa dawa aina ya methotrexate, ambayo ina uwezo wa kuzuia mimba kukua zaidi. Wakati dawa hii inapotolewa, ni muhimu pia kufuatilia kiwango cha HCG ili kujiridhisha kuwa kimeshuka mpaka kufikia sifuri ili kuwa na uhakika kuwa mimba haipo tena.

Baadhi ya madaktari pia hutumia njia ya kuchoma dawa ya sumu ya potassium chloride kwenye mimba ili kuifanya isinyae na hatamaye kufyonzwa na mwili. Matibabu haya hufanyika chini ya uangalizi wa kipimo cha ultrasound.

2. Matibabu kwa kutumia upasuaji

Iwapo mrija tayari umepasuka, upasuaji wa dharura hufanyika kwa ajili ya kuzuia kupotea zaidi kwa damu. Sehemu ya mrija iliyopasuka huondolewa na mshipa wa damu uliopasuka hufungwa. Athari za matibabu kwa njia hii ni kuwa, huondoa uwezo wa mrija ulioathirika kupitisha yai tena maishani na hivyo kupunguza uwezekano wa mama kupata mimba siku za usoni.

Njia za kuzuia mimba kutunga nje ya kizazi

Yawezekana kupunguza uwezekano wa mimba kutunga nje ya kizazi kwa kuzuia na kujiepusha na vihatarishi vinavyosababisha hali hiyo. Njia hizo ni k**a

Kujikinga na maambukizi katika mfumo wa uzazi wa mwanamke kwa kujiepusha na ngono zembe, au kupunguza idadi ya wapenzi wa kufanya nao ngono.
Kuacha kutumia holela dawa za homoni bila kupata ushauri wa daktari, na
Kujiepusha na uvutaji wa sigara.

Source. Jamii forum.

Address

Magogoni
Zanzibar

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Dr. Abounabil posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram